CHANZO CHA BLOG YA MAISHA YA USHINDI.




BWANA YESU asifiwe.
Kama Wewe Ni Mgunduzi Wa Mlima Kilimanjaro, MUNGU Ni Muumbaji Wa Mlima Huo Na Sisimizi Wapo Pale Kabla Wewe Hujaenda Na Hawajiiti Wagunduzi. 

Kama Wewe Ni Mgunduzi Wa Ziwa Victoria, MUNGU Ni Muumbaji Wa Ziwa Hilo Tena Yeye Alijua Kuna Maji Lita Ngapi Ziwani Kabla Wewe Hujaja, Na Ajabu Kuna Sangara Na Sato Ambao Wako Ziwani Kabla Yako Na Hawajiiti Wagunduzi.

Mimi Peter Si Mdunduzi Wa Chochote Ila MUNGU Hugundua Viti Vingi Kwa Ajili Yangu. Mfano September 2012 MUNGU Alisema Nami Kwa Njia Ya Ndoto Jinsi Ya Kutengeneza Blog Na Website, Akinielekeza Kipengele Kwa Kipengele, Nilipoamka Asubuhi Nikaandika Maelekezo Ya MUNGU Na Kuyafanyia Kazi, Kwa Urahisi Sana Nikatengeneza Blog Yangu Ya www.maishaushindi.blogspot.com. 
Sijawahi Kusomea Computer Wala Mambo Ya Blog Hata Kwa Dakika Moja Lakini MUNGU Alinipa Bure Elimu Hii. Na Baada Ya Hapo Nimewatengenezea Watumishi Blog Zaidi Ya 7. Namshukuru MUNGU Kwa Hilo Moja Katika Yale Mengi Sana Alionitendea Na Heshima Na Utukufu Tumpe Yeye Milele. 
 
                  Katika blog hii
 
 -Habari ya kwanza kupost ni ''NILITAKA KUJIUA.'' HII HAPA,FUNGUA .
-Habari iliyosomwa kuliko zote ni ''HISTORIA YA ASKOFU MOSES KULOLA'' imesomwa mara 4010 hadi tarehe 31 May  2014 HII HAPA,FUNGUA
-Aina za habari zilizosomwa zaidi ni shuhuda mbalimbali zikifuatiwa na Historia mbalimbali za watumishi.
-Hadi 31 may 2014 blog hii ilikuwa imesomwa mara 223,925.
-BWANA YESU ametukuzwa na atatukuzwa milele mahali hapa.
 
                     Shukrani. 
1. Kwa MUNGU BABA.
2. Kwa waliosoma blog hii wote.
3. Kwa waliotuombea ili tufanye vizuri zaidi.
4. Kwa blog marafiki ambao tunashirikiana nao.
5. Kwa blog zote ambazo walitumia habari za kutoka hapa.
6. Kwa watumishi wa MUNGU wote ambao masomo yao yanatumika hapa, hii yote ni kwa ajili ya kuujenga mwili wa KRISTO.
7.Kwa wote ambao tumewaombea na sasa wanaishi maisha ya ushindi dhidi ya dhambi katika KRISTO YESU BWANA wetu.

Ndugu Zangu Tumpe MUNGU Sifa na utukufu siku zote za maisha yetu.

Comments