Askofu Kiongozi wa Kanisa la Moravian nchini, Alinikisa Cheyo. Picha na Maktaba
Na Lauden Mwambona, Mwananchi
Cheyo alitoa kauli hiyo jana ikiwa ni siku moja
baada ya Waziri Chikawe kutishia kulifuta kanisa hilo na madhehebu
mengine yatakayoendekeza migogoro.
Akizungumza Dar es Salaam kwenye maombezi ya
kuliombea Taifa yaliyoandaliwa na Jumuiya ya Karismatiki Katoliki Jimbo
Kuu la Dar es Salaam juzi, Chikawe alisema Kanisa la Moravian lina
migogoro inayosababisha hata waumini wake wapigane hadharani wakati wa
ibada.
\
\
Waziri wa Mambo ya Ndani, Matthias Chikawe ©Mwananchi |
Kutokana na kauli hiyo, Askofu Kiongozi huyo
alijibu jana akisema: “Waziri hana uwezo wa kufuta kanisa kwani ni la
Mungu, lakini migogoro itamalizwa na sisi wenyewe.”
Kwa kipindi kirefu kanisa hilo limekuwa na migogoro maeneo ya Tabata na Mwananyamala, Dar es Salaam na Jimbo la Kusini Mbeya.
Hivi karibuni, wachungaji na waumini wa kanisa
hilo katika Jimbo la Mbeya walifunga lango kuu la kuingia makao yake
makuu na kusababisha polisi na Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Dk Norman Sigala
kuingilia kati.
Kutokana na mgogoro huo, Kamati ya Ulinzi na
Usalama ya wilaya hiyo, ilifanya kikao cha dharura na halmashauri ya
kanisa hilo na ilidokezwa kwamba walifikia mwafaka mzuri.
Hata hivyo, baada ya siku mbili kanisa hilo
liliwasimamisha kazi wachungaji watano ambao nao kupitia kwa wakili
walitoa siku saba kwa makamu mwenyekiti aliyeandika barua kuwarudisha
kazini haraka.
Hivi karibuni, askofu huyo kiongozi aliliambia
gazeti hili kwamba sababu za migogoro ndani ya kanisa lake ni utovu wa
nidhamu na watu wachache kutaka madaraka.
Source:Mwananchi.
Source:Mwananchi.
Comments