Alikatika miguu yote akiwa usingizini.

Yohana Nkwera
Mkazi wa Ludewa, Mkoani Njombe, Yohana Nkwera (54) anadai kukatika miguu katika hali ya kushangaza.
Yohana anasema katika maisha yake amekuwa ni mwenye hofu kubwa baada ya kukumbwa na tukio hilo la aina yake la kukatika miguu akiwa usingizini.
 Anasema hadi sasa haelewi namna hasa tukio hilo lilivyomtokea, kwani hakuhisi maumivu yoyote .
Anasema tukio hilo la aina yake lilimtokea mwaka 1992, lakini halikuwahi kuandikwa wala kutangazwa, badala yake ni watu wachache waliokuwa wakilifahamu.Anasema siku hiyo usiku alikwenda kulala kama ilivyo kawaida, alipoamka asubuhi alikuta miguu yake imekatika.

Kilichomshangaza zaidi ni kwamba hapakuwa na damu wala jeraha lilionekana. Palionekana pana kovu, kana kwamba alikatika mguu muda mrefu uliopita.


Anasema mara ya kwanza ulianza kupotea mguu wa kulia, hiyo ilikuwa ni mwezi Machi, 1992. Kutokana na tukio hilo, ndugu zangu walifanya jitihada mbalimbali ikiwemo kufanya maombi katika nyumba mbalimbali za ibada, huku wengine wakienda kwa kuwaona waganga wa jadi.

“Kama binadamu wa kawaida ilichukua muda sana kuamini kilichotokea ndani ya maisha yangu na mguu wangu,” anasema.


Mwezi mmoja baadaye yaani mwezi Aprili mguu wa kushoto nao ulikatika katika mazingira yaliyo sawa na yale ya awali.Inaweza kuwa vigumu kuamini lakini ulimwengu ndivyo ulivyo.

Anakumbuka mazingira ya kukatika kwake yanahusishwa na imani za kishirikina kwa sababu siku chache zilizopita kabla ya kukumbana na dhahama hiyo aliwahi kukorofisha na mtu katika vilabu vya pombe za kienyeji anayesadikiwa kufanya tendo hilo.Baada ya miaka saba kupita Yohana alipelekwa Hospitali Teule ya Ikonda wilayani Makete kupata huduma za tatizo lake. Alifanikiwa kupata msaada wa baiskeli ya magurudumu, ambayo aliitumia kwa miaka mitano.

Kwa sasa baiskeli hiyo haifanyi kazi kutokana na watu wanaosadikiwa kuwa ni wezi kuiba matairi na vyombo muhimu vinavyoiwezesha baiskeli hiyo kufanya kazi.


Pamoja na kupewa baiskeli hiyo na wasamaria wema, Yohana anakiri pia kuchongewa viatu na hospitali hiyo ambavyo vinamuwezesha angalau kutembea umbali mfupi.

                   Kutoka Maisha ya ushindi
 

Dunia nzima tunamhitaji BWANA YESU ili wachawi watuogope.

BWANA YESU anasema katika Mathayo 11:28 ''Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.''

             MUNGU akubariki sana

Comments