![]() |
| Na Mwl Peter Mabula Mtenda kazi katika Shamba la MUNGU Mwenyezi |
Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe rafiki.
Karibu Tujifunze Neno la MUNGU.
◼️Maombi yana nguvu sana na leo tunaenda kuomba Maombi yakuleta.
➡️Ni baada ya kujifunza Neno hili la MUNGU la Ufunuo wa ROHO MTAKATIFU.
◼️Kuna vitu hushindikana kwa njia zote na kusubili Maombi tu.
Marko 9:29 "Akawaambia, Namna hii haiwezi kutoka kwa neno lo lote, isipokuwa kwa kuomba."
◾Ngoja nikufundishe kwa mifano namna Maombi yalivyoleta.
✔️✔️Maombi yalimleta samweli.
1 Samweli 1:10 "Naye huyo mwanamke alikuwa na uchungu rohoni mwake, akamwomba BWANA akalia sana."
➡️Hannah alikuwa na uchungu sana kwa sababu ya kukosa Mtoto katika Ndoa yake kwa miaka mingi, akaijua Siri kwa vingine vitaletwa na Maombi tu hivyo akawa muombaji.
Siku Moja wakati akiomba Mtumishi wa MUNGU akamuona na kumtamkia baraka na baraka ile ikawa kama alivyotamka yule Mtumishi wa MUNGU hivyo Maombi ya Hannah yamleta Nabii Samweli ambaye alikuja kuwa Mtu mkuu sana.
1 Samweli 1:17-18 "Ndipo Eli akajibu, akasema, Enenda kwa amani; na MUNGU wa Israeli akujalie haja yako uliyomwomba.
Naye akasema, Mjakazi wako na aone kibali machoni pako. Basi huyo mwanamke akaenda zake, naye akala chakula, wala uso wake haukukunjamana tena. Wakaondoka asubuhi na mapema, wakasali mbele za BWANA, kisha wakarejea na kufika nyumbani kwao huko Rama; Elkana akamjua mkewe Hana; naye BWANA akamkumbuka. Ikawa, wakati ulipowadia, Hana akachukua mimba na kuzaa mtoto mwanamume; akamwita jina lake Samweli, akisema, Kwa kuwa nimemwomba kwa BWANA."
➡️Ili Maombi yalete Samweli ilibidi Maombi yafanye kazi nyingi ikiwemo kuondoa utasa, Maombi kusababisha mimba kutungwa, kumlinda kumlinda Mtoto tumboni na Mama kujifungua salama, hiyo ni kazi aliyoifanya MUNGU baada ya Maombi ya Hannah na Kuhani.
◼️Maombi yanaweza kuleta mwenzi, mtoto, kazi, uponyaji n.k
◼️Maombi Yako katika Jina la YESU KRISTO yanaweza kumleta Samweli wako.
Mimi Peter Mabula simjui Samweli wako ambaye Wewe rafiki yangu unamhitaji sana.
Inawezekana Samweli wako Wewe ni kupata kazi au kujenga nyumba.
Inawezekana Samweli wako Wewe ni kupona ugonjwa au kuzaa katika Ndoa Yako n.k
Katika Jina la YESU KRISTO Ukiomba yote yanawezekana.
◾Mfano wa pili ni huu
✔️✔️Maombi yalimtoa Petro gerezani.
Matendo 12:4-9 " Alipokwisha kumkamata, akamweka gerezani akamtia mikononi mwa vikosi vinne vya askari wanne wanne, wamlinde, akitaka baada ya Pasaka kumtoa na kumweka mbele ya watu. Basi Petro akalindwa gerezani, nalo kanisa likamwomba MUNGU kwa juhudi kwa ajili yake. Hata wakati Herode alipotaka kumtoa, usiku ule ule Petro alikuwa analala katikati ya askari wawili, amefungwa minyororo miwili; walinzi mbele ya mlango wakailinda gereza. Mara malaika wa BWANA akasimama karibu naye, nuru ikamulika mle chumbani, akampiga Petro ubavuni, akamwamsha, akisema, Ondoka upesi. Minyororo yake ikamwanguka mikononi. Malaika akamwambia, Jifunge, kavae viatu vyako. Akafanya hivyo. Kisha akamwambia, Jivike nguo yako, ukanifuate. Akatoka nje, akamfuata; wala hakujua ya kuwa ni kweli yaliyofanywa na malaika; bali alidhani kwamba anaona maono."
➡️Nani yuko kwenye gereza la kiroho unataka atoke?
Leo omba kwa Imani katika Jina la YESU KRISTO Mwokozi maana Maombi yanaweza kumtoa Mtu gerezani.
◼️Neno la MUNGU linatuhakikishia kwamba yeyote tutakayoomba kwa Imani tukiamini yatakuwa hivyo hivyo kama tulivyoomba.
Mathayo 21:22 "Na yo yote mtakayoyaomba katika sala mkiamini, mtapokea."
◼️Kama ulikuwa hujui ni kwamba Maombi yanaweza yakamleta Mtoto wako wewe unayehitaji Mtoto katika ndoa yako.
◼️Maombi yanaweza kuleta Kazi unayotaka katika kusudi la MUNGU Wewe unayehitaji kazi.
◼️Maombi yanaweza kumleta Mume au Mke wewe mwanaume au mwanamke unayehitaji Ndoa takatifu.
◼️Maombi yanaweza yakaleta kibali unachohitaji katika jamii, ndoa, familia, idara n.k
◼️Mtukuze tu MUNGU anapokutendea.
✔️✔️Maombi yana nguvu sana.
Waefeso 6:18 "kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika ROHO, mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote;"
◾Mfano wa tatu.
