Kanisa la Anglican Uganda kujitoa kwenye umoja wa makanisa ya Anglican Ulaya,kutokana na Sakata la Ushoga
Kanisa la Anglikana nchini Uganda
(Church of Uganda) limesema halitasita kujiondoa kwenye umoja wa
makanisa ya Kianglikana na nchi za ulaya endapo wataendelea kusukumwa
kuishinikiza serikali ya nchi hiyo kubadilisha sheria iliyowekwa na Rais
Yoweri Museveni dhidi ya watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja.
Akizungumza na mwandishi wa AFP askofu
mkuu wa kanisa hilo ambalo linaheshima na wafuasi wengi nchini Uganda
Stanley Ntagali, amesema nchi za magharibi zinapaswa kuheshimu msimamo
na sheria za nchi ya Uganda dhidi ya watu wa mapenzi ya jinsia moja kama
hawataki kuheshimu hilo wao kama kanisa Anglikana nchini humo wako
tayari kujitoa kwenye muungano wa makanisa hayo na kujiendesha lenyewe.
Askofu Ntagali amesema vitendo vya
kishoga ni kinyume na neno la Mungu na kwamba hakuna kiongozi wa kweli
wa kanisa ambaye ataruhusu vitendo hivyo ikiwa na kuruhusu watu hao
kuoana na kupata kibali cha ndoa na kuongeza kwamba wakiwa katika
muunganiko wa kanisa la England wasingependa kuona kanisa hilo
linaruhusu vitendo hivyo endapo wataruhusu wao kama kanisa nchini Uganda
watajiondoa.
Tangu Rais Yoweri Museveni apitishe sheria hiyo ya watu wanaojihusisha na vitendo vya mapenzi ya jinsia moja kupata kifungo cha maisha gerezani, sheria hiyo imepokelewa kwa hisia tofauti katika nchi mbalimbali duniani hususani nchi za magharibi ambako vitendo hivyo vinaruhusiwa kwa asilimia kubwa hadi mataifa hayo kufikia hatua ya kumtaka Rais Museveni kutengua sheria hiyo kwakuwa inakwenda kinyume na haki za binadamu.
Rais Museveni alikaririrwa katika moja ya mahojiano akisema "hakuna uthibitisho wa kusema mtu anaweza kuzaliwa shoga…. na mwanaume kumpenda mwanaume mwenzake wakati kuna wanawake wengi warembo wamejaa.. ni uchaguzi wa mtu na si vinginevyo, baada ya kuwasikiliza wana sayansi nimegundua nimepata ukweli" alikaririwa Rais Museveni.
Ukiachana na mataifa ya magharibi ambayo yameijia juu Uganda kwa msimamo wake huo, lakini tukio lililowashangaza waumini wa dini ya Kikristo waliowengi Afrika ni kitendo cha askofu mkuu mstaafu wa kanisa hilo nchini Afrika ya kusini Desmond Tutu naye amelaani Uganda kupitisha sheria hiyo huku pia kukiwa na fununu kwamba askofu huyo aliyeonyesha wazi kuunga mkono vitendo vya mapenzi ya jinsia moja yuko njiani kuanzisha chama kitakachounga vitendo hivyo.
Credits:gospelkitaa
![]() |
Askofu mkuu wa kanisa Anglikana Uganda Stanley Ntagali akizungumza na vyombo vya habari nchini humo. |
![]() |
Askofu Stanley Ntagali katikati na wasaidizi wake wakiwa katika moja ya huduma nchini humo |
![]() |
Kanisa kuu la Anglikana Mtakatifu Paul Kampala nchini Uganda |

Comments