WAHESHIMU WATUMISHI WA MUNGU .

 

Na Mwl Peter Mabula 
Mtenda kazi katika Shamba la MUNGU Mwenyezi 

Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe rafiki 

Karibu Tujifunze Neno la MUNGU.
➡️Ukisoma Waebrania 5:4 Biblia inasema "Na hapana mtu ajitwaliaye mwenyewe heshima hii, ila yeye aitwaye na MUNGU, kama vile Haruni."

◼️Kumbe hakuna Mtu anayejipangia ili awe Mtumishi wa MUNGU wa kweli katika KRISTO YESU bali Mtumishi wa kweli huchaguliwa na MUNGU Mwenyewe.

◼️Watumishi wa MUNGU huitwa na MUNGU mwenyewe katika KRISTO YESU ili wamtumikie .

◼️Watumishi wa kweli hawakujipangia ili wawe Watumishi bali Bwana YESU mwenyewe aliwatafuta akawaita ili wamtumikie 

➡️Mfano hai  ni Mitume ambapo ni Bwana YESU KRISTO mwenyewe ndiye aliyewatafuta na kuwaita ili wamtumikie, hawakujichagua wenyewe.

Marko 1:16-20 " Naye alipokuwa akipita kando ya bahari ya Galilaya, akamwona Simoni na Andrea nduguye, wakitupa jarife baharini; kwa maana walikuwa wavuvi. YESU akawaambia, Njoni mnifuate, nami nitawafanya kuwa wavuvi wa watu. Mara wakaziacha nyavu zao, wakamfuata. Akaendelea mbele kidogo, akamwona Yakobo wa Zebedayo, na Yohana nduguye, nao pia walikuwa chomboni, wakizitengeneza nyavu zao. Mara akawaita, wakamwacha baba yao Zebedayo ndani ya chombo pamoja na watu wa mshahara, wakaenda, wakamfuata."

➡️Watu hawa walikuwa na kazi zao lakini YESU akawafuata na kuwaita wamtumikie.

➡️Sasa inawezekana kuna Mtumishi unamfahamu lakini hujui malengo ya Maisha yake  mwanzo yalikuwa yapi,  lakini YESU alipomwita akatii kwa sasa anamtumikia MUNGU katika mazingira yote.

➡️Ujumbe wangu leo waheshimu Wachungaji na Watumishi wa kweli wa Bwana YESU KRISTO wanaomtumikia MUNGU.
Na anayetaka Watu hawa waheshimiwe sio Mimi Bali ni Neno la MUNGU wa Mbinguni.

1 Wathesalonike 5:12-13 " Lakini, ndugu, tunataka mwatambue wale wanaojitaabisha kwa ajili yenu, na kuwasimamia ninyi katika BWANA, na kuwaonyeni; mkawastahi sana katika upendo, kwa ajili ya kazi zao. Iweni na amani ninyi kwa ninyi."

➡️Biblia inatutaka tuwastahi sana yaani tuwaheshimu sana, Neno "Kustahi" kwenye kamusi ya kiswahili sanifu Lina maana ya "Kumheshimu Mtu"
   
➡️Wakati mwingine Watumishi wa MUNGU wanajitaabisha sana kwa ajili ya wengine ili waokolewe au wafunguliwe au wawe huru dhidi ya Nguvu za giza n.k
Ndugu, hawa inatupasa kuwheshimu.

1 Timotheo 5:17 "Wazee watawalao vema na wahesabiwe kustahili heshima maradufu; hasa wao wajitaabishao kwa kuhutubu na kufundisha."

◼️Andiko hilo katika tafasiri rahisi Lina maana kwamba Viongozi wa Kikanisa wanastahili heshima hasa wale ambao huhubiri na kufundisha Neno la MUNGU, tafasiri hii Iko katika Tafasiri ya Biblia ya BHN unaweza ukaiangalia.
Kumbe Wahubiri na Wafundishaji wa Neno la MUNGU wanastahili kuheshimiwa, na hilo ni kusudi la MUNGU.

➡️Sina maana uwanyenyekee Watumishi wa MUNGU bali maana yangu uwape heshima wanayoistahili.

➡️Nayasema haya kwa sababu Moja ya watu wanaoongoza kusema vibaya bila sababu, kuonewa, kutukanwa n.k ni pamoja na Watumishi wa MUNGU wa kweli.
Nikupe Mfano mmoja ambao Mimi ulinikuta kati ya mingi ila naomba eileweke sisemi haya ili kutafuta heshima Bali ni sehemu ya somo.
siku Moja nilifundisha somo la misingi ya Ndoa Kibiblia Kuna baba mmoja alinitukana kwa hasira kwa sababu Ndoa yake ilikuwa na migogoro na alikuwa ametengana na Mke wake hivyo hakunielewa niliposema habari ya misingi ya Ndoa Kibiblia wakati yeye Ndoa imemshinda.

Siku Moja Kanisa fulani nilifundisha somo la kukemea uasherati, Dada mmoja baada ya somo aliniambia ananichukia akisema "dhambi zote hukuona ila umeona tu uzinzi, wengine hukuwaona umeniona Mimi tu" yeye alidhani nimefundisha kwa sababu yake kumbe Wala Sikuwa najua lolote lile kuhusu yeye.
Mtu wa hivyo anaweza akamchukia Mtumishi wa MUNGU na hata anaweza kwa hasira kuanza vita na Mtumishi kwa kumsema vibaya kwa uongo mbele ya watu, hivyo Watumishi wa kweli wa MUNGU katika KRISTO YESU wakati Mwingine kuchukiwa bila kosa ni kawaida tu.

➡️Ndugu unaweza kupata madhara makubwa kwa kuwatukana Watumishi waaminifu wa Bwana  YESU na Wewe  kutoka katika madhara hayo ni hadi wao wakuombee  wao.

➡️Unaweza kupata ukoma kama Miriamu kwa kumsema vibaya  Musa.

Hesabu 12:1-2 " Kisha Miriamu na Haruni wakamnenea Musa kwa sababu ya mwanamke Mkushi aliyekuwa amemwoa; maana, alikuwa amemwoa mwanamke Mkushi. Kisha hilo wingu likaondoka kutoka pale juu ya hema; na tazama, Miriamu akawa mwenye ukoma, mweupe kama theluji; Haruni akamwangalia Miriamu, na tazama, yu mwenye ukoma."

◼️Ndugu, waheshimu Watumishi wa MUNGU katika KRISTO YESU Kwa heshima ya ki MUNGU, wastahi na usiwatangazie uongo.

Asante kwa kujifunza Neno la MUNGU la  siku ya leo, Kabla sijamaliza nakuomba Wewe ambaye hujaokoka au uliokoka ukarudi nyuma, nakusihi sana amua Leo kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi wako na Jina lako litaandikwa katika kitabu Cha uzima Mbinguni, katika maeneo Yako tafuta Kanisa safi la kiroho linalohubiri Wokovu wa KRISTO YESU nenda kamweleze Mchungaji atakuongoza Sala ya Toba utaokoka Kisha baada ya hapo fuata mafundisho ya Neno la MUNGU hapo Kanisani.
MUNGU wa Mbinguni akubariki sana.
By Mwl Peter Mabula 
Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292 ( kwa Ushauri, maombezi,  pamoja na Whatsapp)
Ubarikiwe.   
                           

Comments