HARUSI YA KANA (wedding in Cana of Galilee) * sehemu ya kwanza*

na mtumishi wa MUNGU Gasper Madumla


“ Na siku ya tatu palikuwa na arusi huko Kana, mji wa Galilaya; naye mama yake Yesu alikuwapo.
Yesu naye alikuwa amealikwa arusini pamoja na wanafunzi wake.” Yoh.2:1-2

Nakusalimu mpendwa;
Bwana Yesu asifiwe…
Karibu tuendelee sasa;

KANA ni mji wa magharibi mwa ziwa Galilaya,mahali ambapo Bwana Yesu Kristo alifanya muujiza wake wa kwanza wa kubadili maji kuwa divai. Muujiza huu ulikuwa mkubwa sana maana Biblia inasema kupitia muujiza huo,Bwana Yesu akaudhihirisha UTUKUFU wake,
nao wanafunzi wake wakamuamini.
KANA ya Galilaya ndipo alikozaliwa Nathanieli,yule muisraeli safi kweli kweli,ingawa Nathanieli hapo awali alikuwa na wasi wasi kwa kwa habari ya Yesu kutoka Nazareti,naye akamuuliza Filipo ya kwamba neno jema ilitatoka Nazareti.?

Yoh.1:46
“Nathanaeli akamwambia, Laweza neno jema kutoka Nazareti? Filipo akamwambia, Njoo uone.”
Alikadhalika ukisoma katika( Yoh.21:1-2,)utaona kwamba mahali ambapo Nathanieli alipozaliwa.

KANA ya Galilaya, ndipo mahali ambapo Bwana Yesu alipofanya muujiza wa pili baada ya kutoka uyahudini.
Muujiza huu wa pili ulikuwani uponyaji wa mtoto wa diwani mmoja wa Karpenaumu.(Yoh.4:46-50.)
Mji huu wa Kana ya Galilaya, haukutajwa katika agano la kale,ila umetajwa katika agano jipya.
Ulikuwa ni mji wa kawaida tu,lakini leo sio wa kawaida tena kwa sababu mji huu umekuwa sehemu ya maandiko matakatifu kwa kile tukisomacho.

Ninafahamu ya kwamba umeshawahi kualikwa harusini labda sio mara chache bali yawezekana umealikwa mara nyingi zaidi.Yeye anayealikwa harusini ni yule anayekuja kushuhudia kufungwa kwa ndoa na kusherekea pamoja na watu wote kwa furaha.
Mualikwa huwa sio muhusika mkuu harusini,
Mualikwa ni yule mwenye kupewa mualiko wa kuhudhulia arusini tu.
Yeye anayestahili kuingia arusini ni yule aliyealikwa tu.

Katika Yoh.2:1-2,(andiko la hapo juu),tunaona ya kwamba naye Yesu amealikwa tu harusini,Yeye pamoja na wanafunzi wake.
Yeye pomoja na wanafunzi wake walikidhi vigezo vya kuingia harusini maana wote walialikwa,hakuwapo hata mmoja aliyejichomeka ili aingie katika harusi hii,bali wote walialikwa.Biblia inatuambia kwamba naye mama yake Yesu alikuwa ndani ya harusi.

Bwana Yesu hakuenda harusini kwa ajili ya kufundisha kama desturi yake ya kufundisha huku na huko, wala hakuenda kwa dhumuni la kutoa mapepo.Bali alikwenda KUSHEREKEA nao washelekeao.
Ilikuwa ni harusi iliyofaana sana,maana baada ya kazi nzito ya Bwana Yesu ya kuchapa injili sasa hatimaye Bwana Yesu amekwenda kujipumzisha naye aweze kushuhudia harusi.

Sasa ona hapa;
“ Hata divai ilipowatindikia, mamaye Yesu akamwambia, Hawana divai.” Yoh.2:3

Wakati ilipokuwa harusi imenoga,gafla divai ikawatindikia,
KUTINDIKA maana yake kuisha,kukaukiwa,kupungua hadi mwisho.Ilikuwa sio mategemeo yao kutindikiwa na divai namna hii,maana kile walichokiamini ni kwamba divai iliyopigiwa bajeti itajitosheleza.
Ndiposa nikajifunza;

*KATIKA MAISHA YA MWANADAMU KUNA HALI YA KUTINDIKIWA.

Mwanadamu yeyote yule ni lazima atafika wakati wa kutindikiwa katika maisha yake aishiyo,haijalishi anaishi wapi,iwe ni Ulaya au Afrika,Lakini ni lazima apitie hali hiyo.Hali ya kutindikiwa huonesha kwamba mwanadamu hana uwezo wa kujiendesha yeye mwenyewe pasipo Yesu Kristo.

Haleluya…
Nasema;
Haleluya…

Nampenda mama yake Yesu namna anavyotufundisha siku ya leo,Biblia inasema pale walipotindikiwa tu,mama yake Yesu alimfuata Yesu Kristo wa Nazareti.Hii ikionesha na kutufundisha kwamba mama yake Yesu hana uwezo ule alionao Yesu.
Na ndio maana unaona mama huyu alimkimbilia Bwana Yesu,akitufundisha kwamba kila jambo lenye kutindika lipeleke kwa Bwana Yesu,nalo litatinduliwa tu…

ITAENDELEA…


 
 Bali wote waliompokea(YESU KRISTO) aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa MUNGU, ndio wale waliaminio jina lake; -Yohana 1:12

Comments