ILIVYOKUWA
Kwa mujibu wa shuhuda mmoja wa tukio hilo, wanafunzi wa shule hiyo wamekuwa wakisikia sauti za ajabuajabu shuleni hapo hali iliyokuwa ikiwafanya wasome kwa hofu. “Hali hiyo ilipozidi baadhi ya wanafunzi wakaenda kuwaambia wazazi wao ambao nao walipopeleleza kwa baadhi ya walimu walihakikishiwa kwamba ni kweli shuleni hapo kuna majini yanawasumbua wanafunzi na walimu pia,” alisema shuhuda huyo.
Ili kuwanusuru wanafunzi kutoka kwenye mauzauza hayo, wazazi waliweka
kikao cha dharura na kuamua kuandika barua kwenye ofisi za serikali ya
mtaa ili kuomba kibali cha kuitwa sangoma mkali, mwenye sifa, anayejua
majini, afike shuleni hapo kuyafukuza.Kwa mujibu wa shuhuda mmoja wa tukio hilo, wanafunzi wa shule hiyo wamekuwa wakisikia sauti za ajabuajabu shuleni hapo hali iliyokuwa ikiwafanya wasome kwa hofu. “Hali hiyo ilipozidi baadhi ya wanafunzi wakaenda kuwaambia wazazi wao ambao nao walipopeleleza kwa baadhi ya walimu walihakikishiwa kwamba ni kweli shuleni hapo kuna majini yanawasumbua wanafunzi na walimu pia,” alisema shuhuda huyo.
Ilidaiwa kuwa mauzauza ya shuleni hapo ni
wanafunzi wakienda chooni husikia vilio vya watoto wachanga au paka
lakini hawaonekani. Wakati mwimgine hupatwa na hali isiyoweza kuelezewa
kwa lugha sahihi.
SANGOMA ATINGA
Ikazidi kudaiwa kuwa, serikali ya mtaa japokuwa haiamini ushirikina, iliwaruhusu wazazi hao kutekeleza azma yao lakini serikali isihusike kwa lolote litakalotokea. Siku ilifika, sangoma huyo akaitwa, akiwa na wasaidizi wake wawili, alitia timu kwenye eneo hilo na kujigamba kuwa, tabu ya majini imekwisha! Yeye ndiye Lambalamba bwana!
ATAKIWA MBUZI MNONO
Habari zinasema kuwa, ili kazi ifanyike kwa ufanisi na kuweza kuleta tija na ili wanafunzi hao wampe tano kwa kazi, sangoma huyo alitaka mbuzi mnono kwa ajili ya kumchinja ili damu yake imwagikie eneo hilo na majini kukimbia.
HALI TETE
Ikazidi kudaiwa kuwa, wakati sangoma akisemasema maneno yake ya kufukiza, ghafla alianza kuyumbayumba mpaka kujikuta yupo chini kisha akatulia tuli licha ya wananchi, wakiwemo wanafunzi kumpigia makofi.
Ilibainika baadaye kwamba, sangoma huyo aliyekuwa amelala chali kama kwenye msalaba alikuwa amepoteza fahamu hivyo wasaidizi wake walianza kuhaha kwa kummwagia maji ndoo nzima ili azinduke kama siyo kurejea kwenye uhai wake (pichani).
CHA AJABU SASA
Cha ajabu sasa, sangoma akiwa hajitambui chini na wasaidizi wake wakiendelea kumzindua, msichana mmoja ambaye hakujulikana jina mara moja, alianza kupagawa, akaishiwa nguvu huku akisemasema maneno yasiyoeleweka, watu ‘waliokula chumvi nyingi’ wakasema amekumbwa na majini.
HALI YATULIA, ZOEZI LASITISHWA
Baada ya sangoma naye kuzinduka, zoezi la kuyatoa majini shuleni hapo lilisimama huku mikakati ikiwekwa kwamba shughuli hiyo itaendelea tena siku kadhaa mbele.
Naye Mwenyekiti wa Mtaa wa Kiluvya-Madukani, Adelaida Bruno alisema yeye alipelekewa barua ya maombi kutoka kwa wananchi wake wakimtaka awaruhusu kumuita sangoma kwa ajili ya kuwasaidia kuondoa mambo hayo ya mauzauza shuleni hapo. “Mimi kama serikali, hatuamini ushirikina, niliipokea hiyo barua, nikawaambia kama wamekubaliana kumwita sangoma kuwasaidia basi wafanye wao wenyewe. Na siku hiyo ya sangoma sikuhudhuria,” alisema mwenyekiti huyo.
MWALIMU MKUU ATUPIA KAMATI
Uwazi lilimtafuta mwalimu mkuu wa shule hiyo ambaye hakutaka kujitambulisha jina ambapo alisema siku ya tukio hakuwepo lakini alisikia kutoka kwa watu na kama ni ukweli utakuwepo kwenye kamati ya shule.
Chanzo:Global Publishers.
USHAURI WANGU WA BURE KWA WANAFUNZI, WALIMU NA WAZAZI.
Ukitaka majini yakutoke au yamtoke mwanao au mwanafunzi wako hakikisha unawafuata wahubiri ili waje waombe na uzima ulio katika jina la YESU KRISTO utashuka.
Hakuna hata mmoja anayeweza kuyatoa majini ila BWANA YESU.
YESU ni mzoefu wa kutoa mapepo na kila aina ya nguvu za giza alidhihilishwa ili kuzivunja kazi za shetani (1 Yohana 3:8b)
BIBLIA inasema
''Mtu wa kwenu amekuwa hawezi? Na awaite wazee wa kanisa; nao wamwombee, na kumpaka mafuta kwa jina la BWANA. Na kule kuomba kwa imani kutamwokoa mgonjwa yule, na BWANA atamwinua; hata ikiwa amefanya dhambi, atasamehewa. Ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi, na kuombeana, mpate kuponywa. Kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana, akiomba kwa bidii. -Yakobo 5:14-16''
''akawaambia, Kwamba utaisikiza kwa bidii sauti ya BWANA, MUNGU wako, na kuyafanya yaliyoelekea mbele zake, na kutega masikio usikie maagizo yake, na kuzishika amri zake, mimi sitatia juu yako maradhi yo yote niliyowatia Wamisri; kwa kuwa Mimi ndimi BWANA nikuponyaye. -kUTOKA 15:26''
''Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo; watasema kwa lugha mpya; watashika nyoka; hata wakinywa kitu cha kufisha, hakitawadhuru kabisa; wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapata afya. -Marko 16:17-18''
NDUGU ZANGU UKITAKA MAPEPO YATOKE KWA MPENDWA WAKO HAKIKISHA UNAKIMBILIA KWENYE MAOMBEZI KANISANI.
Comments