MAOMBI YAMUONDOA KWENYE KAZI YA KUHESABU MISUKULE


ATOKEA KWENYE CHUMBA CHA MZEE MSESENGE

Binti aliyefahamika kwa jina la Irene Danifit atokea kwenye chumba cha mzee Msesenge baada ya maombi yaliyo fanywa na mchungaji Frank Andrea wa kanisa la Ufufuo na Uzima Arusha. Anasema alikuwa anafanya kazi ya kuhesabu misukule wanao ingia katika chumba hicho kwa ajili ya kuwapeleka kwenye maeneo mbalimbali ya kichawi. Irine anasema alichukuliwa kichawi na babu aliye fahamika kwa jina la Msesenge. anasema alisikia NJOOOOOOOOOOOOOOO akajikuta ametoka kwenye chumba alicho kuwa amewekwa.

Huu ni ushuhuda kwa ufupi, tukipata kamili tutakuwekea hapa.

Mchungaji Frank Andrew akiwa na binti huyo.

Hapa akihojiwa kuhusiana na alikokuwa.

Baadhi ya umati wa watu uliofika kanisani hapo kwa maombi.©Ufufuo Crew.

Comments