WEWE UKO WAPI?

Wewe uko wapi?

BWANA YESU asifiwe ndugu yangu.
Ni mara nyingi sana huwa namshukuru MUNGU ninapoona maelfu ya watu wamehudhuria mbele ya MUNGU kujifunza neno la MUNGU, Kupokea uzima wa BWANA YESU , Kumpa maisha yao BWANA YESU.

Watumishi wa MUNGU hujitoa sana ili tu injili imfikie kila mtu. Kuna Mchungaji mmoja rafiki yangu alifunga siku 11 bila kula wa kunywa chochote ili MUNGU aguse wanadamu ambao watakuja katika mkutano wa siku 3  wa neno la MUNGU ambapo mchungaji huyo alikuwa ni mfundishani. Watu waliokoka na wengi walifunguliwa, hakika injili inasonga mbele.
Watumishi wa MUNGU wengi hujitoa miili yao dhabihu kama neno linavyoaagiza ili tu wewe uokoke.

 Warumi 12:1-2 ( Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake MUNGU, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza MUNGU, ndiyo ibada yenu yenye maana. Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya MUNGU 

Wengine hawakulala usingizi ili wewe na mimi tuupate uzima wa kweli ulio katika KRISTO YESU. 
Yawezekana ulihudhuria mara moja tu mkutano wa injili  kwa lengo la kuponywa ugonjwa wako, na MUNGU siku hiyo hakukuponya kwa sababu alikujua unataka kupona tu harafu uondoke na kwenda kuwasimanga wahubiri.
Yawezekana ulihudhuria mikutano ya injili lakini umerudi nyuma je kwa sasa huihitaji tena mbingu?
Yawezekana ulienda kushangaa watu tu.
Ndugu yangu penda mahubiri na penda uzima wa milele, na kama utapenda uzima wa milele utakuwa unampenda YESU KRISTO maana uzima wa milele hauko kwingine nje na yeye. Na siku zote BWANA anawatuma wahubiri hao unaowaona ili wewe umruhusu yeye YESU kutawala maisha yako.
Ni wakati wa kumpa YESU maisha yako maana kesho huijui itakuwaje.


Kuna watumishi wa MUNGU wameonekana kama vichaa mbele ya watu ambao ufahamu wao umetekwa na shetani lakini hawakukata tamaa, lengo na nia ya mioyo yao ni watu wampokee BWANA YESU kama BWANA na MWOKOZI wa maisha yao kama neno la MUNGU linavyosema  ''Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa MUNGU, ndio wale waliaminio jina lake; waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa MUNGU-Yohana 1:12-13''.

Ndugu yangu yawezekana hujawahi kuona umuhimu wa kuhudhuria mikutano ya injili, yawezekana ukiwaona wahubiri unawaona tu kama watu waliokosa kazi, yawezekana mahubiri yao unayaona kama kelele tu  lakini napenda kukutaarifu kuwa mahubiri yote ambao utayasikia iwe ni redioni, sokoni au popote ni MUNGU anakuhitaji wewe ili tu usiende motoni.
Maelfu ya watu wanaokoka lakini yawezekana wewe haumo kwenye orodha hiyo, unadhani ni kwanini haumo?

Wengi wanakimbilia uzima wewe uko wapi? 
Wengi wanamhitaji YESU usiku na mchana je wewe uko wapi?
Wengi wanaokoka, je wewe uko wapi?
Wengi wanatamani mahubiri kila siku, wewe je?
Wengi majina yao yanaandikwa kwenye kitabu cha uzima, wewe je?
Nakushauri kumpokea BWANA YESU leo na utaona mabadiliko makuu sana.
MUNGU akubariki sana na hapo chini ni picha mbalimbali katika mikutano ya injili ambapo maelfu ya watu wanaokoka lakini yawezekana wewe hauko katika orodha hiyo ya wateule wa MUNGU kwa sababu tu hukuhudhuria mahubiri.

J-XVkWKfsxmEV0eTJrZp7JTV0u copy_BIG
Daniel Kolenda kutoka marekani, hapa ilikuwa mwaka jana katika mkutano mkubwa wa injili  jijini Dar es salaam nje ya uwanja wa Taifa , maelfu ya watu wanampokea YESU lakini yawezekana wewe haumo kwenye kundi kama hili kwa sababu ulikataa kuhudhuria au unadhani humhitaji YESU kwa sasa.

Mchungaji  Frolian Katunzi, hapa watu wakipokea muuujiza yao kutoka kwa BWANA YESU, muujiza mkubwa kuliko yote ni kumpokea BWANA YESU kama BWANA na MWOKOZI wa maisha. wewe yawezekana huhitaji kuhudhuria katika ibaada kama hii, unadhani ni kawnini? je huhitaji mbingu? kundi kubwa kama hili wanamhitaji YESU lakini wewe haumo, je uko wapi?

Mtumishi wa MUNGU Adam Haji Mohamed Kutoka Somalia akihubiri hapa Tanzania na watu wengi tu wakiokoka lakini yawezekana wewe haumo katika wale wanaompokea BWANA YESU, unadhani ni kwanini?. Hapa watu wengi wakifunguliwa na kuokoka lakini yawezekana wewe haumo kwenye kundi la wanaompokea YESU, unadhani ni kawnini/ je uko wapi? je huitaki mbingu leo?



Mchungaji Josephat Gwajima katika mkutano wa injili jijini Arusha. Maelfu ya watu wanaokoka, je wewe uko wapi? . kundi kubwa kama hili wanamhitaji BWANA YESU je wewe uko wapi/ je leo huitaki mbingu?



%_tempFileNameP9093194%
Mwl Christopher Mwakasege akifurahia jinsi watu wanavyotoka mbele ili kumpokea BWANA YESU kama BWANA na MWOKOZI wa maisha yao. Yawezekana wewe haupo kwa sababu  hukuhudhuria, je utampokea YESU lini? au je leo hutaki mbingu?. umealikwa mara ngapi kuhudhuria ibada, semina au mikutano ya injili lakini hukuona umuhimu wa MUNGU anayetaka kukuponya na kukuokoa?



photo (32)
Mwl Mwakasege katika maombezi.


Mtume Peter Nyaga. hapa maelfu ya watu wanampokea YESU lakini yawezekana wewe haumo kwa sababu ulikataa kuhudhuria.
 
Kwa leo naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. ROHO MTAKATIFU aliyenipa ujumbe huu ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA.
                     MUNGU akubariki sana .
                      Ni mimi ndugu yako
                       Peter M Mabula
                 Maisha ya Ushindi Ministry.
                           0714252292

                 MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili.

 MUNGU Akubariki.

Comments