UJUE UMUHIMU WA KUPEWA ROHO MTAKATIFU NDANI YAKO ILI AKUONGOZE.

Na Emmanuel Kamalamo.

Bwana Yesu asifiwe.

Nipenda kukushukuru wewe ambaye umekuwa ukifuatana nami katika masomo nayoweka mahari hapa, lengo nikuta kulijenga kanisa ambalo ni mwili wa Kristo.

Kila mkristo anamsikia ROHO MTAKATIFU anapotajwa katika sala, lakini kusudi la Mungu anataka akaye ndani yako ili awe kiongozi katika maisha yako.Maandiko yanasema...Yohana 16:13 " Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote.."
Kama kusudi la Roho Mtakatifu nikutaka tuijue "KWELI" Neno linasema.."NAYE ROHO NDIYE ASHUHUDIAYE, KWA SABABU ROHO NDIYE KWELI" 1 Yohana 5:7. Kama Roho Mtakatifu anataka kukupa ukweli basi ujue kuna"UONGO" uliopo duniani ambao shetani anaweka ili awapoteshe watu wasilijue Neno na wasijue mapenzi ya Mungu.
Pia Roho Mtakatifu ni muumbaji maana alishiriki katika kuiumba dunia na mwanadamu.Mwanzo 1:26 " Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, sura yetu. (mfano huo ni hari ya kutokuwa na dhambi, na pia kuwa katika utukufu)
Ayubu 33:4 "Roho ya Mungu imeniumba,Na pumzi ya za mwenyezi hunipa uhai.


ROHO MTAKATIFU NI NANI?

Roho Mtakatifu ni NAFSI ya tatu ya Mungu katika Mungu mmojo.
1 Yohana 5:8 "Kwa maana wako watatu washuhudiao [mbinguni, Baba, Neno, na Roho Mtakatifu na watatu hawa umoja.
Nafasi ya "NENO" ni Yesu Kristo..."Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli.
Yohana 1:14.
Ndiyo maana Neno linatwambia Mungu ni Roho nao wamwabduo yeye imewapasa kumwabudu katika ROHO NA KWELI.

UMUHIMU WA KUPEWA ROHO.
JAMBO LA 1.
~KUKUSAIDIA KUMKARIBIA. BABA KATIKA KUMWABUDU.
Waefeso 2:18 " Kwa maana kwa yeye sisi sote tumepata njia ya kumkaribia Baba katika Roho.
Angalia lile neno " kwa yeye" maana yake ni hii, Umzungumziwa Yesu ambaye ukimpoke moyoni mwako anakupa ROHO MTAKATIFU atakayekupa uwezo na mbinu za kumkaribia Mungu. Ndiyo maana maandiko yanasema..BALI WOTE WALIOMPOKEA ALIWAPA UWEZO WA KUFANYIKA WATOTO WA MUNGU.." Yohana 1:12.
Kama hujaokoka yaani hujampokea Yesu moyoni mwako na kuzaliwa mara ya pili ujue haumkaribii Mungu kumwabudu, niulize kwa nini?....sikia nikwambie, anaye kuwezesha KUMWABUDU MUNGU NI ROHO MTAKATIFU. Sikia nikwambie bwana kama ndani yako hujafanyika kuwa HEKARU LA ROHO MTAKATIFU hata ukienda kanisani kwako kuabudu uwe na uhakia hajamkaribia Mungu aliye hai.
Maandiko yanasema.." Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli. Yohana 4:24 .
Roho ni roho yako maana imeandkwa herufi ndogo, na kweli ni Roho mwenyewe. Kwa mantiki hiyo kama roho yako imeokoka unapewa USHIRIKA NA ROHO MTAKATIFU ndani yako na huyo Roho anakuweza kumkaribia Mungu ili kumwabudu. Na kama hujaokoka huwezi kuwa na USHIRIKA NA ROHO MTAKATIFU na kama huna ushirika na Roho Mtakatifu kuabudu kwako kunakuwa bure maana wewe si wa Mungu, si mimi nimesema kasome Biblia yako uwe na uhakia utaambiwa...." LAKINI MTU AWAYE YOTE ASIYEKUWA NA ROHO WA KRISTO, HUYO SI WAKE" Warumi 8: 9.

Tunaendelea...
KAMA HUJAOKOKA OKOKA LEO
BAADA YA KUFA NI HIKUMU.
Waebrania 9:27.

MUNGU WANGU AKUBARIKI.
By  Emmanuel Kamalamo.

Comments