IMANI NI MSAADA KWA WATOTO WA MUNGU

Imani ni uhakika wa rohoni kwamba jambo fulani lazima lifanikiwe Imani ndio mkono wenye nguvu sana utumie katika maisha yako kama mtoto wa MUNGU uliyesafishwa kwa damu ya YESU.YESU Akamwambia, Binti, imani yako imekuponya, enenda zako kwa amani, uwe mzima, usiwe na msiba wako tena.Marko 5:34
Kwa sasa unashindwa kwa sababu imani yako inapigwa na shetani  hivyo ongeza imani na maombi

Wokovu ni vazi likufaalo ambalo MUNGU anamekupa hivyo jitahidi vazi lako la wokovu lisichafukechafuke na kumbuka pia kwamba kadili unavyomtumikia MUNGU ndivyo mafuta ya ROHO MTAKATIFU kwako yanaongezeka. ona mfano huu waziri analindwa lakini huyohuyo waziri akija kuwa raisi atalindwa maradufu yaani walinzi wataongezeka na mambo mengi yataongezeka hivyo hivyo kwa wewe unayemtumikia BWANA YESU kwa kadiri ya kuongezeka kwako kiutumishi yaani kumtumikia MUNGU kutafungua na baraka nyingine nyingi ikiwe  pamoja na mafunuo mapya ya kuboresha huduma yako na haijalishi wewe ni mchungaji, mwanakwaya,mpiga vyombo,mwanamaombi au kazi yeyote ya kumtumikia MUNGU.
Ndugu kumbuka kuna kupanga viwango vya imani , IMANI hadi IMANI na UTUKUFU hadi UTUKUFU na pia UTAKATIFU hadi UTAKATIFU.
Kila mtu atalibeba furushi lake mwenyewe hivyo changamka kwa YESU mwenye uzima wako wa milele. na kumbuka kuwa mchungaji au askofu hajakuita katika huduma ila MUNGU ndiye kakuita na siku ya mwisho hatakuuliza habari za wengine ila za kwako. vua dhambi na vaa vazi la wokovu, na wokovu ni kuishi maisha ya ushindi dhidi ya dhambi.
KATIKA Esta 6:1-14 Tunajifunza kwamba ''Muda Hamani anawaza kukata kicha cha mordekai ndio muda huohuo Mfalme  anawaza kumpandisha cheo mordekai serikalini''
VITU 3 VINAVYOCHAFUA IMANI YAKO NI
1;MASHAKA
2;HOFU
3;WASIWASI
Ndugu kumbuka kuwa hakuna mtu anayeweza kufanikiwa kiroho bila neema ya MUNGU ndani yake.
kuna watu husema kuwa ''mwanamke ni dhaifu ila mimi ninachojua wanawake sio dhaifu ila huonekana dhaifu kwa sababu ya maamuzi ya haraka''
Ndugu panua mipaka yako ya imani na kumbuka kuwa BWANA wako YESU KRISTO aliushinda ulimwengu ili awe kielelezo kwako na wewe kama mtoto wake uushinde huu ulimwengu na mambo yake yote. 
 Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. MUNGU ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA.
MUNGU akubariki sana .
Ni mimi ndugu yako
Peter M Mabula
Maisha ya Ushindi Ministry.
0714252292
mabula1986@gmail.com
MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili.
MUNGU Akubariki.

Comments