1Falme 18:15-30,1Falme 19:15-22,2 Falme 10:1-15
Kwenye biblia Mungu anawachukia sana wachawi, imeandikwa
usimwache mwanamke mchawi kuishi, makuhani wa kichawi ndiyo hao unaweza kuwaita
wataabishaji. Mungu ni roho kwa hiyo
hawezi kutenda Kazi kwa wanadamu hivyo huwatumia watu ili kutenda kazi ambao ni
makuhani wa Yehova, Shetani naye ni roho naye anatenda kazi kwa kutumia watu
ambao ni wachawi, waganga, madarueshi na wanajimu ambao tunawaita makuhani wa shetani.
Utaona hata Mungu alipotaka kuja
duniani alivaa mwili akazaliwa kama
mwanadamu Yesu Kristo. Kwa hiyo hata shetani anakuwa na nguvu pale anapokuwa
amevaa mwili. Mungu aliagiza wachawi wapigwe kwa mawe lakini leo tunayo njia
ambayo tunaweza kuwaangamiza wataabishaji wa watu (makuhani wa shetani) na mawe
hayo ni neno la Mungu kwa maana imeandikwa neno la Mungu ni nyundo ivunjayo
mawe vipande vipande.
II.
SOMO
1Falme 18:15-30 , Eliya aliwakusanya makuhani wa baali mia nne na
makuhani wa ashera mia nne hamsini akawapeleka mlima karmeli ili watoe sadaka
kwa Mungu wao baali naye atoe sadaka kwa
Mungu wake Yehova ili Mungu atakayejibu kwa moto ndiye awe Mungu wa Israel kwa maana nyakati zile watu walikuwa
hawawezi kumjua Mungu wa kweli. Lakini makuhani wa baali walimwita mungu wao
wala hakujibi, ilipofika jioni ikawa zamu ya Eliya, ndipo Eliya alipoitengeneza
madhabahu ya Yehova iliyokuwa imevunjika na akaweka mawe kumi na mbili
kulingana na kabila kumi na mbili za Israel. Baada ya hapo alichinja ng’ombe awe kafara na akaimwagia maji mapipa manne
halafu akaomba baba Yehova leo ujulikane kuwa ni Mungu, ndipo moto uliposhuka
ukairamba sadaka na watu wote wakasema Yehova ndiye Mungu. Baada ya hapo Eliya akawachinja makuhani wote
wa baali na ashera na jumla yao ni mia nane na hamsini kwa maana alijua
wakibaki hai wanaweza kujenga madhabahu ya baali na kuendeleza uchawi wao. Na leo kwa jina la Yesu tunawakusanya wachawi
wa pande zote waliotesa maisha yetu na kuwapiga wote.
III.
ILI MUNGU
ATENDE KAZI ANAHITAJI MAMBO YAFUATAYO:
·
Madhabahu
(Isaya 19:14-15) Eliya alitengeneza
madhabahu kwa maana Mungu hawezi kushuka bila kuwepo madhabahu yake kwa maan nyakati
zile madhabahu ya Yehova ilikuwa imevunjwa na madhabahu ya baali ilikuwa
imeimarishwa.
·
Kuhani
wa
madhabahu,ni mtu anayesimama kama wakili wa Mungu ,Eliya alikuwa kuhani wa
Yehova.
·
Kafara ya
madhabahu , Eliya alichinja ng,ombe kama kafara ya madhabahu.
·
Mungu wa
Madhabahu, Eliya alikuwa anamwabudu Mungu Yehova kwa hiyo Yehova ndiye
aliyekuwa Mungu wa madhabahu ya Eliya aliyoitengeneza.
·
Nguvu ya
madhabahu, Eliya alipoomba moto
ulishuka, moto ulioshuka ndiyo nguvu ya madhabahu
IV.
ELIYA
KABLA YA KUPAA ALIWATIA MAFUTA WATU WATATU ILI WATENDE KAZI PAHALA PAKE
1Falme 19:15-22, Mungu alimwambia Eliya kabla hajapaa awatie mafuta watu watatu ambao watasimama badala yake, alimtia mafuta Yehu
awe mfalme wa Israel, alimtia mafuta Elisha awe nabii badala yake na alimtia mafuta Hezael awe mfalme wa Yuda ili
mchawi yeyote atakayepona kwa upanga wa Hezael upanga waYehu au Elisha
hautamkosa. Hii inatufundisha kuwa Mungu ni Mungu wa mipango madhubuti kwa
ajili ya kazi na watu wake hivyo huwainua manabii na watumishi wake kizazi hata
kizazi ili ufalme wa giza ubomolewe kabisa.
2 Falme 10:1-15, mfalme Yehu alipoanza kutawala akawaagiza
watumishi wake wamletee vichwa sabini vya wana wa Ahabu (mchawi) kwenye kikapu.
