USHUHUDA KWA KILE MUNGU ALICHOTENDA


PETER
usije ukacheza na Mungu ambaye mimi ninamuamini, Mungu ambaye mimi namuita Baba, uhalali wangu wa kumuita Baba mwenyezi mungu unapatikana kwa kipekee sana na hasa ukimtambua Yesu ni nani? Kinyume na hapo huna haki ya kumuita Mwenyezi Mungu Ni Baba yako. Basi kuna mtu mmoja alinikosea sana! Nikajikuta nalia kama mtoto mdogo, kwa takribani kama wiki mbili mfululizo, kuna usiku mmoja wakati niko kwen
ye majonzi mazito nikiwa nimelala, nikaona mbingu zimefunguka na mala nikajikuta niko dunia nyingine kabisa na watu wa kwenye hiyo dunia ni wakarimu vibaya mno! Mara wakaja watu watatu, wakanisalimia kwa pamoja nami nikiwa nashangaa shangaa wawili wakajitenga mbali kidogo nikabaki na mmoja wao, nae akaniuliza je! Una wasi wasi na mimi? Bila kutegemea nikajikuta nimemwambia hapana! Sina wasi wasi na wewe hata kidogo! Akaniambia najuwa kuwa huna wasi wasi na mimi, nikamuuliza sasa kwanini kumbe kuniuliza!? Akania mbia kuwa kwanini unalia mpaka unaninyima raha? Nikamwambia kuwa napenda ninyamaze kulia lakini nashindwa, akaniambia kuwa tamka neno lolote kwa anayekufanya ulie hivyo nami nitalifanya. Ndugu zangu wapendwa, ningese uyu mtu na afe si dhani kama leo hii tungekuwa nae nashukuru nilitamka kitu kingine kabisa! Na leo hii kile kitu kimekuwa dhahili. Wangapi wanamtegemea Mungu kwa kila jambo? Mwenyezi Mungu ndo kila kitu, na Mungu wa kweli ni yule ambaye Yesu kristo alitufundisha kuwa daima tumuite Baba. Tumtambuwe kama Baba. Amen. Amen maana yake na iwe, imekuwa tayari.By Peter T Peter.
PETER T PETER


PETER AKIWA NA RAFIKI YAKE
{ ndugu zangu ni jambo muhimu sana kushuhudia matendo makuu ambayo MUNGU amekutendea ili na wengine wajifunze na wabarikiwe ila iwe tu ni ushuhuda wa kweli ndugu yetu huyu ambaye anaishi springs free state south Africa ambaye ni mdau mkubwa wa page yetu ya maisha ya ushindi katika facebook ametoa ushuhuda huu na ameruhusu utumike kuwafundisha na wengine na haya MUNGU anayatenda sana kumbuka MUNGU alivyomsaidia Ibrahimu akawapiga wafalme kumi sasa [Mwanzo 14:17-24] sasa swali hivi familia moja inaweza kupiga mataifa kumi? lakini MUNGU alimpigania Ibrahimu na akawapiga hawa na MUNGU huyo huyo ndie MUNGU wako na yale matendo aliyoyatenda enzi zile anaweza kuyatenda hata leo kwani yeye ni yule yule jana leo na hata milele [waebrania 13:8] MUNGU akubariki sana na kama una ushuhuda wa kweli tutumie katika www.facebook.com/maishaYaUshindi. MUNGU akubariki sana na KWA MSAADA WA MUNGU TUTATENDA MAKUU MAANA YEYE ATAWAKANYAGA WATESI WETU.{ZABURI 60:12}

Comments