BRANEA SPIRITUAL MINISTRY IMEKUANDALIA SEMINA KUBWA YA WANANDOA KATIKA KANISA LA SINZA CHRISTIAN CENTER - SINZA DAR ES SALAAM


Ndoa ni tatizo la Kitafa. Watu wengi wanalia kutokana na ndoa zao kutokuwa katika msimamo mzuri. Famila zinapotea na kujishtukia zinaingia katika vitendo vibaya kwa sababu ya mama na baba kutokuwa na maelewano mazuri. Wengine ndoa zao zinayumba kutokana na "Michepuko" . Inasikitisha sana kuona wanandoa hawa waliofunga ndoa kanisani na wakaahidi ya kuwa kifo ndicho kitakachowatenganisha, lakini leo wametengana kabla ya hicho kifo.

Branea Spiritual Family baada ya kuliona hilo ikaamua kuandaa semina kwaajili ya kuliweka sawa suala hili ili wanandoa hawa waishi maisha ya furaha na amani. Siku hiyo utajifunza mengi na kujua chanzo cha wanandoa kuvunja ndoa zao, madhara yake, ni jinsi gani ya kuepuka tatizo hili ambalo ni baya mbele za Mungu na mbele za wanandamu.

Semina hii ya kipekee itaongozwa na watumishi wa Mungu kama wanavyoonekana katika tangazo letu hapo chini. Usipange kukosa kabisa kwani baada ya somo utapata ujumbe kutoka kwa waimbaji kama vile Furaha Isaya, Hondwa Mathias, Madam Ruti, Grace Rwegasha na Magreth Sembuche. Rumafrica Online Tv itakuwepo kuhakikisha matukio yanarushwa online

Comments