WATU 8 WANAOMTUKUZA MUNGU.

 

Na Mtumishi wa MUNGU Peter Mabula.
Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi 

Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe rafiki.
Karibu Tujifunze Neno la MUNGU wa Mbinguni.

Malaki 2:2 "Kama hamtaki kusikia, na kama hamtaki kuitia moyoni, ili kulitukuza jina langu, asema BWANA wa majeshi, basi nitawapelekeeni laana, nami nitazilaani baraka zenu; naam, nimekwisha kuzilaani, kwa sababu hamyatii haya moyoni."

◼️Kuna Watu wengi wanamtukuza MUNGU, Mimi sijui kama na Wewe ni mmoja wao, lakini ni jambo jema Mtu kumtukuza MUNGU wa Mbinguni. 

Isaya 25:1 "Ee BWANA, wewe u MUNGU wangu; Nitakutukuza na kulihimidi jina lako; Kwa kuwa umetenda mambo ya ajabu, Mashauri ya kale, kwa uaminifu na kweli."

➡️Kumtukuza MUNGU ni kufanyaje?

◼️Kumtukuza MUNGU ni kitendo cha kumpa Heshima kuliko wote, ni kukiri na kuonyesha Ukuu wake na Nguvu zake.

Mathayo 15:31 "hata ule mkutano wakastaajabu, walipowaona mabubu wanasema, vilema wanakuwa wazima, viwete wanakwenda, na vipofu wanaona; wakamtukuza MUNGU wa Israeli."

◼️Kumtukuza MUNGU ni kumpa yeye Utukufu wote.
Kumbuka Watu  wenye Imani kubwa humtukuza MUNGU hata kwenye magumu.

 2 Wakorintho 9:13 "kwa kuwa mkijaribiwa kwa utumishi huo, wanamtukuza MUNGU kwa ajili ya utii wenu katika kuikiri Injili ya KRISTO, na kwa ajili ya ukarimu wenu mliowashirikisha wao na watu wote."

➡️Wapo Watu ambao Maandiko yanaonyesha wanamtukuza MUNGU, na wewe rafiki jikague ili uwe kwenye kundi hili bora la Watu wanaomtukuza MUNGU wa Mbinguni.

Zaburi 69:30 "Nitalisifu jina la Mungu kwa wimbo, Nami nitamtukuza kwa shukrani."

➡️ Ndugu Achana na Habari za kutukuza Watu, Wewe Mtukuze MUNGU katika KRISTO YESU. 

◼️Mtukuze Bwana YESU utafanya vyema sana.

Zaburi 50:15 "Ukaniite siku ya mateso; Nitakuokoa, na wewe utanitukuza."

Je Wewe huwa unamtukuza MUNGU?
Inawezekana hata hujui Kumtukuza MUNGU ni kufanyaje?
Niko mahali hapa kukujulisha namna ya Kumtukuza MUNGU na ujue ni watu gani humtukuza MUNGU katika KRISTO YESU ili na Wewe uwe mmoja wao.

◾Watu ambao Wanaomtukuza MUNGU .

1. Unapotendewa Muujiza na YESU KRISTO kisha ukarudi kwa MUNGU kumshukuru hapo unamtukuza MUNGU.

➡️Mfano hai ni huyu aliyeponywa ukoma na Bwana YESU KRISTO.

Luka 17:15-16 " Na mmoja wao alipoona kwamba amepona, alirudi, huku akimtukuza MUNGU kwa sauti kuu; akaanguka kifudifudi miguuni pake, akamshukuru; naye alikuwa Msamaria."

➡️Mfano ukaenda Kanisani ukaombewa ukapona baada ya kupona unarudi pale na kutangaza umekuja kumshukuru MUNGU kwa kukuponya, tendo hilo ni kumtukuza MUNGU.

Matendo  11:18 "Waliposikia maneno haya wakanyamaza, wakamtukuza MUNGU, wakisema, Basi, MUNGU amewajalia hata mataifa nao toba liletalo uzima."

◼️Mtu ambaye ni rahisi sana kumtukuza MUNGU ni Mtu mwenye ROHO MTAKATIFU.

Yohana 16:13-14 " Lakini yeye atakapokuja, huyo ROHO wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake. YEYE ATANITUKUZA MIMI, kwa kuwa atatwaa katika yaliyo yangu na kuwapasha habari."

◼️ Kwa hiyo Mtu yeyote anayeponywa na Bwana YESU Kisha akarudi Kanisani kushukuru huyo ndio anamfukuza MUNGU.

