NIMEPATA UKIMWI SABABU SIKUITII SAUTI YA MUNGU

ASOMAYE NA AFAHAMU!!
Naitwa Anna naishi Tabata, nimezaliwa mwaka 1987 hapahapa Dar, nina Elimu ya Chuo Kikuu.
Ninatoa ushuhuda huu uwe onyo na fundisho kwa wadogo zangu na dada zangu. Hapa nilipo ni mwathirika wa Ukimwi. Niliokoka mwaka 2003 na kwa kweli nalimuona Bwana katika maisha yangu ya wokovu,  nilifurahia maisha niliyokuwa nayo kwakweli, washirika na Mchungaji walinipenda sana na pia nilikuwa kiongozi wa sifa pale kanisani. Baada ya kumaliza Chuo na kupata shahada yangu nilifanikiwa kupata kazi katika Benki moja hapa hapa Jijini Dar.

Miaka ikaenda na umri wa kuolewa ulipofika pale kanisani kulikuwa na kijana mmoja alikuwa akimpenda sana Mungu na kujitoa kwa huduma pale kanisani, huyo kijana alitaka kunioa...., nikakubali! Tatizo yule kijana alikuwa na Elimu ya kidato cha nne na alikuwa akifanya biashara ndogo ndogo ambazo zilikuwa zikimwingizia kipato na kuweza
kuyamudu maisha yake ya kila siku. Kuna wakati nilikuwa najaribiwa nimwache kwani niliona hanifai kwani mimi nilitaka mtu mwenye elimu kama yangu au angalau anizidi na pia niliwaza kuwa itakuwa shida kwangu kumtii na kunyenyekea akizungumza kama Kiongozi wa famila na wakati nimesoma kuliko yeye, kweli hilo lilinitesa saaana.
Alipotaka kumwambia Mchungaji juu ya mahusiano yetu nilimwambia tusubiri kidogo tusomane tabia ingawa kiukweli sikuwa na nia hiyo,,, nilikuwa nataka kubuy time ili ikitokea kijana handsome na msomi kuliko huyo atokee ili nibadiri maamuzi. 

Kweli siku ikaja nikiwa natoka kanisani siku moja kijana mmoja tulikuwa tunasali naye alinibeba kwa gari yake njiani kila mmoja alikuwa kimyaaaa!!! Nikawa nawaza moyoni kuwa huyu ndiye mwanaume mwenye sifa za kuitwa mume wangu lakini kamwe nisingeweza kumwambia kitu. Safari ikaendelea tukafika nyumbani akanishusha. Niliumiaaaa sana kwanini hakusema neno lolote?????

Ikawa jioni kisha asubuhi siku nyingine, siku hiyo nikiwa kazini simu yangu ya mkononi iliita moyoni nikawa natamani awe yule kijana. Kuangalia simu ilikuwa ni ya yule kijana kweli, niliruka kwa furaha bila hata kujua anaenda kusema nini.., alinisalimu kisha akaomba anitoe out siku hiyo.., nikwambie ndugu yangu toka niokoke ndio mara ya kwanza
nilimsikia mtu akiniambia kutoka out, na hapo nilijibu bila kufikiri mara mbili.., YEEEEES!!! Alicheka akakata simu nami nikabaki nimeishika ile simu mpaka rafiki yangu pale ofisini aliponishtua akinitania kuwa mapenzi yataniua kwani yeye alijua naongea na yule mchumba wangu kwani walimfahamu baadhi ya rafiki zangu na hapo wapo walionitia moyo kuolewa naye na wengine waliniona zuzu kuwa nataka kuolewa na mtu nisiyeendana naye kwani hakuwa na cash ya kutosha.

