1Wakorintho 13:4-6{Upendo …haufurahii udhalimu, bali hufurahi pamoja na kweli.}
![]() |
SAMWEL MABULA NA MKEWE HAPPY MASAWE BAADA YA KUFUNGA NDOA |
Neno
KUPENDA, au UPENDO, limekuwa msamiati mgumu sana kwa vijana wa leo,
shetani amefanikiwa kwa asilimia 90 kuwanasa vijana wengi na kuwaangusha
katika dhambi, akitumia msamiati huu NAKUPENDA. Nikiwa katika huduma
zangu za Injili, nilikutana na binti mmoja ambaye alikuwa amezidiwa
kitandani akiwa anaumwa, lakini pia alikuwa mja mzito. Nilipomuuliza
mumewe yuko wapi, akaanza kulia, mwishowe akaeleza kisa cha kusikitisha
jinsi kijana wa kiume alivyomdanganya kuwa anampenda, lakini baada
kutimiza haja yake, akampiga “KIBUTI” hakutaka hata kumuona,
alitelekezwa bila msaada. Vijana
wengi leo hasa wa kike wanaingizwa “CHAKA” wanadanganywa na vijana wa
kiume kwa neno NAKUPENDA, Binti akiambiwa nakupenda, utamuona Macho na
masikio yanaaza kulege, kusema ukweli wengi HAWAPENDI, bali WANATAMANI.
Wengi wamepitia changamoto hiyo ya kuambiwa wanapendwa, lakini baadaye
walijikuta hukana Upendo. Na matatizo ya ndoa nyingi za siku hizi
yanatokana na mwanzo wa mahusiano kuwa ni kukidhi TAMAA ya mwili.
Misukumo na Mihemuko ya Tamaa za NGONO imechukuliwa na Vijana wengi kuwa
ni Upendo. Utakuta kijana wa kiume anaonyesha hisia zote za kupenda,
yuko tayari kukupigia magoti, kukulamba miguu, kukupatia chochote
utakacho, ili mradi akuonyeshe kuwa anakupenda. Kisa cha Amnoni na Tamari katika biblia “1Samweli 13:1-22”,
kinaeleza jinsi Amnoni alivyougua kwa kumpenda dada yake Tamari, lakini
baada ya Kuzini naye, Mihemuko ya Ngono ilipoisha akamchukia Vibaya
sana.
Kuna
ujinga ambao shetani ameuhalalisha kwa vijana wa kizazi hiki, kuwa
Upendo unadhihirishwa kwa tendo la NGONO, yaani bila kumuonjesha eti
utakuwa hujakubali penzi lake, na wengine ukiwanyima eti wanaangua kilio
nakusema “Darling mwenzio utaniua aaaaaa” ,
Mwambie kama kweli unanipenda basi kufa nione, utashangaa macho
makavuu! anaendelea kula dagaa. KIJANA ANAYELILIA NGONO KABLA YA NDOA
HAKUPENDI ANAKUTAMANI,
na jambo la hatari kabisa ni kwamba
anakutenganisha na Mungu wako kwa kukuingiza katika Dhambi – Neno
linasema “Enyi Wazinzi, hamjui ya kwamba kuwa rafiki wa Dunia ni kuwa ADUI wa Mungu? …” Yakobo 4:4.
Iweni na akili, upendo unaokutenga na Mungu wako una faida gani?
Ulimwengu utakapokugeuka na Tufani kuvuma juu yako, utamkimbilia nani
kama sio Mungu?

Wito wangu kwa vijana wote wanaopenda kuwa na maisha yenye Baraka za mungu ni huu “Basi Mtiini Mungu, Mpingeni Shetani, naye atawakimbia. Mkaribieni Mungu naye atawakaribia ninyi ….” Yakobo 4:7-8. Mungu anahitaji vijana wanaoweza kumwambia Shetani “NO” au “HAPANA”, mpaka lini Shetani ataendelea kutawala maisha ya vijana? It is time to say “NO” and be ready because JESUS is around the corner. Mwisho nawapongeza vijana wote waliotangaza NIA ya kufunga Ndoa halali, na kuachana na Dhambi ya Uzinzi. Nitazidi kuwaombea ili Mungu azidi kuifanikisha mipango yenu. MUNGU AKUBARIKI .
Comments