WACHAWI WALINILUSHIA MOTO NA SIKUUNGUA

ONESMO PHILIMON

Shalom watu wa MUNGU, Mimi ni Onesmo Philimon niko ,Kabindi Biharamulo mkoa wa kagera, ndugu zangu ilikua ni Feb 2012 nikiwa bwenini shuleni huko bukoba usiku nikiwa nimelala. na ajabu siku hiyo ndio siku pekee ambayo nililala bila kuomba maana tangu niokoke mwaka 2008 niliendelea vizuri sana katika wokovu na siku hiyo ndio siku ambayo niliamini kwamba ROHO MTAKATIFU hutusaidia katika udhaifu wetu maana siku hiyo nilienda kulala mapema maana nilikua nimechoka sana na nililala mida ya saa 3:30 usiku bila kuomba yaani nilisahau na ilipofika saa 5 usiku nilisikia sauti moyoni mwangu ikisema ''AMKA UOMBE'' sauti hiyo ilizungumza ndani yangu kwa muda mrefu sana lakini hata sijui kwanini siku hiyo nilikua na usingizi kiasi hicho. Sauti hiyo iliendelea kwa muda hadi ikaongeza spidi niliamka na kukaa kitandani na kuomba kwa ufupi nikasema tu ''ASANTE YESU' nikalala baada kama ya dakika 5 ile sauti ilianza tena kusema amka uombe niliamka na kukaa maana usingizi ulikua mzito sana nikikaa kama dakika tano na sikujua nililala vipi maana nilikuja tu kushtuka kwa sauti ile ndani yangu ikiniambia ''AMKA UOMBE'' tena wakati huu ilisema kwa ukali kidogo niliamka na kuanza kuomba kimyakimya maana bado usingizi ulikua mzito sana nikiwa nimekaa kitandani ndani ya chandarua nilitazama dirishani na kushangaa maana usingizi uliisha ghafla baada ya kuona wanaume wawili wakiwa vifua wazi huku wakiwa wamevaa manyoya ya kuku na ngozi ya chui kichwani walichokua wanafnya walikua kama wanatupia moto moto upande niliopo mimi maana nilikua nalala karibu na dirisha japokua kwenye hilo bweni tulikua tunalala wanafunzi 16 na wenzangu wote muda huo walikua wamelala tu huku wengine wanakoroma. Hapo ndipo nilipojua kwanini ROHO wa MUNGU alikua ananiambia niamke niombe kwa muda wa kama wasaa mawili nilikua naambiwa kuamka ili niombe ila mimi sikujua kwanini naambiwa niamke niombe ila baada ya hapo nikajua kwanini ROHO MTAKATIFU yuko pamoja na wateule wa MUNGU ni kwa ajili ya kuwasaidia maana wengi wetu hatuna macho ya rohoni, mfano mimi nadhani kwa muda huo wote walikua wanajalibu kuroga lakini walishindwa. nikiwa nawatazama niliwaona wanarusha moto yaani wakielekeza viganja vyao kwangu moto unatoka viganjani mwao na kuja kwangu ila kila wakirusha huo moto ulienda kidogo tu na kuzimika  na mmoja kati ya wale wachawi ambaye alikua mfupi kidogo alisema ''HUYU MJINGA ANA NINI MBONA MOTO HAUMBATI?'' mwenzake akasema kama hatakufa leo basi kesho tutatafuta chochote kati ya nywele zake,kinyesi,au mchanga sehemu alipokanyaga na tutaona kama hatakamatika. kwa muda kama wa dakika 10 nilikua tu nimeduwaa na kuwa kama mtu aliyeganda tu huku nikiwa naangalia waliendelea kutupa moto wao ambao ulikua unazimika kila wakirusha yaani wakiwa wanarusha unatoka moto na hata mwanga mkubwa unaonekana lakini ajabu wenzangu hakuna hata mmoja aliyeona lakini kila tu wakirusha moto huo ulizimika baada ya kwenda kama umbali wa rula moja.baada ya dakika 10 nilitoka kwenye chandarua ili niwakemee hadharani kwa jina la YESU nilipotoka tu kwenye neti wakaniomba na kupotea na wakati huo huo nilikemea kwa nguvu kwamba mshindwe kwa jina la YESU.pale pale wakapotea na wenzangu wote wakaamka wengine wakitamka maneno sifahamu kama walikua wanaota au niliwaambia yote na baada ya hapo sikulala niliendelea na maombi huku nikitafakari kwamba hakika napendwa sana na MUNGU hata tofauti na ninavyodhani.Tangu siku hiyo nilijua hakika ROHO WA MUNGU yupo kwa ajili ya kutusaidia katika udhaifu wetu na wale wachawi walisema watachukua nywele au mchanga lakini namwamini MUNGU hawawezi kufanya chochote maana aliyeko ndani yetu yaani ROHO MTAKATIFU ni mkuu kuliko waliyenae hao wachawi.MUNGU awabariki sana na ndugu kama huna ROHO MTAKATIFU basi tamani kuwa nae na enda kanisani ukaombewe na wachungaji na baada ya hapo utaona ushindi kwa kila jambo na ROHO MTAKATIFU anajua hata yajayo hivyo anaweza kukusaidia.na mimi hata sasa 2013 niko salama sana maan YESU KRISTO kwake tunashinda na zaidi ya kushinda.

Comments