Mimi Steven Gwasa Anthony Mwakatwila pamoja na Mke wangu Beth
Tunamshukuru sana Bwana Yesu Kristo aliyetuokoa na kutupa nafasi ya kuwa Watoto wake na pia kutuita ili tupate
kumtumikia katia maisha yetu aliyotupatia kuishi hapa Duniani, Bwana Yesu Kristo aliniokoa tarehe 19-11-1995,
jioni katika mkutano wa injili uliofanyika katika viwanja vya ccm Tukuyu, Mkutano huo uliandaliwa na watu wa
Tukuyu Christian Fellowship, Mtumishi wa Mungu Mmanyi toka Dar es salaam alihudumu katika mkutano huo wa Injii,
Mke wangu Beth pia amempokea Bwana Yesu Kristo, alimpokea mwaka 1997, Katika semina iliyofanika mjini Tukuyu,na
mtumishi C.Mwakasege toka Arusha alihudumu katika semina hiyo.
Mimi ni mfanyakazi katika Shirika liitwalo Here’s Life Tanzania,
nikiwa Msimamizi wa Kanda ya Nyanda za juu kusini Magharibi, Makao yetu yapo Mjini
Mbeya, Baba yangu ni askari mstaafu wa jeshi la Mageleza anaitwa Anthony Gwasa. Mwakatwila yeye aliokoka mika ya
sitini, Mama yangu anaitwa Lideya Mwakibete, pia amempokea Yesu kamaBwana na Mwokozi wa maisha yake, tupo sita
katika Familia ya Mzee Mwakatwila, nikwa motto wa tatu na mzaliwa wa kwanza wa kiume,nina dada zangu waili wa
kwanza anaitwa Sara,wa pili ni Upendo, na nina wadogo zangu wa kiume wawili nao ni Daved, na Geofrey, wa Mwisho
kwa sasa ni marehemu aliitwa Neema, Mke wangu anatokea katika
familia ya Mzee Seth M wang’onda, Baba pia ni mstaafu kutoka shirika la mapato TRA.
Mimi na mke wangu tunamshukuru Mungu aliyetuupa watoto Watatu, Mtoto wetu
wa Kwanza anaitwa, Birgita, wa pili Daniel, na watatu ni Priska
Baada ya kumpokea Bwana Yesu Kristo, Mungu aliweka ndani yangu wito wa
kumtumikia, na ninamshukuru kwa kunipa ofisi ya Ualimu ndani yangu, na kuniambiwa wazi kuwa anataka Nifundishe
Watoto wake na watu wake, na tulianza utumishi huo rasmi mwaka
2006, baada yakupitishwa na Bwana katika maandalio mbalimbali,
ya kiutumishi, Mwaka huo nikiwa Lilongwe Malawi kikazi ndipo Bwana
aliposema nami kuwa sasa “Lundi Tanzania kwa kazi ninayotaka uifanye nayo ni ya kufundisha Watoto wake yaani
Kanisa lake, na Watu wake pia kuwaombea watu na nchi yetu” ni
kweli Toke wakati huo nilipoludi tu nchini kila kitu kilibadilika, na ndipo Mimi na mke
wangu tulpoanza kazi hii ya kufundisha neno la Mungu atupalo kulifundisha kwa wakati, na Mungu ameweka kitu
ndani yetu nacho ni kuwahudumia Watoto wake yaani watu waliomwamini Yesu waliopo mahali popote pale,
tunafanya kazi mahali popote pale tupatapo mialiko ya kufundisha neno lake bila kujari dhehebu gani ilimladi
tumepata kibari kutoka kwa Bwana wa huduma hii Yesu Kristo.