2. Mtu anayetoa Sadaka za shukrani.

Zaburi 50:23 "Atoaye dhabihu za kushukuru, Ndiye anayenitukuza. Naye autengenezaye mwenendo wake, Nitamwonyesha wokovu wa MUNGU."

➡️Mtu yeyote anayetoa sadaka ya shukrani kwa MUNGU kupitia Watumishi wake au Kanisani, tendo hilo la kutoa Sadaka ya shukrani ni tendo la Kumtukuza MUNGU.

◼️Hivyo Mtu anayetoa Sadaka ya shukrani katika KRISTO YESU Mtu huyo anamfukuza MUNGU wa Mbinguni.

3. Unapokubali matendo ya MUNGU.

➡️Mfano hai ni huu

Danieli 4:37 "Basi mimi, Nebukadreza, namhimidi Mfalme wa mbinguni, namtukuza na kumheshimu; maana matendo yake yote ni kweli, na njia zake ni za adili; na wale waendao kwa kutakabari, yeye aweza kuwadhili."

◼️Unapoyakubali matendo ya MUNGU na kuyatangaza kwamba umeyakubali hapo unamtukuza MUNGU.

4. Mtu anayeomba maombi ya Kumshukuru MUNGU .

Zaburi 118:28 "Ndiwe MUNGU wangu, nami nitakushukuru, Ndiwe MUNGU wangu, nami nitakutukuza."

◼️Mtu anayeomba Maombi katika jina la MUNGU wa akimshukuru MUNGU huyo Mtu hapo anamtukuza MUNGU.

5. Unapolipa heshima Neno la MUNGU .

Matendo  13:48 "Mataifa waliposikia hayo wakafurahi, wakalitukuza neno la BWANA, nao waliokuwa wamekusudiwa uzima wa milele wakaamini."

➡️Mfano unapoenda kulisikiliza Neno la MUNGU katika mkutano wa Injili n.k, hapo unakuwa unamtukuza MUNGU.

6. Unapompigia magoti MUNGU au Kumsujudia.

Zaburi 86:9-10 " Mataifa yote uliowafanya watakuja; Watakusujudia Wewe, BWANA, Watalitukuza jina lako; Kwa kuwa ndiwe uliye mkuu, Wewe ndiwe mfanya miujiza, Ndiwe MUNGU peke yako."

 ◼️ Kumsujudia MUNGU wa Mbinguni katika KRISTO YESU ni Kumtukuza.

◼️ Kumpigia magoti MUNGU katika KRISTO YESU ni Kumtukuza.

7. Unapofurahia MUNGU baada ya kuona miujiza aliyowatendea wengine.

Mfano hai ni huu.

Mathayo 9:8 "Makutano walipomwona, walishikwa na hofu, wakamtukuza MUNGU, aliyewapa watu amri ya namna hii."

◼️Unapofurahia Miujiza ambayo MUNGU katika KRISTO YESU amewatendea wengine hapo unamtukuza.

Ayubu 36:24 "Kumbuka kuitukuza kazi yake, Watu waliyoiimbia."

8. Unaposikia Habari njema za MUNGU katika KRISTO YESU ukabarikiwa nazo.

Luka 2:20 "Wale wachungaji wakarudi, huku wanamtukuza MUNGU na kumsifu kwa mambo yote waliyosikia na kuyaona, kama walivyoambiwa."

  ◼️Ukiwa Mtu ambaye unaposikia habari njema za Bwana YESU KRISTO unabarikiwa nazo hapo unakuwa unamtukuza MUNGU aliyezileta hizo habari njema.

◼️Unapozingatia mambo ya MUNGU katika KRISTO YESU hapo unakuwa unamtukuza MUNGU wa Mbinguni.

➡️Je na Wewe uko kwenye Kundi la watu wanaomtukuza MUNGU wa Mbinguni?

◼️Ndugu Hakikisha unakuwa mmoja wao wa watu wanaomtukuza MUNGU wa Mbinguni.
 Asante kwa kujifunza Neno la MUNGU la  siku ya leo, Kabla sijamaliza nakuomba Wewe ambaye hujaokoka au uliokoka ukarudi nyuma, nakusihi sana amua Leo kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi wako na Jina lako litaandikwa katika kitabu Cha uzima Mbinguni, katika maeneo Yako tafuta Kanisa safi la kiroho linalohubiri Wokovu wa KRISTO YESU nenda kamweleze Mchungaji atakuongoza Sala ya Toba utaokoka Kisha baada ya hapo fuata mafundisho ya Neno la MUNGU hapo Kanisani.
MUNGU wa Mbinguni akubariki sana.
By Mwl Peter Mabula 
Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292 ( kwa Ushauri, maombezi,  pamoja na Whatsapp)
Ubarikiwe. 

Comments