Skip to main content
NILIONA JINI JUU YA MTI NA KUTAKIWA KUUANGAMIZA HUO MTI.
 
  | 
  | 
Usidharau
 Ndoto Unayoota. Mwaka 2009 Nikiwa Zanzibar. Mimi Na Rafiki Zangu 4 
Tulipanga Nyumba 1 Kwa Wakati 1. Baada Ya Kuanza Maisha Pale Majirani 
Walikua Wanatushangaa Na Tulipowauliza Wakasema Kwamba Nyumba Tuliyo 
Panga Huwa Haikaliwi Na Watu Maana Ina Nguvu Za Giza Za Hatari Sana, 
Hivyo Wanatushangaa Sana Na Siku Tunahamia Pale Tulikuta Godoro Na 
Vyombo Viko Nje, Tukaambiwa Vitu Hivyo Amevikimbia
 Mpangaji Mmoja Mpemba. Hatukuwa Na Wasiwasi Maana JEHOVAH Ndiye Mlinzi 
Wetu. Maisha Yaliendelea Kama Kawaida Na Baada Siku Chache Kabla Hata Ya
 Wiki Tangu Tuhamie Pale Niliota Ndoto Usiku Nikiona Miti Ya Machungwa 
Miwili Ambayo Iko Nje Ya Nyumba Yetu, Ndani Ya Mti 1 Ambao Ulikua 
Kushoto Nilimuona Njiwa Wa Kijani, Nikaambiwa Huyo Sio Njiwa Ila Ni 
Jini, Natakiwa Kesho Yake Niende Kwenye Huo Mti Na Kukata Ka Tawi Kadogo
 Sana Kisha Niombe Nikiuzunguka Huo Mti Nikisema " ENYI NGUVU ZA GIZA 
NAWATEKETEZA KWA JINA LA YESU KRISTO" Kweli Kesho Yake Nikafanya Kama 
Nilivyoelekezwa Ndotoni,Nikaomba Nikiuzunguka Ule Mti. Baada Ya Kuomba 
Niliendelea Na Kazi Zangu Kama Kawaida. Baada Ya Siku 2 Tangu Nivunje 
Nguvu Hizo Za Giza Kwenye Mti, Ule Mti Ulianza Kupukutika Majani Na 
Baada Ya Wiki Mti Mzima Ulikuwa Umekauka. Wenzangu Hawakujua 
Kinachoendelea, Baadae Kidogo Yule Mzee Baba Mwenye Nyumba Akaja Na 
Kuanza Kutukana Akisema Kuna Mtu Mbaya Kati Yetu Na Ambaye Ameharibu 
Vitu Vyake. Wenzangu Hawakujua Ila Siri Mimi Niliijua. Yule Mzee 
Alifanya Uchunguzi Wake Wa Kipepo Na Kugundua Ni Mimi Ndio Nimeua Vitu 
Vyake, Akawa Ananiogopa Sana Na Hata Kuniangalia Usoni Akawa Hawezi. 
Baadae Alianza Visa Akisema Kwamba Niache Kuweka CD Za Gospel Kwenye 
Redio Yangu Maana Zinamomonyoa Nyumba Yake. Pale Kama Kuna Mtu Alikua 
Analiza Redio Kwa Sauti Ndogo Basi Ni Mimi Lakini Mimi Huyo Huyo Ndio 
Nageuka Adui. Baada Ya Kodi Yangu Ya Chumba Kuisha Yule Mzee Alikataa 
Nisiongeze Kodi Bali Nihame Kwenye Nyumba Yake. Nikahama, Ndugu Yangu 
Usidharau Ndoto Unayoota Bali Husika Nayo Kwa Maombi Kwa Jina La YESU 
KRISTO.
Baadhi ya ndoto nazifahamu maana zake nitakuwa nakuletea ili ujue ufanyeje maombi.
Ubarikiwe.
  
 Kwenye
 Ndoto Ukiota Uko Barabarani Na Unaongozwa Na Askari Na Kuamrishwa 
Sehemu Ya Kwenda Na Ukakubali, Hiyo Ni Ndoto Mbaya, Maana Yake Adui Zako
 Wanakusimamia Na Kukuongoza Kila Mahali Kuhusu Mipango Yako. Haribu 
Mipango Hiyo Ya Uovu Kwa Kutumia Jina La YESU KRISTO, Kwenye Maombi 
Tumia Ufunuo 12:11, Zaburi 62:11-12, Yohana 8:36 Na Mathayo 12:37. 
Lakini Ukiona Kwenye Ndoto Unakataa Kuwatii Askari Mkiwa
 Barabarani, Hiyo Ni Ndoto Nzuri, MUNGU Anakupa Ushindi Juu Ya Maadui 
Zako, Mshukuru BWANA Na Endelea Na Maombi Ukitumia Zaburi 35 Na Zaburi 
140. Lakini Ukiota Askari Mkiwa Barabarani  Analazimisha Kwa Nguvu Nawe 
Ukamuua, Hiyo Nzuri, Una Nguvu Za MUNGU, Mshukuru MUNGU Na Endelea Na 
Maombi, Tumia Yakobo 4:7. BWANA YESU Anakupenda Sana Na Anakuwazia Mema 
Sana.
 Kwenye
 Ndoto Ukiota Unamuua Paka Ni Ndoto Nzuri. Maana Yake MUNGU Amekuwezesha
 Kuwafukuza Adui Zako, Mshukuru MUNGU Na Endelea Na Maombi Katika ROHO 
MTAKATIFU. Tumia Wafilipi 2:10:11
 Kwenye
 Ndoto Ukiota Unalima Jangwani, Hiyo Ni Mbaya, Maana Yake Biashara 
Unayoifanya Haitakupa Mahitaji Unayohitaji Katika Maisha Yako. Kataa 
Hali Hiyo Kwa Maombi Ya Vita Kupitia Jina La YESU KRISTO Ukitumia 
Mathayo 12:37, Isaya 41:10 Na Yeremia 15:21. MUNGU BABA Akubariki Sana 
Na BWANA YESU Anakupenda Sana, Songa Nae Tu Hadi Uzima Wa Milele.
Kwenye
 Ndoto Ukiota Mtu Anakupa Yai Lililopikwa, Ni Mbaya, Maana Yake Adui 
Zako Wamekutegea Mtego Mbele Yako Kwa Njia Ya Chakula, Unatakiwa Kuwa 
Mtulivu Na Kufunga Mdomo Wako Kwa Ajili Ya Kujilinda, Ondoa Hasira Na 
Ufunge Na Kuomba Kuharibu Mipango Hiyo Ya Maadaui Zako. Omba Maombi Ya 
Vita Ukitumia Waefeso 6:12, Yeremia 23:29, Mithali 18:21, Zaburi 50:15 
Na Isaya 48:17. MUNGU Akubariki Sana Na BWANA YESU Anakupenda Sana, 
Songa Mbele Na Yeye Milele Yote.
Kwa sasa naishia hapo, 
MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea 
BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na 
atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu
 kwa mafundisho kanisani. ROHO MTAKATIFU aliyenipa ujumbe huu ana 
makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani 
aliko KRISTO BWANA.
                                            MUNGU akubariki sana .
                                              Ni mimi ndugu yako
                                                 Peter M Mabula
                                     Maisha ya Ushindi Ministry.
                                                    0714252292
                 MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili.
 MUNGU Akubariki.
 
 
 
 
 
 
 
  
 
 
 
 
 
Comments