USIENDE KUULIZA JAMBO LAKO KWA BAAL-ZEBUBU.

 

Na Mwl Peter Mabula 
Mtenda Kazi katika Shamba la MUNGU Mwenyezi 

Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe rafiki.

Karibu Tujifunze Neno la MUNGU.


◼️Usiende kamwe kuuliza jambo lako kwa baal-zebubu.


◾Baal zebubu nini?


➡️Baal-zebubu ni neno linalotokana na maneno mawili ya baal na zebubu.


➡️Baal ni miungu ambayo waabudu shetani walikuwa wanaisujudia na Zebubu ni makao makuu.


➡️Baal-zebubu ni miungu ambayo wafilisti walikua wanaiabudu.


➡️Waisraeli kuita baal-zebubu iliwasumbua wakaita baali-zebuli ilikuwa ina maana ya shetani.


◼️Hivyo Mteule wa KRISTO hutakiwi kamwe kuuliza jambo lako kwa mawakala wa shetani wa namna yeyote kama waganga wa kienyeji au mapepo.

Mtu mmoja alikosea akaenda kuuliza kwa Baal-zebuli badala ya kwenda kuuliza kwa MUNGU ikapelekea kifo chake.


2 Wafalme 1:3 "Lakini malaika wa BWANA akamwambia Eliya Mtishbi, Ondoka, uende ukaonane na wale wajumbe wa mfalme wa Samaria, ukawaambie, Je! Ni kwa sababu hapana MUNGU katika Israeli, hata mnakwenda kuuliza kwa Baal-zebubu, mungu wa Ekroni?"


➡️Hivyo baal-zebubu au baal-zebuli au miungu mingine yote ni miungu iliyo kinyume na MUNGU wa Mbinguni.


➡️Kuna hadi watumishi wa miungu hii naweza kusema watu hao ni watu waliojitoa ufahamu.


Mfano ni huu 


1 Wafalme 18:26 "Wakamtwaa yule ng'ombe waliyepewa, wakamtengeza, wakaliitia jina la Baali tangu asubuhi hata adhuhuri, wakisema, Ee Baali, utusikie. Lakini hapakuwa na sauti, wala aliyejibu. Nao wakaruka-ruka juu ya madhabahu waliyoifanya."


◼️Sasa kiini cha ujumbe wangu ni hiki.


◼️Haipaswi kamwe Mteule wa KRISTO Kwenda kuuliza jambo lako kwa miungu ya aina yoyote ile.


➡️Ahazia badala ya kuuliza kwa MUNGU yeye alienda kumuuliza baal-zebubu jambo hilo lilimchukiza MUNGU sana akamtuma eliya Nabii kumtangazia kifo.


2 Wafalme 1:2 "Na Ahazia akaanguka katika dirisha la chumba chake orofani, katika Samaria, akaugua; akatuma wajumbe, akawaambia, Enendeni mkaulize kwa Baal-zebubu, mungu wa Ekroni, kwamba nitapona ugonjwa huu."


➡️Huyu mtu baada ya kupata tatizo la kuanguka akaumia akaamua Kwenda kuuliza kwa miungu na sio kwa MUNGU kitendo hicho kilisababisha madhara Zaidi kwake.


➡️Huyu alikufa kwa sababu alienda kuulizia kwa shetani na sio kwa MUNGU wa Mbinguni.


◼️Hii inatufundisha kwamba Wewe Mteule wa KRISTO hutakiwi kamwe Kwenda kuuliza lolote kwa waganga wa kienyeji.


◼️Hutakiwi kuuliza mambo yako kwa wanajimu.


◼️Hutakiwi kuuliza  mambo yako kwa manabii wa uongo ambao ni manabii wa shetani.


 ◼️Ni kosa kubwa sana Wewe umeokoka lakini unaenda kuuliza kwa waganga.


➡️Kuna watu huuliza je nitapona, je nitaingia katika ndoa, je nitapata hiyo kazi n.k


◼️Hayo unaweza ukauliza kwa MUNGU na ukapata majibu.


➡️Ukienda kuuliza kwa shetani umefuata maangamizi Yako kama ahazia.


2 Wafalme 1:16-17  "Akamwambia, BWANA asema hivi, Kwa kuwa umetuma wajumbe waulize kwa Baal-zebubu, mungu wa Ekroni, je! Ni kwa sababu hapana MUNGU katika Israeli, uulize neno lake? Kwa hiyo hutashuka katika kile kitanda ulichokipanda, bali hakika utakufa. Basi akafa, sawasawa na neno la BWANA alilolinena Eliya. Na Yoramu alianza kutawala mahali pake katika mwaka wa pili wa Yehoramu mwana wa Yehoshafati mfalme wa Yuda; kwa kuwa yeye hakuwa na mwana."


◼️Ndugu uliyeokoka Jifunze kuuliza mambo Yako kwa MUNGU kupitia ROHO MTAKATIFU na sio vinginevyo, waulize Watumishi waaminifu wa Bwana YESU KRISTO watakusaidia.


◼️Ndugu, Uwe kama Yehoshafati aliyeuliza kwa MUNGU na sio kwa mawakala wa shetani.


2 Wafalme 3:11 "Lakini Yehoshafati akasema, Je! Hapana hapa nabii wa BWANA, ili tumwulize BWANA kwa yeye? Akajibu mtumishi mmoja wa mfalme wa Israeli, akasema, Yupo hapa Elisha mwana wa Shafati, aliyekuwa akimimina maji juu ya mikono yake Eliya."


◼️ Ndugu, Uwe kama Daudi aliyeuliza kwa MUNGU na sio kwa Baal-zebuli.


1 Samweli 23:2 "Basi Daudi akamwuliza BWANA, kusema, Je! Niende nikawapige hao Wafilisti? Naye BWANA akamwambia Daudi, Nenda ukawapige Wafilisti, na kuuokoa Keila."


◼️Ndugu, Uwe kama Rebeka aliyeuliza kwa MUNGU na sio kwa waganga wa kienyeji.


Mwanzo 25:22 "Watoto wakashindana tumboni mwake. Naye akasema, Ikiwa ni hivi, kuishi kwanifaa nini? Akaenda kumwuliza BWANA."


◼️ Ndugu, Uwe kama mitume walimwiliza Bwana YESU KRISTO na sio kuuliza kwa miungu.


Matendo  1:6 "Basi walipokutanika, wakamwuliza, wakisema, Je! Bwana, wakati huu ndipo unapowarudishia Israeli ufalme?"


➡️Achana na wasoma nyota, waganga, wenye mapepo ya utambuzi wale wanajimu.


Asante kwa kujifunza Neno la MUNGU la  siku ya leo, Kabla sijamaliza nakuomba Wewe ambaye hujaokoka au uliokoka ukarudi nyuma, nakusihi sana amua Leo kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi wako na Jina lako litaandikwa katika kitabu Cha uzima Mbinguni, katika maeneo Yako tafuta Kanisa safi la kiroho linalohubiri Wokovu wa KRISTO YESU nenda kamweleze Mchungaji atakuongoza Sala ya Toba utaokoka Kisha baada ya hapo fuata mafundisho ya Neno la MUNGU hapo Kanisani.

MUNGU wa Mbinguni akubariki sana.

By Mwl Peter Mabula 

Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.

+255714252292 ( kwa Ushauri, maombezi,  pamoja na Whatsapp)

Ubarikiwe.

Comments