Salamu za Pasaka kutoka kwa Gasper Madumla

mtumishi wa MUNGU Gasper Madumla



Bwana Yesu asifiwe...
Awali ya yote nimshukuru BWANA Mungu kwa kunipa uzima mimi na familia yangu yote,pamoja na wewe mpendwa wangu usomaye sasa
hivi ujumbe huu maana natumaini na wewe pia ni mzima.
Hakika ni kwa neema na rehema tu hata sasa tu wazima wa afya za rohoni hata za mwilini pia.

Maana kwa kazi yake Bwana Yesu,kazi ya msalaba imetutenga mbali na dhambi,imetupa maisha mengine mapya,hakika yakale yamepita,na yamekuwa mapya.

Haleluya...


Wedding revival party mlima wa moto
Pili;
Nawatakia PASAKA njema marafiki zangu woote,watenda kazi pamoja nami,watu wa blogs,magazines,na wana habari wote wenye kuinjilisha pia hata wewe rafiki usomaye ujumbe huu,
Ninachoweza kusema ni kwamba;

Sikukuu hizi ni za kutulia wewe na familia yako,ukitafakari mateso na ufufuko wa Bwana Yesu Kristo aliyekufia msalabani kwa sababu ya dhambi zako,na zangu pia,kisha akatuweka huru,huru kweli kweli.

Zaidi ya yote Mungu akupiganie na nuru ya maisha ya WOKOVU yakushukie,UOKOKE ili hata kama unasherekea sikukuu hizi basi ujue ni nini unasherekea pasipo kufuata mkumbo wowote ule.

Mungu wa mbingu,akubariki na mibaraka yote,
Akulinde,akupe uzima wa rohoni na wa mwilini pia,
Ninaomba hayo yote katika Jina la Uweza la Yesu Kristo,
na useme;

AMEN.

Comments