Hii inatufundisha kuwa Mungu hapendi kabisa wachawi na leo kwa jina la Yesu
katika ulimwengu wa roho tunaamuru vichwa vya wachawi vifyekwe mahali popote na
kuletwa hapa na baadaye tunaviteketeza kwa moto kwa jina la Yesu.
2Falme 10:18-28
,Baada ya hapo mfalme Yehu aliamua kuwaangamiza
makuhani wote wa baali akapanga hila na kusema , mimi nimeamua
kumtumikia baali
hivyo nawaomba makuhani wate wa baali mkusanyike pamoja ili tumfanyie
baali
ibada na kafara, walipokusanyika ndipo alipoamuru wachinjwe wote na
hivyo
akawakomesha makuhani wa baali katika utawala wake. Na baada ya
kuwaangamiza makuhani wa baali
akaivunja madhabahu ya baali na mahali pale akapafanya kuwa choo mpaka
leo. Hii
inatufundisha kuwa Mungu hapendi kabisa wachawi waishi katika maisha ya
watu
wake, na leo kwa jina la Yesu katika ulimwengu wa roho tunawakusanya
wachawi
wote, waganga, madarueshi, wafuga majini na wanajimu na tunawachinja
wote na
kuwaangamiza wote kwa jina la Yesu, na madhabahu zao tunazibomoa na
viwanja vyote wanapokusanyika wachawi tunavigeuza kuwa jalala kwa
jina la Yesu.
Namna
ya kumwangamiza mtu
anayetaabisha maisha yako kwa mfano mtu
unayemwota sana kwenye ndoto anakufanyia vimbwanga au ambaye moyo wako
unakushuhudia kuwa Fulani ndiye anayekutesa basi ili umwangamize lazima
umtaje kwa jina lake ukisema Fulani leo nakuangamiza kwa jina
la Yesu.
V.
MAOMBI
Kwa jina la Yesu waliofunga
biashara yangu, promosheni yangu, ndoa yangu, fedha zangu leo nawakusanya kama
Eliya alivyowakusanya makuhani wa baali na kuwachinja nami leo nawakusanya na
kuwaangamiza kabisa. Leo napenya na kupita katikati ya wachawi wote kwa maana
katika ulimwengu wa roho nimebeba silaha za Mungu.
Leo napambana na kazi za
kishetani, Mtu yeyote aliyetesa maisha yangu namwangamiza kabisa kwa jina la
Yesu. Leo nafanya vita na mwanadanu yeyote anayetumiwa na shetani kuharibu
maisha yangu kwa jina la yesu. Kila mapango, vibanda na ngome vya kichawi leo
navibomoa na nyota yangu iliyofichwa humo itoke kwa jina la Yesu.
Kwa damu ya Yesu naamurisha kila
aliyenifunga mimi ajulikane sasa, ninawakusanya wanawake , wanaume, watoto na vijana
wachawi na leo ndiyo mwisho wao nawafyeka wote kwa jina la Yesu. Nawakusanya kwenye
ulimwengu wa roho walionizuia nisiolewe, walionizuia nistajirike, walionizuia
nisisafiri nawakusanya kutoka bahari, angani na kwemye mapango yao na leo
nawaangamiza wote kwa jina la Yesu. Nawakusanya wote waliofanya vita na familia
yangu, nawakusanya wote walionifanya nikataliwe wote nawaleta hapa na
kuwaangamiza kwa jina la Yesu.
![]() |
Maelfu wakiwa katika Nyumba ya Ufufuo na Uzima |
Namkusanya mjomba, shangazi ,
dada mkubwa,kaka mkubwa, mama wa kufikia, jirani yangu,boss wangu kutoka
kijijini na mahali popote walipo na leo nawateketeza kwa jina la Yesu.
Nawakusanya walionifanya nisifanikiwe, walionipaka matope usoni ili nikataliwe,
nawakusanya wachawi wote kwenye mikoa yote ya Tanzania na kuwaleta hapa na nawakata
nguvu zao, nawafyeka wote kwa damu ya Mwanakondoo.
Kwa jina la Yesu ikiwa ndani
yangu imewekwa roho ya uchawi bila mimi kujua naamuru vunjika ewe roho ya
uchawi kwa jina la Yesu. Alama zozote za kichawi zilizowekwa kwangu leo nazifuta
kwa damu ya Yesu. Leo nakuteka nyara ewe mchawi mkuu wa Tanzania na silaha zake
zote nakufyeka kwa jina la Yesu. Nawakusanya wachawi wote waliowekwa kusimama
kinyume na kanisa na kazi ya Mungu nawafyeka
wote kwa jina la Yesu.
AMENI
Comments