CHANZO CHA USHIRIKA NA ROHO MTAKATIFU NI KUMPENDA MUNGU.

Mtumishi Gasper Madumla


Bwana Yesu asifiwe…

Ushirika na Mungu hauji kwa kuomba sana,Au kwa kufunga sana.Bali ushirika na Mungu huja kwanza kwa kumpenda Mungu.

Tunasoma Yohana 14:23;
“Yesu akajibu, akamwambia, Mtu akinipenda, atalishika neno langu; na Baba yangu atampenda; nasi tutakuja kwake, na kufanya makao kwake.”

*Umeona hapo,;
Neno linasema kwanza ni KUMPENDA Bwana Mungu,alafu sasa baada ya kupenda ndipo KULISHIKA NENO LAKE.

Tena baada ya kulishika neno lake ndipo Baba wa Mbinguni pamoja na Yesu,na Roho mtakatifu sasa wanakuja kufanya makazi ya kudumu ndani ya mtu huyo ampendaye Bwana Mungu.

*Wakristo wengi hatumpendi Bwana Mungu bali twapenda kupendwa.Yatupasa kwanza KUMPENDA Bwana Mungu kwa maana Yeye alitupenda kwanza (1 Yoh 4:19),
ili kuruhusu Neema ya kulishika neno la Kristo ikae ndani yetu.
*Ushirika wa Roho Mtakatifu upo katika NGUVU YA KUPENDA.

*Na ipo gharama ya kumpenda Mungu
*Tunapoamua kuishi maisha ya kumpenda Bwana Mungu yatatupelekea kupata urejesho wa USHIRIKA wa Roho mtakatifu ambao hapo mwanzo ulipotea kwa sababu ya dhambi.

Tazama pale mwanadamu wa kwanza alipotenda dhambi.Dhambi ikampelekea kupoteza USHIRIKA WA ROHO MTAKATIFU.Kisha Bwana Mungu akashindwa kumuona mwanadamu katika UWEPO wake.

Tunasoma Mwanzo 3 :9 ;
“ Bwana Mungu akamwita Adamu, akamwambia, Uko wapi?”

Kumpenda Mungu ni kuitii sauti yake Bwana Mungu kwa bidii,kufanya maagizo yake yote na kutembea katika sheria zake zote.

*Mungu anachokiitaji kwetu sisi wanadamu ni kitu kimoja tu,nacho ni kurejesha Ushirika wa Roho mtakatifu ndani yetu ili kuruhusu NENO lake lipate nafasi ndani yetu.Maana kusudi kuu la kuumbwa kwa mwanadamu ni kukaa katika UWEPO wake/Ushirika wa Roho Mtakatifu.

Na ndio maana Bwana Mungu akaacha ENZI na MAMLAKA,akashuka mpaka chini ili amkomboe mtu aliyepoteza USHIRIKA WA ROHO MTAKATIFU.Hivyo Bwana Mungu anachokiitaji kwako ni KUMPENDA YEYE.Tunasoma

Kumbu.10:12
“ Na sasa, Israeli, Bwana, Mungu wako, anataka nini kwako, ila umche Bwana, Mungu wako, na kwenda katika njia zake zote, na KUMPENDA , na kumtumikia Bwana, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote;”

*Mpenyo wa mwamini upo katika kumpenda Mungu, Ushirika wa mkristo upo katika Kumpenda Mungu.

*Mtu anayetaka USHIRIKA NA ROHO MTAKATIFU kwanza lazima akamatwe na PENZI maana penzi hulipwa kwa penzi.

-Tazama hata tu kwa mpenzi wako wakawaida ,ile namna unavyojisikia kuongea naye mara kwa mara,yaani ile kama hujamuona tu,
ni lazima utajisikia vibaya,Na ndio hali ilivyo kwa Yule anayempenda Mungu,
Kamwe hawezi kukaa mbali na UWEPO wa Mungu,Kamwe hawezi kukaa pasipo kuwasiliana na Mungu kwa njia ya Maombi.

*Amua kumpenda Mungu kwa kuomba NEEMA YA PENZI KWA MUNGU ili UKAE KATIKA USHIRIKA WA ROHO MTAKATIFU mahali ambapo kuna Ushindi ,
Maisha ya kweli,
Kuinuliwa,
Kufanikiwa kiroho hata kimwili maana sisi tumeumbwa ili tuwe watu safi kila eneo la kiroho hata kimwili.

UBARIKIWE.

Comments