Na Mchungaji
kiongozi Josephat Gwajima, UFUFUO NA UZIMA.
|
Utangulizi
Zaburi 116:1-19
Madhabahu,
Kafara ya madhabahu, kuhani wa madhabahu, Mungu wa madhabahu na nguvu ya
madhabahu.Utaona kwenye biblia watu wengi wa Mungu mfano Ibrahimu, Nuhu na Yakobo
walitengeneza madhabahu ili wapate kukutana na Mungu. Eliya alipoitengeneza
madhabahu ya Yehova iliyokuwa imevunjika , Eliya alikuwa kuhani wa madhabahu na ng’ombe aliyemchinja
alikuwa kafara ya madhabahu na moto uliotoka madhabahuni ndiyo nguvu ya
madhabahu na Mungu wa madhabahu alikuwa Yehova.
Hivyo Mungu hawezi kutenda kazi isipokuwa kwa kupitia watumishi wake
manabii, wachungaji, wainjilist, mitume.
Shetani naye vile vile hawezi kutenda kazi mwenyewe kwa maana yeye ni
roho kwa hiyo lazima atumie watumishi wake wachawi , waganga, wasoma nyota ,
wafuga majini , watabiri na madarueshi.
Madhabahu ni daraja au kiunganishi kutoka
ulimwengu wa roho kwenda ulimwengu wa mwili au kutoka ulimwengu wa mwili kwenda
ulimwengu wa roho. Na kuhani anapokuwa
madhabahuni anabeba vitu kutoka
ulimwengu wa roho na kuvileta ulimwengu wa mwili kwa watu. Hata bwana Yesu
alipokuwa msalabani kalvari alifanyika
kafara/sadaka na damu yake ilipomwagika pale kalvari inaendelea kunena hata
sasa kwa hiyo kalvari ikafanyika madhabahu
ya wokovu. Kwa hiyo kila damu inayomwagwa huwa inanena maana imeandikwa na damu ya Yesu kristo mjumbe wa agano
jipya inenayo mema kuliko damu ya Abili
ineneayo kisasi. Hii inatudhihirishia kuwa katika dunia hii zipo kafara
nyingi za damu zinazotolewa na wachawi
lakini tunaposema damu ya Yesu inaharibu
kafara zote.
Utaona kwenye
historia sehemu zote ambazo ukristo ulianzia kwa sasa sehemu hizo ndiyo makao
ya shetani, kwa mfano bustani ya Eden Mungu alipokuwa anatembea wakati wa jua kupunga kwa sasa mahali pale
ndiyo Iraq ya sasa yaani ni ngome ya Uislam. Dameski mtume Paulo
alipokuwa anaenda kuwakamata walokole safi kwa sasa mahali pale kunaitwa Siryia
yaani nchi ya kiislam . Ufunuo 1:2-6, utaona mahalii ambapo
kulikuwa na makanisa saba ambayo mtume Paul aliwaandikia waraka kwa sasa mahali
pale panaitwa Uturuki yaani nchi ya kiislam. Sasa unaweza kujiuliza kitu gani
kilitokea mpaka mahali patakatifu kukageuzwa kuwa ngome za majini na Uislaam.
Hii ni kwa sababu shetani alifanya ya hila ya kuwainua watawala ambao ni makuhani
wake ili watende kazi na hatimaye
watokomeze ukiristo na ushetani (uislaam) Ukaimarika. Uislaam unaendana na
ushetani kwa maana imeandikwa kila Roho isiyokiri kwamba Yesu Kristo ni bwana haitokani na Mungu kwa hiyo maeneo yote yanayoongozwa na uislaam
ni ngome za kishetani.
Utaona
hata
mahali pale Yesu alipozaliwa Bethelehem na kupelekwa Misri ili asiuawe
na
Herode na huo ulikuwa unabii ya kuwa wakati wa mwisho injili ya uamsho
ya
kuokoa ulimwengu mzima dunia itaanzia Africa, lakini sasa utajiuliza
mahali
pale ambapo Yesu alillewa na sasa imekuwa nchi ya kishetani (Kiislam).