✔️✔️Kumbuka Maombi yalimleta Malaika ili atatue tatizo kwa Mtu wa MUNGU.
Mwanzo 21:17 "MUNGU akasikia sauti ya kijana. Malaika wa MUNGU akamwita Hajiri kutoka mbinguni, akamwambia, Una nini, Hajiri? Usiogope, maana MUNGU amesikia sauti ya kijana huko aliko."
◼️MUNGU husikia maombi.
1 Wafalme 9:3 "BWANA akamwambia, Nimeyasikia maombi yako na dua zako, ulizotoa mbele zangu. Nimeitakasa nyumba hii uliyoijenga ili niweke jina langu humo milele; tena macho yangu na moyo wangu utakuwapo hapo siku zote;"
◾Mfano wa nne.
✔️✔️Maombi ya Hezekia yalileta ongezeko la miaka kwake.
2 Wafalme 20:5-6 " Rudi, ukamwambie Hezekia, mkuu wa watu wangu, BWANA, Mungu wa Daudi baba yako asema hivi, Nimeyasikia maombi yako, na kuyaona machozi yako; tazama, nitakuponya; siku ya tatu utapanda nyumbani kwa BWANA. Tena, nitazizidisha siku zako, kiasi cha miaka kumi na mitano, nami nitakuokoa wewe, na mji huu, na mkono wa mfalme wa Ashuru, nami nitaulinda mji huu kwa ajili yangu, na kwa ajili ya Daudi, mtumishi wangu."
◼️Hezekia ilikuwa afe lakini Maombi yake yalileta miaka 15 ya kuendelea kuishi.
Hata kwako Inawezekana katika Jina la YESU KRISTO ukaomba na Maombi yakaleta kitu unachohitaji.
✔️✔️Leo Omba kwa Imani Maombi yanayoleta ushindi wako, wakumbuka hata akina Sulemani na Eliya ambao Maombi yao yalishusha moto toka mbinguni.
✔️Sulemani kuomba moto ukashuka kutoka Mbinguni imeandikwa hapa.
2 Nyakati 7:1 "Basi Sulemani alipokwisha maombi hayo, moto ukashuka kutoka mbinguni, ukateketeza sadaka ya kuteketezwa na dhabihu; utukufu wa BWANA ukaijaza nyumba."
✔️Eliya kuomba Maombi ya kushusha moto kutoka Mbinguni imeandikwa hapa.
2 Wafalme 1:10 "Eliya akajibu, akamwambia yule akida wa hamsini, Ikiwa mimi ni mtu wa MUNGU, na ushuke moto kutoka mbinguni, ukuteketeze wewe na hamsini wako. Moto ukashuka, ukamteketeza, yeye na hamsini wake."
✔️Na sehemu nyingine ni hii
1 Wafalme 18:37-39 " Unisikie, Ee BWANA, unisikie, ili watu hawa wajue ya kuwa wewe, BWANA, ndiwe Mungu, na ya kuwa wewe umewageuza moyo wakurudie.
Ndipo moto wa BWANA ukashuka, ukaiteketeza sadaka ya kuteketezwa, na kuni, na mawe, na mavumbi, ukayaramba yale maji yaliyokuwamo katika mfereji. Na watu wote walipoona, wakaanguka kifudifudi; wakasema, BWANA ndiye Mungu, BWANA ndiye Mungu."
Ndugu hata Leo katika Jina la YESU KRISTO unaweza ukaomba kushusha moto dhidi ya Nguvu za giza zinazokutesa na baada ya hapo hazitakutesa Tena.
◼️Leo katika Jina la YESU KRISTO Omba leo maombi yanayoleta kitu unachohitaji.
◾Nini ufanye ?
1. Tubia dhambi na amua kuziacha ili kuruhusu msaada wa MUNGU kuja kwako.
Yeremia 14:20 "Ee BWANA, tunakiri uovu wetu, na ubaya wa baba zetu; maana tumekutenda dhambi."
2. Omba kwa Imani isiyo yumba juu ya yale unayotaka yawe .
Mathayo 17:20 "YESU akawaambia, Kwa sababu ya upungufu wa imani yenu. Kwa maana, amin, nawaambia, Mkiwa na imani kiasi cha punje ya haradali mtauambia mlima huu, Ondoka hapa uende kule; nao utaondoka; wala halitakuwako neno lisilowezekana kwenu."
3. Tumia Mamlaka ya jina la YESU KRISTO kuamuru unachohitaji kwa njia ya Maombi.
Luka 10:19 "Tazama, nimewapa amri ya kukanyaga nyoka na nge, na nguvu zote za yule adui, wala hakuna kitu kitakachowadhuru."
4. Msikilize ROHO MTAKATIFU katika Maombi.
Yuda 1:20 "Bali ninyi, wapenzi, mkijijenga juu ya imani yenu iliyo takatifu sana, na kuomba katika ROHO MTAKATIFU,"
Asante kwa kujifunza Neno la MUNGU la siku ya leo, Kabla sijamaliza nakuomba Wewe ambaye hujaokoka au uliokoka ukarudi nyuma, nakusihi sana amua Leo kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi wako na Jina lako litaandikwa katika kitabu Cha uzima Mbinguni, katika maeneo Yako tafuta Kanisa safi la kiroho linalohubiri Wokovu wa KRISTO YESU nenda kamweleze Mchungaji atakuongoza Sala ya Toba utaokoka Kisha baada ya hapo fuata mafundisho ya Neno la MUNGU hapo Kanisani.
MUNGU wa Mbinguni akubariki sana.
By Mwl Peter Mabula
Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292 ( kwa Ushauri, maombezi, pamoja na Whatsapp)
Ubarikiwe.

Comments