
Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Mashariki ya Ziwa Victoria (DMZV), limeitaka Serikali kuhakikisha inawatafuta watu waliohusika na tukio la bomu lililolipuka kanisani hapo juzi.
Pia, limewataka Wakristo kuwa watulivu, wasiogope wala wasitishwe na mashambulizi hayo na kwamba wasilipize kisasi.
Akizungumza kwenye Kanisa la Imani Makongoro
Misheni jana, Askofu wa KKKT Dayosisi ya Mashariki Ziwa Victoria, Andrew
Gulle alisema wanaamini shambulio hilo ni la kigaidi na kwamba,
Serikali inapaswa kuchukua hatua ya kuwasaka wanaohusika.
“Kanisa tunaamini tukio hili linahusiana na
ugaidi, umefika wakati Serikali ikachukua hatua za kuwasaka waliohusika
ili sheria ifuate mkondo wake,” alisema Gulle.
Hata hivyo, wachambuzi wa masuala ya dini wanasema
huenda tukio hilo linatokana na migogoro inayoendelea kanisani hapo kwa
sababu tayari kuna baadhi ya waumini wamejitenga kwa kuanzisha kanisa
lingine
.
.
“Wasikwepe matatizo yao ya ndani, kuna askofu
aliuawa kwa kupigwa tofali kutokana na migogoro, hivyo hata hili (tukio)
litakuwa ni migogoro inayoendelea,” alisema mmoja wa waumini ambaye
hakutaka kutajwa jina lake.
Askofu Gulle alikanusha kuwapo kwa migogoro
kanisani hapo na kwamba, tukio hilo halihusiani na mgogoro wowote ndani
ya Kanisa bali ni ugaidi.
Majeruhi aendelea vizuri
![]() |
hili ndilo kanisa ambalo Bomu hilo lilipuka katika moja ya maeneo ya Jengo hilo |
![]() |
Mhudumu wa nyumba ya kupumzikia wageni wa Kanisa la KKKT Dayosisi ya Mashariki ya Ziwa Victoria, jijijini Bernadetha Alfred (25) akiwa amelazwa katika Hospitali ya Bugando baada ya kulipukiwa na Bomu hilo jijini Mwanza |
Comments