MUNGU AMEKUSAMEHE WEWE VYOTE HIVYO NA WEWE WASAMEHE WATU YOTE.

Na Mwinjilisti John Chinyuli
Sijui hata nianze kulieleza vipi hili ambalo limeujaa moyo wangu ok wacha nianzie hapa ..........!
ninachotaka kusema ni kuwa asilimia 99 ya kizazi cha leo atamsamehe kila mtu hata aliyewahi kumvunja mkono lakini sio aliyewahi kumsaliti katika mapenzi, mimi sikatai alikupa jeraha kubwa kiasi gani na kukuacha na maumivu ambayo mpaka leo bado unayaugulia baada ya nafsi yako kukosa ile kitu ilikuwa inapenda lakini wewe je umemfanyia mangapi Mungu madudu,mambo ya ovyo lakini Mungu hata siku hajawahi kukufutilia mbali au akunyime oxygen hata kwa dakika 2 tu zaidi bado anakupenda sana akitumai ipo siku utabadilika.


sikia, unajichelewesha mwenyewe na kujizibia baraka zako mwenyewe ambazo Mungu alitaka akushushie haijarishi alikutendea nini, hivi ulishawahi kusoma andiko hili ..kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao ,na Baba wa mbinguni atawasamehe ninyi ''Mathayo 5:14''..vigezo na masharti kuzingatiwa je unataka Mungu akusamehe wewe? samehe kwanza wapenzi wako wa zamani mlio kwaluzana nao,maana utakapo achilia msamaha wa kweli kwa huyo aliye adui ndani ya moyo wako naye Mungu atakusamehe wewe na mtu akisamehewa na Mungu unakuwa rafiki wa Mungu mnakuwa mnaushirika mkiwa mnaushirikika na Mungu hakuna utakacho pungukiwa atakupatia zaidi ya vile ulivyokuwa unahitaji.

 Amua kuweka moyo wa msamaha ndugu yanini kuishi na maumivu kila siku yasiyoisha upate mwisho vidonda vya tumbo na inawezekana kabisa kusamehe Mungu wetu anaweza kila jambo mwambie akupe hiyo neema yakusamehe na kukuondolea uchungu utakonda bure mwenzio hana hata habari.

Utapata faida gani hivi ukianza kulipiza kisasi? leo hii tunasikia watu wanauana kwa sababu ya maumivu ya moyo(usaliti) na kujiingiza kwenye shida zaidi,  


Potelea mbali fuata usitarabu mwingine ndugu hebu yaishe yanini kila siku kutumiana mesages za matusi,unapoteza muda wako wa bure
Hapo ulipo hukutakiwa uwe ila kutokuwa na moyo wa msamaha ndio kumeshika kila jambo lako halisogei mbele,samehe na acha kuzungumzia tena habari hizo,halafu kumsamehe Mtu na kumaliza hayo magomvi siyo mpaka umwambie waweza kunyamaza tu actions speaks loud than words


Acha kuutesa moyo mpendwa,jipe raha mwenyewe,ushauri tu,ukitaka utumie kama unaona nimeandika pumba tupu endelea kufuata slogan zako,

karibu
  MUNGU akubariki sana.
 
                 By Mwinjilisti John Chinyuli 
                 0767 592989/0712 592989

Comments