MAOMBI YALETAYO USHINDI

Mwl Sospeter Simon S. Ndabagoye
New Elshaddai Ministries NEM-Tanzania.


Katika jina la YESU KRISTO-BWANA WA MAJESHI na mwokozi wa Ulimwengu.
Navuruga hila zote za shetani ndani yangu, napitisha moto wa Roho mtakatifu ung'oe, uharibu na kutekekteza viini vyote vya nguvu za giza, vinavyozuwia nisipone,nisipate amani moyoni,nishindwe kuomba,niwenyonge na kukataliwa. Kwa jina La YESU WA NAZARETH,Naamuru roho ya hofu,kutokujiamini na wasiwasi kwa kila ninachofanya-Kwa jina la Yesu-TOKA! naziamulu roho za uharibifu zote kwa jina la Yesu TOWEKA! Moto wa Roho mtakatifu,ulambe mawimbi yote ya laana,mikosi, mapepo ya kila namna,uchawi na mizimu yote Kwa Jina la Yesu-ONDOKA. Roho ya Uzinzi,majungu,kusingizia kwa jina la Yesu-TOKA.Roho ya umalaya,ulevi na uongo-TOWEKA KWA JINA LA YESU.
Naziapisha roho za mauti, ajari na magonjwa na umasikini,taabu za kila namna Kwa Jina la Yesu-HAUNA NAFASI TENA!

Nijaze roho ya Kukupenda Yesu,nifunike kwa damu yako ya dhamani,niondolee majivuno,kiburi,ulafi na kunijaza hamu ya kukupenda wewe,nipo roho ya maombi na kulisoma neno.KWA JINA LAKO YESU, ili nizidi kuzishinda tamaa mbaya za mwili,hamu ya pombe,sigara, ugomvi na masengenyo.

Niko huru sasa,kwa damu ya Yesu niko juu ya wachawi wote na mamlaka zote,mapepo yote na baba yenu shetani kaeni Kimya kwa Jina la Yesu!Nimefunikwa na damu ya Yesu tangu sasa na hata milele.

                                           AMEN

Mungu akubariki na kukuinua, akufunulie zaidi na zaidi umjue sana na kumpenda, Katika Jina la Yesu Kristo nimeomba.
Mwl Sospeter Simon S. Ndabagoye
New Elshaddai Ministries NEM-Tanzania.


sos.sesi@yahoo.com.
Simu +255 712 909 021.
+255 784/757 464 141.

Comments