Huduma ya Mchungaji Eliza Kihwili yatimiza mwaka mmoja kwa mafanikio.

Kanisa la Pentecostal Asemblies of GOD (PAG)  Vijibweni soweto chini ya mpakwa mafuta wa BWANA Mchungaji Eliza Kihwili limetimiza mwaka mmoja tangu lifunguliwe December Mwaka 2012. Katika ibaada ya shukrani mchungaji Eliza alisema anamshukuru sana MUNGU kwa neema yake licha ya kuanza kwenye mazingira magumu lakini BWANA alitengeneza njia pasipo na njia kwani hadi sasa wanalo eneo la kuabudia, wanavyo vyombo vya mziki na mafaikio mengine ikiwemo kuongezeka kwa waumini kwani walianza  familia moja lakini sana wako zaidi ya 20, na changamoto yao ni ujenzi wa kanisa ambao unahitaji Milioni 20, mpendwa kama ukipenda kuifanya kazi ya MUNGU pamoja na mtumishi huyu basi unaweza kutoa mchango wako kwa kuwasiliana nae kwa namba 0715929231 au wasiliana nami kwa namba 0714252292 na tutakuunganisha moja kwa moja na mchungaji Eliza. zifuatazo ni baadhi ya picha za tukio hilo la ibaada ya shkrani. MUNGU akubariki sana

Beatrice William wengi wananijua kwa jina la Beatrice wa BSS alikuwepo kumtukuza MUNGU


Mchungaji Eliza Kihwili akifundisha katika ibaada hiyo ya shukrani


Baadhi ya waumini

Mchungaji Eliza akihubiri


Kutoka maisha ya ushindi, Scholar Mungusa alikuwepo

Nilivyo hivi ni kwa neema tu ya MUNGU

Kutoka KPC kawe, Mtumishi wa MUNGU Paulo akitoa neno fupi la shukrani kutoka Wafilipi 4:4

Katibu wa kanisa akisema machache kuhusu utaratibu wa ibaada

Kwaya wakimtukuza MUNGU

Kwa YESU panalipa sana

ilikuwa ni shangwe ajabu, Beatrice akiimba wimbo wa  RAFIKI NYOKA



Beatrice akiwajibika kumtukuza MUNGU

K



Bali wote waliompokea(YESU KRISTO) aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa MUNGU, ndio wale waliaminio jina lake; -Yohana 1:12