NILIONA JINI JUU YA MTI NA KUTAKIWA KUUANGAMIZA HUO MTI.


Usidharau Ndoto Unayoota. Mwaka 2009 Nikiwa Zanzibar. Mimi Na Rafiki Zangu 4 Tulipanga Nyumba 1 Kwa Wakati 1. Baada Ya Kuanza Maisha Pale Majirani Walikua Wanatushangaa Na Tulipowauliza Wakasema Kwamba Nyumba Tuliyo Panga Huwa Haikaliwi Na Watu Maana Ina Nguvu Za Giza Za Hatari Sana, Hivyo Wanatushangaa Sana Na Siku Tunahamia Pale Tulikuta Godoro Na Vyombo Viko Nje, Tukaambiwa Vitu Hivyo Amevikimbia Mpangaji Mmoja Mpemba. Hatukuwa Na Wasiwasi Maana JEHOVAH Ndiye Mlinzi Wetu. Maisha Yaliendelea Kama Kawaida Na Baada Siku Chache Kabla Hata Ya Wiki Tangu Tuhamie Pale Niliota Ndoto Usiku Nikiona Miti Ya Machungwa Miwili Ambayo Iko Nje Ya Nyumba Yetu, Ndani Ya Mti 1 Ambao Ulikua Kushoto Nilimuona Njiwa Wa Kijani, Nikaambiwa Huyo Sio Njiwa Ila Ni Jini, Natakiwa Kesho Yake Niende Kwenye Huo Mti Na Kukata Ka Tawi Kadogo Sana Kisha Niombe Nikiuzunguka Huo Mti Nikisema " ENYI NGUVU ZA GIZA NAWATEKETEZA KWA JINA LA YESU KRISTO" Kweli Kesho Yake Nikafanya Kama Nilivyoelekezwa Ndotoni,Nikaomba Nikiuzunguka Ule Mti. Baada Ya Kuomba Niliendelea Na Kazi Zangu Kama Kawaida. Baada Ya Siku 2 Tangu Nivunje Nguvu Hizo Za Giza Kwenye Mti, Ule Mti Ulianza Kupukutika Majani Na Baada Ya Wiki Mti Mzima Ulikuwa Umekauka. Wenzangu Hawakujua Kinachoendelea, Baadae Kidogo Yule Mzee Baba Mwenye Nyumba Akaja Na Kuanza Kutukana Akisema Kuna Mtu Mbaya Kati Yetu Na Ambaye Ameharibu Vitu Vyake. Wenzangu Hawakujua Ila Siri Mimi Niliijua. Yule Mzee Alifanya Uchunguzi Wake Wa Kipepo Na Kugundua Ni Mimi Ndio Nimeua Vitu Vyake, Akawa Ananiogopa Sana Na Hata Kuniangalia Usoni Akawa Hawezi. Baadae Alianza Visa Akisema Kwamba Niache Kuweka CD Za Gospel Kwenye Redio Yangu Maana Zinamomonyoa Nyumba Yake. Pale Kama Kuna Mtu Alikua Analiza Redio Kwa Sauti Ndogo Basi Ni Mimi Lakini Mimi Huyo Huyo Ndio Nageuka Adui. Baada Ya Kodi Yangu Ya Chumba Kuisha Yule Mzee Alikataa Nisiongeze Kodi Bali Nihame Kwenye Nyumba Yake. Nikahama, Ndugu Yangu Usidharau Ndoto Unayoota Bali Husika Nayo Kwa Maombi Kwa Jina La YESU KRISTO.
Baadhi ya ndoto nazifahamu maana zake nitakuwa nakuletea ili ujue ufanyeje maombi.
Ubarikiwe.

  
 Kwenye Ndoto Ukiota Uko Barabarani Na Unaongozwa Na Askari Na Kuamrishwa Sehemu Ya Kwenda Na Ukakubali, Hiyo Ni Ndoto Mbaya, Maana Yake Adui Zako Wanakusimamia Na Kukuongoza Kila Mahali Kuhusu Mipango Yako. Haribu Mipango Hiyo Ya Uovu Kwa Kutumia Jina La YESU KRISTO, Kwenye Maombi Tumia Ufunuo 12:11, Zaburi 62:11-12, Yohana 8:36 Na Mathayo 12:37. Lakini Ukiona Kwenye Ndoto Unakataa Kuwatii Askari Mkiwa Barabarani, Hiyo Ni Ndoto Nzuri, MUNGU Anakupa Ushindi Juu Ya Maadui Zako, Mshukuru BWANA Na Endelea Na Maombi Ukitumia Zaburi 35 Na Zaburi 140. Lakini Ukiota Askari Mkiwa Barabarani Analazimisha Kwa Nguvu Nawe Ukamuua, Hiyo Nzuri, Una Nguvu Za MUNGU, Mshukuru MUNGU Na Endelea Na Maombi, Tumia Yakobo 4:7. BWANA YESU Anakupenda Sana Na Anakuwazia Mema Sana.


 Kwenye Ndoto Ukiota Unamuua Paka Ni Ndoto Nzuri. Maana Yake MUNGU Amekuwezesha Kuwafukuza Adui Zako, Mshukuru MUNGU Na Endelea Na Maombi Katika ROHO MTAKATIFU. Tumia Wafilipi 2:10:11

 Kwenye Ndoto Ukiota Unalima Jangwani, Hiyo Ni Mbaya, Maana Yake Biashara Unayoifanya Haitakupa Mahitaji Unayohitaji Katika Maisha Yako. Kataa Hali Hiyo Kwa Maombi Ya Vita Kupitia Jina La YESU KRISTO Ukitumia Mathayo 12:37, Isaya 41:10 Na Yeremia 15:21. MUNGU BABA Akubariki Sana Na BWANA YESU Anakupenda Sana, Songa Nae Tu Hadi Uzima Wa Milele.



Kwenye Ndoto Ukiota Mtu Anakupa Yai Lililopikwa, Ni Mbaya, Maana Yake Adui Zako Wamekutegea Mtego Mbele Yako Kwa Njia Ya Chakula, Unatakiwa Kuwa Mtulivu Na Kufunga Mdomo Wako Kwa Ajili Ya Kujilinda, Ondoa Hasira Na Ufunge Na Kuomba Kuharibu Mipango Hiyo Ya Maadaui Zako. Omba Maombi Ya Vita Ukitumia Waefeso 6:12, Yeremia 23:29, Mithali 18:21, Zaburi 50:15 Na Isaya 48:17. MUNGU Akubariki Sana Na BWANA YESU Anakupenda Sana, Songa Mbele Na Yeye Milele Yote.


Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. ROHO MTAKATIFU aliyenipa ujumbe huu ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA.
                     MUNGU akubariki sana .
                      Ni mimi ndugu yako
                       Peter M Mabula
                 Maisha ya Ushindi Ministry.
                           0714252292
                 MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili.
 MUNGU Akubariki.

Comments

MziziMkavu said…
Hi ni hadithi ya kutunga hongera kwa hadithi yako ya kutunga.
Peter Mabula said…
Siwezi kutunga ndugu