Baada ya simu ile kiukweli nilishaanza kumdharau yule mchumba wa mwanzo hata sikutaka hata kuona simu yake wala meseji, nikawa najibu nionavyo ingawa yeye alikuwa mnyenyekevu na siku zote alinitia moyo kuwa ipo siku maisha yatabadirika na kuwa vile nataka.., hapo tena sikutaka kusikia kitu ila huyu kijana mpya.
Siku hiyo tumetoka out tulienda Serena na hiyo ilikuwa mara yangu ya kwanza kwenda hapo kufurahi.., tukiwa hapo tuliongea mengi ila sikusikia lolote juu ya mahusiano, nilianza kumchukia kidogo kidogo. Baada ya masaa kama mawili alisimama akaenda msalani, siku hiyo ndo niligundua kuwa alikuwa ni Mhasibu kwenye Kampuni moja hapa
jijini na alikuwa na Masters so hapo niliona niko na mwenye sifa haaaasa!! Ambaye nilijua ndugu, rafiki na hata kanisani wakijua ndo mtarajiwa nitaheshimiwa zaidi. Aliporudi yule kijana alikaa kimyaa kama mtu aliyekuwa akitafakari jambo.., akaniuliza swali.., Anna will you marry me?? Kweli nilingoja wakati kama huo ufikeeee.., nilitabasamu.., nikajibu.., Yes baby!!
Alisimama akanikumbatia nami bila kufikiria niliitikia. Alinirudisha home siku hiyo nilikuwa na furaha sana. Yule kijana alizidisha upendo kwangu kweli nikajisahau kuwa nimeokoka.., akawa ananichukua kwenda kwake Mbezi Beach tukawa tunashinda wote mpaka usiku, na wakati mwingine nalipotoka kazini nilikwenda kwake bila hata kusema, penzi lilipozidi tukawa tunashiriki tendo la ndoa na kwa jinsi nilivyompenda sikujali kwenda bila kinga sembuse kuwa tutendalo ni dhambi mbele za Mungu. Yule kijana wa mwanzo alipoona vituko vimezidi aliniacha akaoa binti mwingine.

Mchumba wangu mpya nikamwambia tumwambie Mchungaji tuoane akaniambia twende taratibu kwani mimi ndio wake.., nilikubali japo kwa shingo upande. Haukupita muda niliumwa sana, nikalazwa hospitali VIPIMO NILIVYOFANYIWA VILIONYESHA MBALI NA MARALIA KALI NILIYOKUWA NAYO....., NILIKUWA NIMEATHIRIKAAAAA!!
Nililia kwa uchungu saaana, nikajichukia na kumchukia sana yule kijana. Ajabu ni kuwa yule kijana sikumuona tena kuja kuniangalia wala baada ya kutoka sikumuona kanisani tena.

Mdogo wangu na dada yangu, NIPO KITANDANI sasa nikisubiria siku nitaondoka. Nimeandika ushuhuda huu kukuonya...., WEWE MSICHANA MWENZANGU..., SIMAMA NA MUNGU....., MTANGULIZE MUNGU KWA KILA JAMBO...., MACHO YASIKUPOTEZE, ELIMU YAKO, PESA YAKO, UZURI WAKO USIACHE VIKUPOTEZE. MUHESHIMU MUNGU OKOKA KWELI KWELI, KAMA WATEMBEA KWA IMANI BASI AMINI JUU YA MUMEO MUNGU ATAKUPA AFANANAE NAWE KWA VIGEZO
VYAKE NA SIO VYAKO WEWE. USIMCHANGANYE MUNGU HUKU UKIISHI MAISHA MACHAFU MTAANI, USIUFANYE MWILI WAKO KITUO CHA UTALII KWANI HILO NI HEKALU LA ROHO MTAKATIFUUU!! USIMDHARAU MTU KWA NAMNA YOYOTE LEO WEWE HUJUI KESHO YA HUYO MTU...., YULE KIJANA NILIMKATAA SASA NI TAJIRI ANA VITU
VYOTE NILIVYOKUWA NATAKA BUT NOW IT'S TOO LATE KWANI NALITAMANI VITU NISIVYOVITOLEA JASHO. KUBALI MTU SI
KWA VILE ALIVYO TU BALI PIA ATAKAVYOKUWA BAADAE, KUBALI KUANZA SIFURI NAYE MUINUKE PAMOJA, LIENI NA KUCHEKA PAMOJA.., MTABARIKIWA. NAPIGANA VITA NAMI HAPA NIKIAMINI MUNGU AMENISAMEHE NA SIKU MOJA TUONANE MBINGUNI.
Nakupenda sana. Mimi Anna K.
-----------------------------------------------------------------------------------------
Habari hii imetumwa na mtu kutoka mitandaoni.

Comments