USHUHUDA:USIACHE KUOMBA HADI UPOKEE



Kuna ndugu mmoja alikua na kaka yake mgonjwa sana na hawezi kugeuka kitandani. Huduma zote zilifanyika kitandani kwa muda mrefu. Kila siku asubuhi huyu ndugu alienda chumbani kwa kaka yake kuomba kwa ajili ya uponyaji wa ndugu yake. Kwa jinsi ya mwilini, hakuona kitu kinatokea kwa muda mrefu.

Haikumkatisha tamaa kwamba anomba halafu haoni nafuu. Aliendelea kuomba kila siku. Siku moja
baada ya kuomba kwa muda mrefu sana, aliamka asubuhi kama kawaida na kwenda kuomba. Alipomaliza akaamka ili atoke chumbani kwa kaka yake. Akiwa mlangoni, akasikia mtu yuko nyuma yake. Natazama! alikua ni ndugu yake alikua akimfuata huku anatembea mwenyewe baada ya muda mrefu kitandani.

Huyu ndugu alimkumbatia kaka yake na kumshukuru Mungu sana kwa muujiza.

Kama kuna kosa unaweza kufanya ni kukata tamaa ya kuomba kwa sababu tu eti huoni mabadiliko. Ni kweli yamkini kwa nje huoni, ila kila uombapo jua kuna kitu kinatokea katika ulimwengu wa roho na iko siku kitadhihirika katika mwili pia.

Bwana anatenda na atatenda kwako pia.

Mungu akubariki sana,

Comments