KUOKOKA KUTAKUTOA KWENYE MAANGAMIZI YOTE, YA DUNIA NA YA JEHANAMU.


BWANA YESU asifiwe.
Karibu kula chakula cha uzima ambacho ni neno hai la MUNGU.
''Kwa maana jinsi hii MUNGU aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. - Yohana 3:16''
Upendo wa MUNGU ndio ulioleta Wokovu.
Wokovu unamhitaji kila mwanadamu atakayependa, Wokovu  wa YESU haulazimishwi ila ukiukataa jehanamu lazima uende.

WOKOVU Maana Yake Ni Kutoka Kwenye Hali Mbaya Na Kuja Kwenye Hali Nzuri. WOKOVU Ni Kuishi Maisha Ya Ushindi Dhidi Ya Dhambi. Watu Wengi Wako Kwenye Hali Mbaya, Hawataki Kuja Kwenye Hali Nzuri Yaani Kuja Kwenye Wokovu Huku Wakijua Kabisa Kwamba Wako Kwenye Hali Mbaya. Ni Heri Kutoka Dhambini Na Kuja Uzimani, Ni Heri Kutoka Kwa shetani Na Kuja Kwa YESU KRISTO.

Ndugu zangu kuna siku ya hukumu.Nayo imekaribia

 ''Kwa Maana Hiyo Siku Ya BWANA I Karibu Juu Ya Mataifa Yote; Kama Ulivyotenda, Ndivyo Utakavyotendewa; Malipo Yako Yatakurudia Juu Ya Kichwa Chako Mwenyewe-Obadia 1:15.''

 Heri Kung'ang'ania Kwa YESU Kuliko Kumkimbia shetani Ambaye Atakuchekea Wiki Ya Kwanza Harafu Wiki Inayofuata Anakuchinja Kama Kuku Ili Mkaishi Nae Jehanamu Milele.

 Kuna Watu YESU Akiwaita Leo Wanafyonza. Ndugu Yangu unayemkataa YESU leo Ipo Siku Utalia Na Kusaga Meno, Yaani Utasaga Meno Kwa Kulia Hadi Meno Yataisha Yote Na Bado Hujamaliza Kulia. Kitambo Kidogo Kuna Kuondoka, Usiishi Kama Hutaondoka Bali Ishi Ukijua Kwamba Kuna Kuondoka. Je Ukiondoka Utaenda Wapi? Ndiposa Leo Tunakuambia Kwamba YESU KRISTO Anaokoa, Ukimwamini Leo Unaokoka. Kataa Dhambi, Ogopa Dhambi, Ikimbie Dhambi Na Usifanye Dhambi. BWANA YESU Anakupenda Sana Na Anataka Uende Uzimani Aliko Yeye.
'' Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya MUNGU ni uzima wa milele katika KRISTO YESU BWANA  wetu. -Warumi 6:23''

 Hakuna Kutubu Baada Ya Kufa, Kama Una Mpango Wa Kutubu Basi Tubu Leo, YESU KRISTO Yuko Tayari Kukusamehe Kama Tu Wewe Ukiamua. Pombe Haitakufikisha Popote, Uzinzi Na Uasherati Hautakufikisha Popote, Uongo Na Upagani Hautakufikisha Popote, Wizi Na Na Matusi Hayatakufikisha Popote, Hata Dini Yako Bila YESU Ni Bure, Uchawi Wako Utakuangamiza Na Kumkataa YESU Ni Kukataa Uzima Wa Milele. Hata Leo YESU Anakuita Baba,mama, Kaka,dada, Vijana Na Wazee; Mpokeeni Tu BWANA YESU Ili Awape Uzima Wa Milele Bure.
BWANA YESU anasema 
 ''Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami. -Ufunuo 3:20''

Ndugu zangu watumishi wa MUNGU na wasio watumishi, wafanyakazi wa serikali na wasio wafanyakazi, wanandoa na wasio wanandoa, wababa na vijana wazee na mabinti, wamama na kila mtu 

'' Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote. -1 Yohana 1:9


- KWA VIJANA: "Ujana Ni Jalala" Msemo Huo Unawahusu Vijana Wasiookoka Maana Kila Anasa Mpya Na Mitindo Ya Kipepo Mipya Watahusika Nayo. Lakini Hata Wewe Kijana Uliyeokoka Usipomtii KRISTO Lazima Tu Utakuwa Jalala Kawa Wamataifa. Jalala Huingia Kila Uchafu, Poleni Sana Majalala, Sisi Tumeshasafishwa Kwa Damu Ya YESU.

- KWA WAIMBAJI: Uhusiano Wako Na MUNGU Ni Jambo Kubwa Mara 100 Kuliko Huduma Yako. Amka Wewe Usinziaye Unayedhani Utaenda Mbinguni Kwa Tiketi Ya Uimbaji Hata Kama Ni Mtenda Dhambi. Harafu Waimbaji Wengi Sio Wasikiza Mahubiri Na Wala Sio Waombaji, Tunamhitaji YESU Ili Tupone.

