KWA MUUJIZA HUU NITAMTUKUZA MUNGU MILELE YOTE




PETER MICHAEL BAADA YA KURUDI KUTOKA KANISANI P A G  KAWE DAR ES SALAAM

shalom ndugu katika BWANA popote ulipo na napenda kushudia kile ambacho BWANA YESU amenitendea ilikua tarehe wiki iliyopita tarehe 04/12/2012 nisafiri kutoka hapa Dar kwenda zanzibar  kwa masuala binafsi na nilifika salama na nilishughurikia kilichonipeleka kama kawaida tarehe tano na ilipofika tarehe 6 nikiwa kwa rafiki yangu mtumishi wa MUNGU Baraka Mhunda mida ya saa tano[5] usiku nikiwa peke yangu maana rafiki yangu alikua kazini kwake nikiwa tu nimemaliza kusikiliza gospel kwenye computer na kuzima computer tayari kwa kulala ghafla alitokea mwanamke mmoja ni mwafrika alikua amevaa ninja nyeusi isipokua macho tu ndio yaliyokua yanaonekana na kuanza kuniambia kwamba lazima tu atazuia yale ambayo MUNGU amepanga maishani mwangu na kwa rafiki zangu kwa sababu lilikua tukio la ghafla nilibaki tu kumtazama katika hali ya kumshangaa na huku sina wasiwasi wowote, akiwa amenikaribia huku akibadirika badirika na kuachama achama hovyo hovyo huku akirudia maneno yaleyale kwamba lazima tu atazuia kusudi la MUNGU juu ya maisha yangu ghafla nikajikuta kama nina roho mbili maana roho yangu ilikua bado inamshangaa na wakati huo huo kwa muda kama wa sekunde 5 nikajikuta nimemwambia kwamba NAKUTEKETEZA KWA JINA LA YESU KRISTO  na hilo neno NAKUTEKETEZA KWA JINA LA YESU KRISTO nillilitamka zaidi ya mara 10 ndani ya sekunde hizo tano pale pale yule mwanamke mi sijui kama ni mchawi au ni jini ametumwa alikatikakatika vipande vinne yaani ulitokea upanga ukamkata kuanzia katikati ya kichwa hadi sehemu za siri na bukakikata kiuno chote hivyo akawa vipande vinne yaani mguu mmoja kivyake na mwingine kivyake na jicho moja na nusu ya kifua kivyake na muda huo huo ukaja moto kutoka mbinguni ukamteketeza yule jini hadi akapotea huku akipiga makelele mengi. niliposhangaa kwanza ni kile kitendo cha kumshangaa huku Roho nyingine ikikemea tena ndani ya sekunde tano nimeshatamka zaidi ya mara 10 yaani nitamka kama umeme . na baada ya kuharibu jini huyo ulikuja mwanga mkali sana kutokea juu na ikatoka sauti ndani ya mwanga ikisema UMEPATA KIBALI KIKUU CHA MUNGU MKUU na ndani ya ule mwanga kulikua na rangi nyekundu nikauliza ni nini nikaambiwa ni damu ya YESU KRISTO ambayo ipo tayari kufanya kazi muda wowote na mahali popote kwa wote waliompa BWANA YESU maisha yao. Na nikiwa bado nashangaa ule mwanga maana hasa ulikua ni utukufu wa MUNGU nikatazama chini nikamwona rafiki yangu Jacob Werema akiwa na dada fulani ambaye mimi naamini ndiye mke wake wakiwa katika maandalizi ya harusi yao ampapo siku iliyofuata yaani jumamosi walikua  wanafunga ndoa huko Tabora kanisa la P A G  na ikatoka sauti ikisema kwamba NI DHAMBI KWA WACHUMBA KUFANYA MAPENZI KABLA YA NDOA KWANI KWANI INAONDOA BARAKA ZA MUNGU KATIKA MAISHA YAO WAKIJA KUOANA NA NIKAAMBIWA JACOB AMESHINDA NA MIMI YANIPASA KUSHINDA. Namshukuru sana JEHOVAH MUNGU wangu kwa neema aliyonipa na kwa jinsi alivyonishindia dhidi ya mipango yote ya shetani juu ya maisha yangu na marafiki zangu, sifa, heshima, ukuu,adhama, utukufu na enzi yote namrudishia MUNGU BABA yetu na kama hujampa YESU KRISTO maisha yako fanya hivyo leo kwani wokovu ni sana na hakuna ajuaye kesho hivyo tumkimbie shetani na mabo yake yote kwa kumpa YESU KRISTO maisha yetu  AMEN. BARIKIWA SANA. NI MIMI NDUGU YAKO PETER MICHAEL
 PETER MICHAEL NIKIWA CHUKWANI ZANZIBAR

JACOB WEREMA AKIWA NA MTOTO JENNIFER HUKO KANISANI P A G CHUKWANI ZANZIBAR HAPA NI KABLA HAJAHAMIA TABORA
PETER MICHAEL NIKIWA DAR
MAISHA NI MAZURI SANA UKIWA NA BWANA YESU KRISTO KWANI TUNAPATA UZIMA SASA KISHA UZIMA TELE

Comments