TAA YA CHEMLI ILIVYOHARIBU FAMILIA




Na mchungaji Jesephat Gwajima
Siku moja niliambiwa na Mch. mmoja wa kanisa la kiroho, ambapo washirika wake, walikuwa wamepooza wote, basi nikaamua kuwatembelea siku moja usiku. Nikiwa ninawaombea nyumbani kwao, jambo la ajabu likatokea, kila nilipokuwa nikitamka "katika Jina la Yesu" taa ile ya chemli ilikuwa inafifia mwangaza wake.

Kumuuliza baba yule kwamba, aliipata wapi taa ile, akase
ma kuwa, alipewa na mtu mmoja wa uturuki ambaye alikuwa anasoma naye nchini humo. Na mara baada ya kuhamia kwenye nyumba mpya ambayo haikuwa na umeme wakaanza kutumia taa hiyo. Kuanzia hapo, ndipo magonjwa yakaanza kumpata baba yule, baadaye mkewe, na mwishowe watoto wote wakapooza.

Kumbe, shetani alikuwa anatumia taa ile kama njia ya kuishambulia familia ile. Hapo Mungu akanifundisha ufunuo huu kuwa kuna viumbe na maumbile vya rohoni vinavyoweza kuvaa mwili na kuharibu maisha ya watu. Kwamba shetani aweza kujibadili na kuwa na maumbo ya aina mbalimbali. Ndio maana ya andiko hili (1Wakorintho 10:31) kabla hujaanza kufanya jambo lolote litakase kwanza kwa damu ya Yesu. Sikwambii ili ukachome moto vitu ambavyo umenunua au kupewa zawadi bali ni muhimu kuviombea kabla ya kuanza kuvitumia.

Comments