Farao = Nyumba kubwa
Festo = Mwenye sherehe
Filemoni = Mwenye upendo. Mkarimu
Filipo = Rafiki wa farasi. Anayependa farasi
Gabrieli = Mtu wa MUNGU
Gamalieli = Zawadi ya MUNGU. MUNGU anatoa thawabu
Gideoni = Anayepiga hadi kufa.
Haruni = Aliyeangaza. Anayeangaa
Hawa = Uhai.
Henoko = Kuweka wakfu
Hezekia = MUNGU ni nguvu yangu
Hosea = Wokovu.
Ibrahimu = Baba wa wengi
Imanueli = MUNGU pamoja nasi
Isakari = Yeye anatoa ajira. Ananipa mshahara
Isaya = YAHWEH anaokoa. YAHWEH ni wokovu
Ishmaeli = MUNGU anasikia maombi
Israeli = MUNGU anapigana. Anapigana na MUNGU
Karmeli = Bustani (ya MUNGU)
Kornelio = Mwenye pembe
Lawi = Umoja. Nia moja
Lazaro = Eleasar = MUNGU ni msaada. MUNGU amesaidia
Lea = Aliyechoka. Mwenye nguvu. Malkia wa nyumba
Luka = Mwanga. Kuangaza
Lutu = Shera. Pazia
Magdalene = Anayetoka Magdala
Malaki = Malaika wangu. Mpeleka ujumbe
Manase = Yeye (MUNGU) amenifanya kusahau
Martha = Malkia
Mathayo = Zawadi ya YEHOVA
Melkizedeki = Mfalme wa busara, Mfalme wa Amani.
Mika, Mikaya = Nani kama YEHOVA
Mikaeli = Nani anayelingana na YEHOVA
Moleki = Mfalme
Musa = Anayevutwa juu
Naftali = Mapambano. Vita vyangu
Naomi = Uzuri wangu. Anayenipendeza. Mzuri
Nathanaeli = MUNGU ametoa
Nathani = Yeye (MUNGU) ametoa
Nehemia = YEHOVA anafariji
Nikodemo = Mshindi wa taifa
Nuhu = Mapumziko
Obadia = Mtumishi wa YEHOVA
Onesimo = Mwenye faida. Anayesababisha baraka
Kwa leo naishia hapo, itaendelea sehemu inayofuata, usikose.
na kama unataka kusomo maana ya majina yaliyopita FUNGUA HAPA
MUNGU akubariki sana ni mimi ndugu yako Peter Michael Mabula Maisha ya ushindi Ministry
0714252292
Comments