Mtwike BWANA fadhaa zako zote ili akuponye





Jina la BWANA YESU lihimidiwe sasa na hata milele.


Karibu ndugu tujifunze  

"......huku mkimtwika yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana kwa mambo yenu" - 1Petro 5:7.

Mpendwa katika KRISTO, neno la MUNGU hapo juu lasema MUNGU anajishughulisha sana na mambo yako. Ndio maana amejishughulisha sana na mambo yako tangu mwaka uanze hadi leo..


Angalia jinsi alivyojishughulisha na kazi zako. Angalia jinsi alivyojishulisha na magumu yaliyokukabili .


Basi ni vyema ukachukua muda huu ukamshukuru kwa hayo.


Mshukuruni MUNGU kwa kila jambo. Lakini pia usichoke kumtwisha yeye haja za moyo wako.


Fadhaa ni yale mahitaji ambayo unahitaji MUNGU akutendee.
Yawezekana unasumbuliwa na njaa, yawezekana unasumbuka kwenye majaribu, yawezekana umeachwa na mme tena ukiwa mimba ya miezi 7, yawezekana ulipata ajali mbaya hata kufanya kazi zako kama kawaida huwezi. Hizo zote ni fadhaa ambazo zinaweza kukusumbua, lakini habari njema ni kwamba MUNGU aliyekuumba anataka akubebee mzigo wako huo  na kukuweka huru.

Kwa MUNGU yote yanawezekana; anaponya na kuokoa.

BWANA YESU anasema tupeleke kwake mizigo yote mizito inayotusumbua, mizigo ya magonjwa, mizigo ya laana, mizigo ya madeni hata mizigo ya mikosi ATATUPUMZISHA. ''Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.-Mathayo 11:28.

Nampenda BWANA YESU maana tukimwita anaitika na kutupumzisha na mateso yote. 

Ndugu yangu haijalishi umeteseka kiasi gani lakini shika neno hili leo ya kwamba BWANA YESU anataka kukupumzisha , ni jukumu lako kukubali na kutii ili ule mema ya nchi. 

Sijajua mzigo wako ni nini
 Sijajua fadhaa yako ni nini lakini napenda kukuambia ya kwamba yupo MUNGU kwa waliookoka na hutenda mambo makuu.

Tena kwake yote yanawezekana .
''kwa kuwa hakuna neno lisilowezekana kwa MUNGU.-Luka 1:37''

 MUNGU ana njia maelfu za kumaliza tatizo lako, jukumu lako ni kumpokea BWANA YESU na kuomba kwa imani maana kila amwendeaye MUNGU lazima aamini kwamba yeye yuko na huwapa dhawabu wote wamtafutao.

Ndugu usilalamike kwa sababu ya shida yako jambo la kufanya ni kulikimbiaza hilo tatizo lako kwa mfalme YESU KRISTO ili akuponye na uwe huru.

Kumbuka jambo hili ya kwamba dhambi na kukusa imani ni vizuizi vikuuu vya kutokujibiwa kwako. 

Acha dhambi na omba kwa imani katika BWANA YESU , lazima utapokea tu baraka yako .
''Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao. -Waebrania 11:6''

Omba kwa imani na utapokea.

Baada ya kujifunza somo hili nakuomba chukua tendo la imani na kuomba kwa imani katika ROHO MTAKATIFU utapokea baraka yao, omba mambo makubwa na sio madogo, omba ukiamni utapokea maana yeyote mtakayoomba kwa imani katika KRISTO mtapokea.
 
 
MUNGU anajishughulisha sana na mambo yako. Upanga wa moto ukulinde siku hii kwa jina la YESU KRISTO..
Ubarikiwe na nakuombea uwe na siku njema.


   na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisha kanisani. ROHO MTAKATIFU aliyenipa ujumbe huu ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA.

                 MUNGU akubariki sana .
                  Ni mimi ndugu yako
                  Peter M Mabula
         Maisha ya Ushindi Ministry.
                   0714252292

Comments