FAHAMU UWEZO WA DAMU YA YESU KRISTO

MWL. CHRISTOPHER MWAKASEGE AKIFUNDISHA NENO LA MUNGU

DIANA MWAKASEGE AKIWAONGOZA WATU KWENYE KONGAMANO LA MAOMBI

 Siku moja usiku nikiwa katika chumba cha hoteli moja hapa hapa nchini, baada ya kutoka kwenye semina ya kiroho; Roho Mtakatifu alisema ndani ya roho yangu kuwa; “Fundisha juu ya Damu ya Yesu Kristo”.

Tangu wakati huo nimekuwa na maombi ya mara kwa mara, nikiomba Roho Mtakatifu anifundishe juu ya Damu ya Yesu Kristo. Nimekuwa nikisoma na kutafakari neno la Mungu linalofundisha juu ya damu ya Yesu Kristo. Ni muda umepita sasa tangu nipate agizo hili. Ndani ya moyo wangu naona ya kuwa muda umefika wa mimi kuanza kuwashirikisha wenzangu yale ambayo tayari yamo ndani yangu ingawa ni machache, juu ya Damu ya Yesu Kristo.

Katika mfulilizo wa somo hili,tutashirikiana juu ya mambo manne tunayopata katika Damu ya Yesu Kristo. Ukweli ni kwamba katika damu ya Yesu Kristo kunapatikana zaidi ya mambo manne nitakayokushirikisha humu; lakini kwa sasa naona nianze na haya manne:-

1. Uwezo wa Damu ya Yesu Kristo katika kuondoa dhambi. Imeandikwa katika kitabu cha 1Yohana 1:9 kuwa; “Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata ATUONDOLEE dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote”.

2. Uwezo wa Damu ya Yesu Kristo katika kupatanisha. Imeandikwa katika kitabu cha Waefeso 2:13-16 kuwa; “Lakini sasa, katika Kristo Yesu, ninyi mliokuwa mbali hapo kwanza mmekuwa karibu kwa damu yake Kristo. Kwa maana yeye ndiye amanin yetu, aliyetufanya sisi sote tuliokuwa wawili kuwa mmoja; akakibomoa kiambaza cha kati kilichotutenga. Naye akiisha kuuondoa ule uadui kwa mwili wake; ndiyo sheria ya amri zilizo katika maagizo; ili afanye hao wawili kuwa mtu mpya mmoja ndani ya nafsi yake; akafanya amani. AKAWAPATANISHA wote wawili na Mungu katika mwili mmoja, kwa njia ya msalaba, akiisha kuufisha ule uadui kwa huo msalaba”

3. Uzima wa Milele katika Damu ya Yesu Kristo. Imeandikwa katika kitabu cha Yohana 6:53-54 kuwa; “Basi Yesu akawaambia Amini, amini, nawaambieni, msipoula mwili wake mwana wa Adamu nakuinywa damu yake, hamna uzima ndani yenu. Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu anao UZIMA WA MILELE…..”

4. Uwezo wa Damu ya Yesu Kristo katika kutulinda. Imeandikwa katika kitabu cha ufunuo wa Yohana 12:11a kuwa; “Nao wakamshinda (shetani) kwa damu ya mwana-Kondoo….”

Mtihani mkubwa sana kwetu sisi wakristo ni kuyaweka katika matendo yale tunayofahamu katika Biblia. Nakushauri kwa Jina la Yesu Kristo kuwa uwe mtendaji wa neno, na usiwe msomaji tu.

Ni maombi yangu kwa Bwana ya kuwa Roho wa ufahamu wa Bwana atakuwa juu yako. BARIKIWA SANA BY MWL CHRISTOPHER MWAKASEGE

Comments

Unknown said…
HAYA NI MANENO MEMA''NASADIKI KATIKA HILI''EWE YESU NAOMBA USINIPITE
Peter Mabula said…
ubarikiwe sana kaka