MBINU ZA SHETANI KUMKAMATA MTU WA MUNGU


shetani mwongo na baba wa uongo na kama aliweza kuwadanganya Adamu na Eva basi anaweza kumdanganya yeyote kama akikaa vibaya
maombezi kwa lengo la kuwafungua watu wanaotumikiswa na shetani ili wafunguliwe kwa jina la yesu kristo
Leo ndugu katika Bwana ningependa tukichambue kitabu cha waamuzi..Ni historia ambayo watu twaisoma na wengi wetu twaifahamu sana.Si habari za SAMSON,Mtumishi wa Mungu.
Waamuzi 13:2-5.
Samsoni alikuwa ni mnadhiri wa Mungu tokea tumboni mwa mama yake,na uzao wake ulikuwa kuja kuwakomboa waisraeli na mikono ya maadui zao Wafilisti.
Samsoni alikuwa akiwamaliza Wafilisti kwa nguvu za ajabu mpaka hao wafilisti walijiuliza siri ya Nguv lakini hawakupata jibu.
Tatizo kubwa na baya sana ambalo watumish wa Mungu tuwe macho ni kujiachilia na kutoa siri za Mungu kwa mtu yeyote.
Jambo alilokosea Samson aliingia kwenye mahusiano na binti aliyeonekana mzuri,binti wa kifilisti,mmoja wa maadui.Wafilisti wakaitumia nafasi hyo kumtumia Delila ili kumchunguza Samsoni.

MBINU ZA SHETANI KUKUANGAMIZA.{waamuzi 16:19-22}
1.Anakulaza usingizi.
2.Anatafuta sababu ya nguvu zako{kama kwenye uimbaji,maombi au kufunga}.
3.Anakupofua macho.
4.Anakuhamisha sehemu yako yenye baraka na kukufungia kuzimu..
5.Anakufunga vifungo{i.e uchoyo,uongo,matusi,fitina,uchawi,uganga,uzinzi,uasherati n.k}
6.Anakupa kazi.
Shetani ana kila mbinu za kumkamata mtu wa Mungu,ila ukisimama atakusìndia.MUNGU awabariki sana BY Raphael Mbogo
RAPHAEL MBOGO

Comments