Siri ya wachawi yafichuliwa na Mtume Peter Rashid Abubakar jijini Nairobi

Mtume Peter Rashid kutoka Dar es salaam akifundisha katika ibada ya mkesha jijini Nairobi
Maelfu wamemiminika katika mkesha  katika huduma ya ATG jijini Nairobi Kenya na wengi saana kufunguliwa kutoka kwenye nguvu za uchawi.  Mhubiri katika mkesha huo na semina ambayo inaendelea ni Mtume. Peter Rashid Abubakar akishirikiana na mwenyeji wake Apostle. Francis Musili ambaye ndiye Founder wa huduma hiyo.


Mtume  Peter Rashid Abubakar Akiwa anafundisha Uchawi wa Ashera( Mika 5:14) alisema watu wengi sana wamerogwa kwa uchawi huo!! 

Alisema uchawi huo, mchawi huchimba shimo dogo ndani yake anaiweka ile mbegu ya Ashera pamoja na Nywele; Kucha; Mate; Mavumbi ya miguu anayehusika; Haja zote kubwa na ndogo. Kabla hajafukia anatamka maneno mfano maisha ya mtu huyu kila siku usiku ifikapo saa saba usiku au saa nane awe mgonjwa saaana lakini ifikapo asubuhi ni mzima kabisaaa! 

Mwingine anaanzisha  Biashara yake mara inakuwa nzuri baada ya muda kidogo  inaharibika kabisaa na madeni lukuku; 

mwengine anakuwa anapata kazi ya muda mfupi tu kazi anafukuzwa bila sababu yeyote n.k

 Mtume. Peter Rashid Abubakar huku zikitokezea amina nyingi nyingi aliwaombea, na matendo makuu ya MUNGU kuonekana na wengi kufunguliwa.  Kwa jina kuu la YESU KRISTO.
Maombezi yakiendelea na watu kufunguliwa
wakati wa semina, mtumishi wa MUNGU Peter Abubakar akifundisha
wakati wa semina:Mtume Peter Rashid Abubakar wakati alipokuwa akizifichua siri za shetani na akihubiri kwa upako wa Kitume na kinabii, watu nao walipokuwa wakimsikiliza mara ,walipokuwa wakibarikiwa waliamua kutoa sadaka ya kujiunganisha na upako huo tena bila kulazimishwa.

 Utukufu kwa BWANA.

Comments