- KWA VIONGOZI WA SERIKALI: Mmepewa Kazi Hizo Ili Mtumike Na Sio Kutumikiwa, Sasa Kwanini Wote Mmegeuka Wa Kutumikiwa Badala Ya Kutumika? Hakika Mnamhitaji YESU Ili Mpone.

- KWA WANASIASA: Inawezekana Kabisa Ndio Mnaoongoza Kwa Kwenda Kwa Waganga Wa Kienyeji Ili Mchaguliwe, Lakini Pia Hamkawii Kupeleka Kero Za Wananchi Kwa Waganga Wa Kienyeji Na Hivyo Kuongeza Laana Na Umaskini Kwa Taifa. Mnamhitaji YESU anayeokoa na kuinua. Mnamhitaji YESU ili mpone.

 -KWA WALIMU: Poleni Na Majukumu Mema Ila Rabi YESU KRISTO Anawahitaji Kwenye Ufalme Wake, Kumpokea Ni Heshima Kuu Maana Yeye Ni MWALIMU Wa Waalimu.

- KWA ASKARI: YESU KRISTO Anaokoa, Ukiamini Leo Unaokoka.

- KWA MADAKTARI: Kataa Kusomea Dhambi Za Utoaji Mimba, Maana Mama Yako Angetoa Mimba Yako, Leo Hata Usingekuwa Daktari, Mche MUNGU Hata Kwenye Kazi Yako, Ni Heri Kuwa Daktari Wa Kupima Mafua Tu Kuliko Daktari Mtoa Mimba. MUNGU anakataa dhambi na hakikisha unaokoka ili uwe na maarifa ya kimungu.

- KWA WATUMISHI: Si Kila Karama Ni Yako Na Sio Kila Baraka Ni Yako. Mtoaji Ni ROHO MTAKATIFU Hivyo Usiwaseme Vibaya Wale Waliopewa Karama Tofauti Na Yako Au Waliopewa Karama Zaidi Ya Moja, Ukiwasema Vibaya Watumishi Wenzako Unazuia Watu Wasiokoke Tu Na Si Vinginevyo.

 -KWA WABABA: Mke Kuwa Msaidizi Wako Haina Maana Yeye Ni Ziada Tu Kwako, Ingekuwa Hivyo Basi Wewe Ungekua Na Macho 3 Na Pua 4 Lakini Vingi Ulivyonavyo Na Yeye Anavyo Na Wakati Mwingine Anaweza Kuwa Na Akili Kuliko Wewe, Kumtesa Au Kumwamlisha Kijeshi Kila Sekunde Itaharibu Ndoa Yako. Mwanamke Ameambiwa Amtii Mmewe Na Mume Ameambiwa Ampenda Mkewe. Kila Mmoja Atimize Wajibu Wake Kama MUNGU Atakavyo Na Liishini Neno La MUNGU Mtaishi.

- KWA WADADA: Kuangalia Vile Vinavyoonekana Kumewafanya Wadada Wengi Kuolewa Na Waume Wasio Sahihi Wanaowakataza Hata Kwenda Kanisani. Ni heri kumtii MUNGU katika yote.

- Kwa Wahubiri Wote: HAKIKISHA KRISTO ANAKUWA NENO NDANI YA KILA NENO UNALOHUBIRI.

Ukiitwa kwenye huduma changamka maana hizi ni zamani za uovu.
 ''Kwa sababu, ukimkiri YESU kwa kinywa chako ya kuwa ni BWANA, na kuamini moyoni mwako ya kuwa MUNGU alimfufua katika wafu, utaokoka. Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu. kwa kuwa, Kila atakayeliitia Jina la BWANA ataokoka. -Warumi 10:9-10,13''
 BWANA YESU Leo Anawaita Watu Wengi Sana Akisema "Njoni Mnifuate, Nami Nitawafanya Kuwa Wavuvi Wa Watu-Marko 1:17". Ndugu Ukiisikia Sauti Yake Acha Ya Dunia Na Mfuate YESU Ili Akawaokoe Makumi Elfu Kupitia Wewe.

 NENO Linapingwa Sana Lakini Kadri Linavyopingwa Ndivyo Linavyogusa Mioyo Ya Watu Na Kuwatengeneza Kwa Ajili Ya Ufalme Wa MUNGU. NENO Ni La MUNGU Na KRISTO Ni NENO Ndani Ya NENO.
 ''Amwaminiye Mwana(YESU) yuna uzima wa milele; asiyemwamini Mwana hataona uzima, bali ghadhabu ya MUNGU inamkalia. -Yohana 3:36''
Ndugu yangu mhitaji YESU leo na mtegee yeye tu 

Wachawi Wakikusumbua Washitaki Mbinguni Kwa YESU Uone Kitakachowapa. Kule Kuna Hukumu Nyingi Sana, Kuna Mchawi Mmoja Alikuwa Na Tabia Ya Kuwalaani Kanisa Hadharani, Aliposhitakiwa Mbinguni Mdomo Wake Ulipinda Kama Ndege Hata Kuongea Hawezi Tena.

Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. MUNGU ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA.
MUNGU akubariki sana .
Ni mimi ndugu yako
Peter M Mabula
Maisha ya Ushindi Ministry.
0714252292
mabula1986@gmail.com
MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili.
MUNGU Akubariki.

Comments