Utaona
pia mahali alipozaliwa Yesu Bethelehem kwa sasa mahali pale ni nchi ya
Waparestina yaani waislam. Yote haya yalitokea kwa sababu shetani
aliyateka
maeneo hayo na kuyatawala kwa kujenga madhabahu zake na kuwaweka
makuhani wake.
Utaona pia rais wa Uingereza , King James ndiye alitafsiri
kitabu cha King James version , hii ina maana kuwa nchi yote ilikuwa
chini ya
ukristo lakini sasa shetani anatawala mpaka kuna ndoa za jinsia moja
pale. Misri pia ilikuwa nchi ya kikristo lakini alipoingia
rais mmoja kuhani wa kishetani alitoa amri kuwa hakuna kukarabati wala
kujenga
kanisa kwa hiyo makanisa mengi yakaharibika na kuisha wakati huo
misikiti
ikaongezeka kila mahali.
Lakini tunaamini na kutumaini kwamba ukristo ni dini ya kurudisha kama Mungu wetu alivyo Mungu wa kurudisha kwa
mfano aliwarudisha wana wa Israel kutoka utumwani Misri , aliwarudisha wayahudi
kutoka utumwani Babel na alimrudisha Yesu kutoka Misri alipofariki mfalme Herode. Kwa hiyo maeneo
yote yaliyotekwa na shetani yatarudishwa kwa jina la Yesu na kila kitu
kilichotekwa na kuibiwa kwenye maisha yetu leo kinarudishwa kwa jina la Yesu.
Shetani
alifanikiwa kuyateka maeneo matakatifu na kuyageuza kuwa ngome zake kwa
kuwatumia makuhani wake yaani wachawi na wasoma nyota. Hata leo kwenye maisha
yako inawezekana kuna makuhani wa kishetani waliotumwa kuharibu maisha yako,
lakini leo tunaamuru moto kutoka mbinguni na kuwala wote kama Eliya alivyoamuru
moto kutoka mbinguni ukawala wale wajumbe hamsini walitumwa na mfalme ili
wamkamate.
Ili kazi ya
Mungu iende vizuri lazima wawepo makuhani wa Mungu ili wanapozungumza ni kama
Mungu amezungumza, wanapobariki ni kama Mungu kabariki. Shetani naye anatenda
kazi kupitia makuhani wake yaani wachawi , waganga nakadhalika. Kwa mfano mtu
anaweza kuwa anamchukia mtu na akaamua kwenda kwa kuhani wa shetani yaani
mganga na kumwambia nitengenezee mambo na mtu Fulani aharibikiwe kwa hiyo
kuhani anatuma mashetani na yule mtu matatizo yanampata Matendo
13:6-8
1krintho 4:20, Ufalme wa Mungu hauwi
katika maneno bali unadhihirishwa katika nguvu, kwa hiyo leo tunatumia nguvu ya jina la damu ya Yesu
kuwaharibu makuhani wa kishetani na baada ya hapo maisha yetu yataenda vizuri .Shetani
ana namna mbili ya kumshambulia mtu
Anaweza kumshambulia mtu akiwa nje ya mtu Zekaria
3:1-4, 1thesalonike 2:19, Anaweza kutenda kazi akiwa ndani ya mtu yaani kumpagaa. .
Maombi
Kwa damu ya Yesu ewe baba Mungu naomba msahaha
kwa jambo lolote nililotenda likamfanya shetani anishambulie. Kwa jina la Yesu
Nafunga milango yote ambayo shetani alikuwa anatumia kuja kinishambulia ,
nafunga milango ya hasira ,kiburi, laana za ukoo kwa jina la Yesu. Kwa mamlaka
ya jina la Yesu namteketeza kila kuhani wa giza anayefanya vita na maisha
yangu, nawafyeka mashetani wote na wakala
wa laana zote kwa jina la Yesu.
