Posted by
Peter Mabula
- Get link
- X
- Other Apps
MWL. CHRISTOPHER MWAKASEGE AKIFUNDISHA NENO LA MUNGU |
DIANA MWAKASEGE AKIWAONGOZA WATU KWENYE KONGAMANO LA MAOMBI |
Siku moja usiku nikiwa katika chumba cha hoteli moja
hapa hapa nchini, baada ya kutoka kwenye semina ya kiroho; Roho
Mtakatifu alisema ndani ya roho yangu kuwa; “Fundisha juu ya Damu ya
Yesu Kristo”.
Tangu wakati huo nimekuwa na
maombi ya mara kwa mara, nikiomba Roho Mtakatifu anifundishe juu ya Damu
ya Yesu Kristo. Nimekuwa nikisoma na kutafakari neno la Mungu
linalofundisha juu ya damu ya Yesu Kristo. Ni muda umepita sasa tangu
nipate agizo hili. Ndani ya moyo wangu naona ya kuwa muda umefika wa
mimi kuanza kuwashirikisha wenzangu yale ambayo tayari yamo ndani yangu
ingawa ni machache, juu ya Damu ya Yesu Kristo.
Katika mfulilizo wa somo hili,tutashirikiana juu ya
mambo manne tunayopata katika Damu ya Yesu Kristo. Ukweli ni kwamba
katika damu ya Yesu Kristo kunapatikana zaidi ya mambo manne
nitakayokushirikisha humu; lakini kwa sasa naona nianze na haya manne:-
1. Uwezo wa Damu ya Yesu Kristo katika kuondoa dhambi. Imeandikwa
katika kitabu cha 1Yohana 1:9 kuwa; “Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni
mwaminifu na wa haki hata ATUONDOLEE dhambi zetu, na kutusafisha na
udhalimu wote”.
2. Uwezo wa Damu ya Yesu Kristo katika
kupatanisha. Imeandikwa katika kitabu cha Waefeso 2:13-16 kuwa; “Lakini
sasa, katika Kristo Yesu, ninyi mliokuwa mbali hapo kwanza mmekuwa
karibu kwa damu yake Kristo. Kwa maana yeye ndiye amanin yetu,
aliyetufanya sisi sote tuliokuwa wawili kuwa mmoja; akakibomoa kiambaza
cha kati kilichotutenga. Naye akiisha kuuondoa ule uadui kwa mwili wake;
ndiyo sheria ya amri zilizo katika maagizo; ili afanye hao wawili kuwa
mtu mpya mmoja ndani ya nafsi yake; akafanya amani. AKAWAPATANISHA wote
wawili na Mungu katika mwili mmoja, kwa njia ya msalaba, akiisha
kuufisha ule uadui kwa huo msalaba”
3. Uzima wa Milele
katika Damu ya Yesu Kristo. Imeandikwa katika kitabu cha Yohana 6:53-54
kuwa; “Basi Yesu akawaambia Amini, amini, nawaambieni, msipoula mwili
wake mwana wa Adamu nakuinywa damu yake, hamna uzima ndani yenu. Aulaye
mwili wangu na kuinywa damu yangu anao UZIMA WA MILELE…..”
4.
Uwezo wa Damu ya Yesu Kristo katika kutulinda. Imeandikwa katika
kitabu cha ufunuo wa Yohana 12:11a kuwa; “Nao wakamshinda (shetani) kwa
damu ya mwana-Kondoo….”
Mtihani mkubwa sana kwetu sisi wakristo
ni kuyaweka katika matendo yale tunayofahamu katika Biblia. Nakushauri
kwa Jina la Yesu Kristo kuwa uwe mtendaji wa neno, na usiwe msomaji tu.
Ni maombi yangu kwa Bwana ya kuwa Roho wa ufahamu wa Bwana atakuwa juu
yako. BARIKIWA SANA BY MWL CHRISTOPHER MWAKASEGE
- Get link
- X
- Other Apps
Comments