MAAMUZI YA LEO NI MATOKEO YA KESHO, AMUA VYEMA ILI UJE UPATE MEMA


  • MATENDO 4:12 [WALA HAKUNA WOKOVU KATIKA MWINGINE AWAYE YOTE, KWA MAANA HAPANA JINA JINGINE CHINI YA MBINGU WALILOPEWA WANADAMU LITUPASALO KUOKOLEWA KWALO] YESU PEKEE NDIO ANA UZIMA WA MILELE
    wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote,kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo kuokolewa kwalo {MATENDO 4:12} Ndugu sijui kama unajua uzima wa milele. kama unautaka uzima wa milele mpe YESU maisha yako.dunia itapita na mambo yake yote ndio maana BWANA YESU alisema kwamba itamsaidia nini mtu akipata vitu vyote harafu akifa aende motoni? ni wakati wa mimi na wewe kugeuka na kumpa YESU maisha yetu awe BWANA na MWOKOZI wa maisha yetu hvyo hakuna haja ya kusema nitaokoka tu ipo siku kwa sasa ngoja kwanza. Ndugu usidanganyike kiasi hicho amua leo kufanyika mtoto wa MUNGU kwa kumpa YESU maisha yako. Na ujumbe huu ni kwa ajili yako kwani sijaandika tu ili kujifurahisha bali ni agizo la MUNGU kwangu leo hivyo MUNGU aliyenifunulia hili akutie nguvu na kukusaidia kufikia kuokoka leo pia shetani asikuhubiri chochote kile iwe ni kupitia ndugu,marafiki au yeyote kwani hao hawana mbingu ya kukupeleka ila YESU pekee ndiye atakupeleka uzimani na yeye alisema katika YOHANA 14:3 BASI MIMI NIKIENDA NA KUWAANDALIA MAHALI ,NITAKUJA TENA NIWAKARIBISHE KWANGU ILI NILIPO MIMI NANYI MWEPO.una heri wewe utakayemchagua BWANA YESU baada ya kupata ujumbe huu na MUNGU wangu akubariki na kukushindia kwa kila hatua ya wokovu AMEN. [HII IMETOKA KWENYE PAGE YETU YA www.facebook.com/maishaYaUshindi.]
    YESU pekee ndie wa kutupeleka uzima wa milele.    www.maishaushindi.blogspot.com
    YESU pekee ndie wa kutupeleka uzima wa milele. www.maishaushindi.blogspot.com
    BIBLIA TAKATIFU

Comments