POKEA MUUJIZA WAKO KWA JINA LA YESU.

Mwl Sospeter Simon S. Ndabagoye
New Elshaddai Ministries NEM-Tanzania.


Ahsante MUNGU kwa wema wako kwetu! Nakuinua na kukutukuza kwa uzima,neema na ulinzi wako kwa ndugu huyu asomae ujumbe huu!

Kwa jina la YESU,naomba umjalie amani,upendo na furaha kwa juma zima lijalo.

Umjalie riziki,mali na fedha!Mpatie mahitaji yake,kutana na haza zake!Lifanye juma hili kua la miujiza kwake;kwa jina la YESU.

Nakomesha kila mashambulizi yaliyoelekezwa kwako!Shetani na kila nguvu za giza,kwa jina la YESU zivunjike. Laana,mikosi,chuma ulete,utapeli,magonjwa,bahati mbaya!roho za magonjwa vivunjike kwa jina la YESU.






Nakutamkia baraka,uzima,kufanikiwa,BWANA akutokee juma hili,aiguse ofisi yako,biashara yako,uzao na nyumba yako!Kwa jina la YESU pokea mtaji,pokea ajira,pokea mwenza,pokea uzao,pokea uponyaji...

Vyeti vifunguliwe,akili yako,watoto wako ifunguliwe,biashara ikue,upandishwe cheo eneo lako la kazi;KWA JINA LA YESU POKEA ZAIDI YA NILIVYOSEMA.



Mungu akubariki na kukuinua, akufunulie zaidi na zaidi umjue sana na kumpenda, Katika Jina la Yesu Kristo nimeomba.
Mwl Sospeter Simon S. Ndabagoye
New Elshaddai Ministries NEM-Tanzania
sos.sesi@yahoo.com.
Simu +255 712 909 021.
+255 784/757 464 141.

Comments