Maombi ya Imani

  • Na Mtu wa Mungu Samson Mboya 
    Utangulizi: Wengi wetu tunapenda sana kufanya maombi ila kuna sababu nyingi zinzoweza kuzuwia maombi yako yasijibiwe na Mungu mojawapo ya sababu hizo nyingi katika somo langu nitaongelea sana kuomba kwa imani, kila anayeomba maandiko yanatufafanulia na aombe kwa imani, 
    Yakobo 1:6, 7 Ila na aombe kwa imani, pasipo shaka yo yote; maana mwenye shaka ni kama wimbi la bahari lililochukuliwa na upepo, na kupeperushwa huku na huku. Maana mtu kama yule asidhani ya kuwa atapokea kitu kwa Bwana.
     · Mashaka katika kuomba ni kama mtu mgonjwa anayejilazimisha kufanya kazi ngumu,
     · Mashaka ni kirusi cha kuharibu imani ya mtu 
    · Mashaka yanahamisha imani ilipo kupeleka sehemu nyingine kwamfano kama ukona mchumba na Mungu alishakudhibitishia labda kwa ndoto maono au kwa mjumbe kuja kwako kukamilisha uhakika huo, usipoamini kile ulichoonyeshwa na mungu umeruhusu Roho nyingine ya kuja kuharibu imani yako na hapo watu wengi huwa wanajikwaa sana ,
     · Kama huwezi kuamini kupokea muujiza wako kutoka kwa Mungu basi maishani mwako usitarajie jambo jema, maana hata ukiomba ni kama unapoteza muda wako bure,
     Isaya 45:11 Bwana, Mtakatifu wa Israeli, na Muumba wake, asema hivi; Niulize habari za mambo yatakayokuja; mambo ya wana wangu, na habari ya kazi ya mikono yangu; haya! Niagizeni. Wakati wote Mungu ameruhusu tumuombe lolote ila kwa utaratibu alioufanya yeye mwenyewe, kile unachokiomba ni kwaajili gani unakitaka je? Unataka kunyanyasa wengine, au kuonekana kwa wengine au ni kwautukufu wa Mungu?
     Yeremia 29:13 Nanyi mtanitafuta na kuniona, mtakaponitafuta kwa moyo wenu wote. Mungu hajajificha sehemu nyingi alizosema nitafuteni alimaanisha maisha yako umuhusishe Mungu kwa kila jambo kuonekana kwa Bwana katika maisha yako ni wewe kumkubali atawale maisha yako yote, * Mathayo 21:21B, 21D, 22Yesu akajibu, akawaambia, Amin, nawaambia Mkiwa na imani, msipokuwa na shaka, mtafanya si hilo la mtini tu, lakini hata mkiuambia mlima huu, Ng'oka, ukatupwe baharini, litatendeka. Na yo yote mtakayoyaomba katika sala mkiamini, mtapokea. 
    1. Kuamini katika kuomba kuna maana kubwa sana mbele za Bwana inaonyesha kumheshimu Mungu na kumtegemea yeye nayeye atatenda juu ya hitaji lako, 
    Marko 11:24 Kwa sababu hiyo nawaambia, Yo yote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba mnayapokea, nayo yatakuwa yenu. Hakuna kinachoweza kuwa chako katika ulimwengu wa Kiroho ikiwa hujaamini kuwa chako hivyo kuchukuwa kitu chochote na kukimiliki katika ibada ya maombi ni kuamini kwanza,
     Luka 11:9, 10 Nami nawaambia, Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa. Kwa kuwa kila aombaye hupokea; naye atafutaye huona; naye abishaye atafunguliwa. Wengi hukata tamaa sana pale wanapoomba maombi yakichelewa na Muovu anafurahia sana kukwama kukatakwako tamaa, 
     Warumi 4:20, 21 Lakini akiiona ahadi ya Mungu hakusita kwa kutokuamini, bali alitiwa nguvu kwa imani, akimtukuza Mungu; huku akijua hakika ya kuwa Mungu aweza kufanya yale aliyoahidi. Imani si mtaji tu bali ni nguvu ya kubeba kile unachokitaka,
     Waefeso 3:20 Basi atukuzwe yeye awezaye kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo, kwa kadiri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu; 
    Ø Kila unaloliomba omba kwakuamini unachokitaka, 
    Ø Omba kwaajili ya utukufu wa Mungu-si kwakumuonyesha mwanadamu 
    Ø Fahamu kwamba kila utakaloliomba kwa usahihi Litajibiwa na Bwana Mungu
     Ø Fahamu siri ya Maombi kisha angalia Mtu wa kumshirikisha si kila mmoja anayetekiwa kufahamu unachokiomba Kwa Mungu, 
    Waebrania 4:16 Basi na tukikaribie kiti cha neema kwa ujasiri, ili tupewe rehema, na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji. Mungu hajibu maombi kwaajili ya machozi au kwakukaa muda mrefu lah bali fahamu si kwaakili zetu bali ni kwarehema zake Mungu 
    Waebrania 11:6 Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao. Kabla hujaomba ukiwa unawaza kuomba Mungu anakuona na ameshafahamu kusudio la Moyo wako, japo wewe inawezekana usifahamu hivyo kabila ya kutamka maneno ya maombi unayoomba kwa Bwana Mungu akiangalia Moyoni mwako anachokiona ni Mashaka na si imani huwezi kupokea mahali hapa patakusaidia sana Mungu ametaka ujifunze kuomba kwaimani Mimi ninaamini baada ya somo hili wewe utaanza kuomba kwa imani Bila ya kukata tamaa, na utashuhudia wengine kile Mungu alichokutendea,
     Yakobo 1:6, 7 Ila na aombe kwa imani, pasipo shaka yo yote; maana mwenye shaka ni kama wimbi la bahari lililochukuliwa na upepo, na kupeperushwa huku na huku. Maana mtu kama yule asidhani ya kuwa atapokea kitu kwa Bwana. Maombi yako yameambatana na machozi mengi kwasababu ya maumivu ambayo hujui yataondoka vipi, mimi natakakukuambia baada ya kumaliza kusoma ujumbe huu hautatumia nguvu kubwa sana wala machozi mengi kama unavyoomba sasa bali utajikuta unaomba katika Roho na kweli, na kwaimani,
     1Yohana 5:14 Na huu ndio ujasiri tulio nao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia. 
    Wahooo!! Sasa unaweza kuingia katika maombi ya imani pata muda wa kutafakari kile unachotaka kukiomba usikurupuke tu kwakuwa umetingwa na matatizo,Tulia na sema nakuona hujatulia, pata kikombe cha maji masafi ya kunywa alafu jiulize unataka kuomba nini kwa Mungu na ni kwanini unaomba, hilo hitaji, tatu unaomba na nani, Musa aliomba na Haruni,uri, Eliya akaomba na Elisha, Yesu akatenga wanafunzi wakuomb naye wewe unaomba na nani!? Ikiwa hujui au ungetaka upatiwe mtu wa kukusaidia kuomba basi usihofu Mungu ameona hitaji lako na amelijibu, 
    Umbali usikuzuwie kupata huduma pata Mtenda mmoja toka katika Hema ya Kinabii naye atakusaidia au ukihitaji ushahuri kabla ya maombi piga simu namba 0756 809 209 huduma hii ni bure kabisa ni kwaajili yako wewe itapokelewa na Mtu wa Mungu

Comments