UJUMBE WA MWAKA MPYA KUTOKA MAISHA YA USHINDI , ZABURI 136

BWANA YESU KRISTO asifiwe
 MUNGU akubariki sana na hongera kwa kufika 2014.
ujumbe wa mwaka mpya kutoka hapa ni ujumbe wa shukrani kwa MUNGU kwa yale aliyoyatenda kwa mwaka 2013.
Hakika MUNGU alitulinda na amekulinda na wewe ndugu hivyo kwa pamoja TUMSHUKURU BWANA KWA KUWA NI MWEMA KWA MAANA FADHILI ZAKE NI ZA MILELE.
amewapiga maadui wakubwa walikuwa wanasaka uhai wako,  ameyakataza magonjwa kukuchukua wala hajawaruhusu wachawi kukufanya lolote hakika FADHILI ZA BWANA NI ZA MILELE.
twende.
     ZABURI 136 yote  ni ujumbe ambao ROHO MTAKATIFU alinipa ili niutumie kumshukuru MUNGU. Mpendwa naomba tumshukuru MUNGU pamoja .


1 Mshukuruni BWANA kwa kuwa ni mwema; Kwa maana fadhili zake ni za milele.  Mshukuruni MUNGU wa miungu; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
3 Mshukuruni BWANA wa mabwana; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
4 Yeye peke yake afanya maajabu makuu; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
5 Yeye aliyefanya mbingu kwa fahamu zake; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
6 Yeye aliyeitandaza nchi juu ya maji; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
7 Yeye aliyefanya mianga mikubwa; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
8 Jua litawale mchana; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
9 Mwezi na nyota zitawale usiku; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
10 Yeye aliyewapiga Wamisri kwa kuwaua wazaliwa wa kwanza wao; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
11 Akawatoa Waisraeli katikati yao; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
12 Kwa mkono hodari na mkono ulionyoshwa; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
13 Yeye aliyeigawa Bahari ya Shamu; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
14 Akawavusha Israeli katikati yake; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
15 Akamwangusha Farao na jeshi lake katika Bahari ya Shamu; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
16 Yeye aliyewaongoza watu wake jangwani; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
17 Yeye aliyewapiga wafalme wakuu; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
18 Akawaua wafalme mashuhuri; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
19 Sihoni, mfalme wa Waamori; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
20 Na Ogu, mfalme wa Bashani; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
21 Akaitoa nchi yao iwe urithi; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
22 Urithi wa Israeli mtumishi wake; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
23 Aliyetukumbuka katika unyonge wetu; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
24 Akatuokoa na watesi wetu; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
25 Kila chenye mwili akipa chakula chake; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
26 Mshukuruni MUNGU wa mbingu; Kwa maana fadhili zake ni za milele.



Nakutakia mwaka wa mafanikio, mwaka wa upenyo, mwaka wa kushinda, mwaka wa kukumbukwa na BWANA , Mwaka wa kujiliwa na nguvu za MUNGU, Mwaka wa Wokovu, mwaka wa kuwaliza waliokuwa wanakuliza miaka ya nyuma, mwaka wa kumkanyaga shetani na mawakala wake, mwaka wa kushi maisha ya ushindi dhidi ya dhambi na Mwaka wa BWANA MUNGU uliokubalika kwa ajili ya baraka zako zote, ziwe za ndoa, watoto , masomo na uzima pia .MUNGU akubariki sana tena sana.
       Ni mimi ndugu yako Peter Michael Mabula.
          Maisha ya ushindi Ministry.
                0714252292 
                     AMEN.




Bali wote waliompokea(YESU KRISTO) aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa MUNGU, ndio wale waliaminio jina lake; -Yohana 1:12