''Hata nitakapokuja ufanye
bidii katika kusoma na kuonya na kufundisha…. ''(1Timotheo 4:11)
Tulianza kufanya huduma hii kwa kufundisha watu wawili
tena wa familia moja, baadaye wakaongezeka kuwa thelathini, mpaka hii leo tunafundisha maelfu ya watu katika
nchi hii ya Tanzania, tumepata mialiko mingi kwa kufundisha katika makusanyiko kwenye
mashule ya sekondari, vyuo mbalimbali, kambi za vijana, Pia semina za Watumishi wa Mungu
Wachungaji, Wainjilisti Waombaji na hata katika madhehebu mbalimbali. mwaka 2006 tulianza kufanya huduma ya
kufundisha kwa kushirikiana na Wapendwa kutoka madhehebu mbalimbali, walijikusanya kama kamati na kuandaa
semina mjini mbeya, na kukodi ukumbi wa St Marys,na watu wasiozidi, 50 walihudhuria semina hiyo , na Bwana
alitupa somo lenye kichwa KUWEKWA HURU, hapoa ndipo ulikuwa mwanzo wa huduma hii kuenea sehemu mbalimbali,
mwaka 2007 kamati hiyo iliandaa tena semina na kukodi tena
ukumbi wa Uhasibu mjii mbeya, watu wapatao mia 200, wakiudhuria, na hapo Bwana alianza
kufungua milango ya kwenda mikoa mbalimbali ya nchi hii kufundisha semina za neno la
Bwana, mwaka 2008, kamati hiyo iliandaa tena semina Mbeya mjini na safari hii tulifanyia
kwenye viwanja vya Chuo Cha Otu mjini Mbeya.
Kamati ilitafuta miti na kuomba maturubai na kuezeka na kukodi viti pia
walikubaliana kutengeneza jukwaa la chuma, walifanikiwa kutengeneza jukwaa hilo, tulikuwa na huduma nzuri sana,
Bwana aliokoa watu wengi sana, na kuwaponya na kuwa fungua, na kuwafundisha, Mwaka 2009, tulianza kutengeneza
darasa linalo hamishika, na kuwa na semina ambayo ilikuwa na watu wengi sana tulitengeneza hema la watu
takribani 2,000 wakae lakini watu walikuja zaidi, na mwaka huu, 2010 tumekuwa na semina nyingi tokea mwanzoni
mwa mwaka, na tuliendelea kuongeza darasa hilo na ili lifikie watu elfu tatu, lakini baada ya semina ya mwezi wa
7 mwaka huu wa 2010 , tumegundua kuwa tunahitaji sasa darasa lisilo pungua watu 5,000 hayo ndio mafanikio ya
utumishi huu ambao Mungu ametupa, mwaka 2008, Mungu alitupa nafasi ya kuweka msomo kwa njia ya ledio, na pia
kwanjia ya iitwayo Mbeya TV, tumekuwa na vipindi kila siku ya jumanne saa tatu mpaka saa nne katika ledio Bomba
fm, pia mwaka 2010,tumekuwa na vipindi kwenye ledio Baraka fm, Ledio hizo zinafikia mikoa takribani nane na nchi
mbili za Malawi na Zambi, kila wiki tumekuwa na semina hizo, na vipindi hivyo vyote tunanunua. Tunahitaji maombi
yako sana.
Malengo yetu ni kuufikisha ujumbe wa neno la Bwana kwa kila mtu mahali
popote pale Duniani. Nakukaribisha sana karibu tushirikiane katika utumishi huu kwa kutuombea kutushauri, na
hata kwa hali na mali. ninamwamini Mungu kuwa Roho Mtakatifu atakufundisha, pia usisite kuwashiriksha watu wengine kile Mungu amekufundisha,pia
utakapo pata nafasi kutushirikisha mahitaji yako ili tukuombee usisite kuwasiliana nasi, nasi tunakuahidi
tutakuombea kwa Bwana na tunamuamini sana Yesu atakuhudumia, ikiwa pia unahitaji kuokoka usisite mpe Yesu maisha
yako, na anza kutendea kazi mambo yale Bwana .
Bwana akubariki sana
Wako: Mr Steven & Mrs Beth
Mwakatwila
|
Comments