SIOSHWI DHAMBI ZANGU BILA DAMU YAKE YESU.

SIOSHWI DHAMBI ZANGU BILA DAMU YAKE YESU.

1:   Sioshwi dhambi zangu, Bila damu yake YESU.
      Hapendezewi MUNGU, Bila damu yake YESU.

                           Hakuna kabisa, Dawa ya makosa.
                           Ya kututakasa, Ila damu yake YESU.

2:   La kunisafi sina, Ila damu yake YESU.
      Wala udhuru tena,Ila damu yake YESU.

3:   Sipati patanishwa,Bila damu yake YESU.
      Hukumu yanitisha, Bila damu yake YESU.

4:   Sipati tumaini ,Bila damu yake YESU.
      Wema wala amani,Bila damu yake YESU.

5:   Yashinda ulimwengu,Hiyo damu yake YESU.
      Na kutufikisha juu,Hiyo damu yake YESU.

6:  Twaimba utukufu, Una damu yake YESU
     Milele twaisifu, Hiyo damu yake YESU.


MUNGU akubariki sana ndugu mwanamaisha ya ushindi popote ulipo na kumbuka kuwa damu ya YESU KRISTO pekee ndio inauwezo wa kutusafisha dhambi zetu.
 ujumbe huu ambao ni wimbo wa tenzi za rohoni tumeutoa kitabu cha TENZI ZA ROHONI na ni namba 78. iko ukurasa wa 50.

Comments