Kwa
jina la Yesu mtu yeyote katika familia yetu anayejihusisha na uchawi leo namfyeka kwa jina la Yesu. Mtu yeyote
anayefanya uchawi kwenye maisha yangu namfyeka kwa jina la Yesu. Kwa jina la
Yesu mtu yeyote kwenye familia yangu
anayetumiwa na shetani kunileta magonjwa , balaa au mikosi leo namfyeka kwa
jina la Yesu. Imeandikwa mimi ni rungu la bwana kwa hiyo natangaza leo mtu
yeyote aliyetuma mashetani wa ,aibi,
umasikini namvunja kwa jina la Yesu .
Naharibu kazi ya kuhani mwanamke, Mtoto, kijana kwa jina la Yesu . Nabomoa
madhabahu zote zilizojengwa ili kuharibu biashara yangu, kazi yangu ,watoto wangu .Imeandikwa kila silaha
itakayofanyika juu yangu haitofanikiwa, kwa jina la Yesu sila ya mauti, ajali,
kukataliwa kushindwa hazitofanikiwa zote kwenye maisha yangu kwa jina Yesu.
Kwa
damu ya Yesu leo nawazunguka watu wote wanaonihusu ili wasishambuliwe na nguvu
za giza ili kila jini aliyetumwa
kuniharibia mipango yangu kupitia watu hao asipate mlango kwa jina la Yesu.
Imeandikwa hakika hakuna uchawi juu ya Yakobo wala uganga juu ya Yakobo nami
nakataa kufa kwa jina la Yesu Imeandikwa sitakufa bali nitaishi nakataa
kufa kwa magonjwa, ajali au sumu kwa jina la Yesu.
Kwa
jina la Yesu kila mtu aliyepanga vita juu yangu namshinda kwa jina la Yesu,
aliyepanga vita ya uchawi au akilia namfyeka kwa damu ya Yesu. Natwaa mamlaka
ya kuharibu nguvu na uwezo wa giza kwa jina la Yesu. Imeandikwa hivyo Mungu
alimwadhimisha mno akamkirimia jina lipitalo majina yote kwa jina la Yesu nawateka
nyara makuhani wote wa giza na majeshi yao nawaponda kwa jionala yesu.
Nawateketeza watu wenye nia mbaya na taifa letu la Tanzania naziharibu
madhabahu zao na kafara zao naziharibu kwa damu ya Yesu. Kila kuhani wa ibilisi
aliyetumwa kusimama kwenye taifa la tanzania leo natumwa moto ikilu, kwenye
bunge na baraza la mawazirin na kumteketeza kwa jina la Yesu. Kila nguzo za
ufalme wa giza leo tunaziharibu kwa jina la Yesiu. Moyo wa kishetani waliovaa
na nia zao leo tunazipurura kwa jina la Yesu. Imeandikwa Mungu wetu na Mungu wa
vita kwa jina la Yesu leo natangaza vita katika ulimwengu wa roho na kuwafuata
majeshi yote ya giza. Imeandkiwa amelaaniwa kila mtu hauzuiaye upanga wake
kumwaga damu kwa jina la Yesu leo nautoa upanga Alani na kuwafyeka wachawi,
mapepo mizumu kwa jina la Yesu.
Kila
kuhani aliyetumiwa kuharibu maisha yangu namtekeketza imeandikwa kila silaha itakayofanyika juu
yangu haitafanikiwa, silaha ya balaa, silaha ya magonjwa, ajali, mauti hazitafanikiwa
kwa jina la Yesu , leo nimeshindana na nimepenya na kuingia katika Baraka zangu kwa jina la
Yesu.
![]() |
Maelfu wakiwa katika Nyumba ya Ufufuo na Uzima
|
Comments