KUOKOKA NI JAMBO LA LAZIMA KWA KILA MWADAMU.

Na mtumishi wa MUNGU Sam Balele
Sijawahi kuona mtu anapewa cake iliyo na vitu vitamu ndani yake halafu anaikataa, ni lazima atafungua mdomo aile, ili imfurahishe kinywani mwake.

 Mtu atakataa kuila cake iwapo ataambiwa kuwa hiyo cake ina sumu ndani yake, hivyo kama atakubali kuila basi itamletea madhara na hata kumsababishia kifo. Hivyo mwanadamu ana hulka ya kukataa vitu vibaya, na si kukataa vitu vizuri.

Sasa ninajiuliza, hivi KUOKOKA kuna ubaya gani? Kuokoka kuna sumu gani ndani yake? Kuokoka kuna athari gani kwa mwanadamu? Hivi nikisema Nimeamini kwa moyo, Nimekiri kwa kinywa, hivyo NIMEOKOKA na nikaanza kuishi maisha ya IMANI hiyo nikiangalia na kujifunza kuwa Neno la Mungu linasemaje kwa habari ya tabia na mwenendo wa mtu aliyeokolewa; NITAKUWA NAPATA ATHARI ZIPI? KUNA UBAYA GANI?

Kwa jinsi Biblia inavyosema kwa habari ya IMANI YA KUOKOKA, kuna faida nyingi zaidi ya hasara, na faida kubwa kuliko zote ni ile AHADI YA UZIMA WA MILELE, JINA KUANDIKWA KATIKA KITABU CHA UZIMA CHA MUNGU MBINGUNI. Hii ni faida kubwa sana, kuwa na ahadi ya urithi katika Yesu Kristo pamoja na watakatifu wa Mungu.

Sasa najiuliza, mwanadamu kwa hulka yake hawezi kupinga kitu kizuri kama hiki kinachozidi utamu wa cake, ambayo huishia chooni. Mwanadamu anapenda mambo mazuri, na kuokoka ni jambo zuri na jema kwa ubadae wa mwanadamu, kwa umilele wake pamoja na Mungu. 

Ila nachojua HABARI YA IMANI YA KUOKOKA si jambo jema kwa Shetani na malaika zake ambao wanataka company katika adhabu waliyokwishaandaliwa, ndomana alisema Ziwa la moto halikuwekwa kwa ajili ya wanadamu, ila kwa ajili ya Shetani na malaika zake. Na sasa wale wanadamu watakaoamua kusikiliza HADITHI, NA MAHUBIRI, NA MAFUNDISHO YAKE SHETANI NAO WATAJIUNGA NAE TU.

Wewe just stop for a minute huo upinzani wako wa KUOKOKA, na jiulize hivi NINACHOPINGA NI NINI HASA? MANAKE HATA KAMA NI UONGO BADO UTAKUWA HUNA HASARA, HIVI UNA HASARA GANI UKISEMA UMEOKOKA ZAIDI YA HASARA YA KUONEKANA KITUKO 

UMECHANGANYIKIWA! NA USUMUBUFU MWINGINE KUTOKA KWA KAMBI YA SHETANI (IKIWA UMEOKOKA NA UMEMAANISHA NA UNAHAKIKISHA KUWA NA UTAKATIFU KATIKA MWENENDO WAKO-1 Petro 1:13-16, 1 Petro 2:11-12).
UKIONA UNAPINGA KUOKOKA, BASI UJUE SI WEWE ILA NI ILE ROHO IKUZINGAYO, AMBAYO SI ROHO YA MUNGU BALI NI ILE ROHO YA MPINGA KRISTO AMBAYO IMEKWISHAKUWAKO ULIMWENGUNI HATA SASA.
MUNGU AKUSAIDIE KUUFUNGUA UFAHAMU WAKO KWA HABARI YA WARUMI 10:9, 10.
MIMI SIIONEI HAYA INJILI KWA SABABU NI UWEZA WA MUNGU UULETAO WOKOVU, KWA KILA AAMINIYE..........WARUMI 1:16
DHEHEBU LANGU KAPUNI, INJILI YA YESU KRISTO KWANZA.

  
Sam Balele

Comments