JINSI YA KUKUA KIROHO



Utaendelea vizuri katika maisha ya kiroho ukiyafuata mashauri yafuatayo kila siku:

1;Zungumza na MUNGU kwa maombi (Yohana 15:7)

Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa.
2: Soma Neno la MUNGU (Matendo 17:11)

Watu hawa walikuwa waungwana kuliko wale wa Thesalonike, kwa kuwa walilipokea lile neno kwa uelekevu wa moyo, wakayachunguza maandiko kila siku, waone kwamba mambo hayo ndivyo yalivyo.
3;Uwe mwaminifu kwa MUNGU (Yohana 14:21)

Yeye aliye na amri zangu, na kuzishika, yeye ndiye anipendaye; naye anipendaye atapendwa na Baba yangu; nami nitampenda na kujidhihirisha kwake.
4;Mshuhudie KRISTO kwa matendo yako na maneno yako (Mathayo 4:19
Akawaambia, Nifuateni, nami nitawafanya kuwa wavuvi wa watu. na Yohana 15:8)
Hivyo hutukuzwa Baba yangu, kwa vile mzaavyo sana; nanyi mtakuwa wanafunzi wangu.
5; Umtumaini MUNGU kwa kila jambo katika maisha yako (1 Petro 5:7)

huku mkimtwika yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana kwa mambo yenu.
6: Umruhusu ROHO MTAKATIFU akutawale (Wagalatia 5:16-18
Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili. Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka. Lakini mkiongozwa na Roho, hampo chini ya sheria. na Matendo 1:8)Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi.

Comments