AJIFANYIAYE MARAFIKI WENGI NI KWA UANGAMIVU WAKE MWENYEWE

Na mwinjilisti John Chinyuli.
''Ajifanyiaye marafiki wengi ni kwa UANGAMIVU wake mwenyewe'' Mithali 18:24b
Nadhani ushawahi kukutana na watu wa jinsi hii au labda ni wewe mwenyewe kila mtu ni rafiki yako fulani ni rafiki yako na fulani naye ni rafiki yako na yule fulani ni rafiki yako uko sawa kabisa na ni vizuri kuwa na marafiki,na si vivema kuwa adui na watu,naomba unielewe vizuri kuwa sijasema mtu kuwa na marafiki ni vibaya la hasha
Nadahani kila mmoja wetu anafahamu maana ya rafiki ni mtu wa karibu ambaye mnakuwa mnamahusiano naye ya ndani sana,urafiki pia ni Agano baida ya watu wawili,waswahili wakasema rafiki ni zaidi ya ndugu.
Unajua mnaweza mkawa na mahusiano mazuri na watu na si mpaka wawe rafiki zako mkawa mmeelewa na ikaishia hapo,si kila mtu mpaka awe rafiki yako,tuendelee utanielewa tu

Ndiposa maandiko matakatifu yanatueleza kuwa ajifanyiaye marafiki wengi ni kwa uangamivu wake mwenyewe Mithali 18:24b,na maneno ya Mungu ndiyo kweli yote,ajifanyiaye au anayewatafuta mwenyewe au anaye watengeneza mwenyewe au nayejitafutia marafiki wengi ni kwa uangamivu wake mwenyewe au hujiangamiza mwenyewe,na kila siku huwa nakwambia kuwa Mungu huwa anatumia watu na shetani naye huwa anatumia watu hao hao
Unajua unapokuwa una marafiki wengi basi bora hao marafiki wawe wa maana wanaweza wakakusogeza mahali au utajifunza jambo kutoka kwao au hao marafiki ulio nao wengi ni Mungu awe amekukutanisha nao na uwe na uhakika kabisa kuwa urafiki wenu chanzo ni Mungu maana yake akiwa Mungu amekufanyia hao marafiki na si wewe lazima nyuma yake kutakuwa kuna agenda nzuri
Lakini sasa hao marafiki ambao umewatafuta mwenyewe tena wengi wao ndani yao hawajaamua kuishi maisha ya kumpendeza Mungu na sote tunajua kama mtu yeyote ambaye hajaamua kuishi maisha ya kumpendeza Mungu shetani aweza kumtumia vizuri tu kutekeleza agenda zake,na shetani hanaga jema na mtu wala huruma na mtu
Lengo lake ni kuweka uharibifu na vilio tu kwenye maisha ya mtu yeyote,sikia si vibaya kuwa na urafiki na mtu ambaye haeleweki lakini uwe na uhakika huo urafiki Mungu kaamua uwepo(kaufanya mwenyewe) labda lengo lake kupitia wewe huyo naye abadilike lakini vinginevyo utakuwa unajiaangamiza mwenyewe
Hebu jaribu kufikilia shetani akampa kila rafiki yako Agenda ya kuja kukuangamiza au kukuwekea uharibu kwenye maisha yako au kukukwamisha kwa namna yoyote ile,na sote tunajua agenda za shetani si tu ikija utajua hii ni agenda ya shetani na hi ni ya Mungu si rahisi kiivo,sasa swali langu je utaweza kila agenda utakayoletewa na rafiki yako kuitambua kuwa hii ni agenda ya shetani na kuipinga,
Ukaipinga agenda ya rafiki yako wakwanza aliyoileta kwako aliyopewa na shetani akaja na mwingine na mwingine na mwingine na mwingine ili hali hawa watu ni rafiki zako watu ambao mna mahusiano ya karibu tena hawa rafiki ni wewe uliyejitafutia,sijui kama umeshawahi kujiuliza kati ya rafiki ulio nao je ni wangapi ambao mpo rafiki kwa mapenzi ya Mungu na wangapi rafiki zako ni kwa mapenzi ya shetani wala Mungu hahusiki hapo
Hii shida hasa ipo kwa dada zangu hawa kila mtu ni rafiki yake wamepeana na namba za simu,hebu sasa fikiria nusu ya rafiki zake wote wakaanza kumtongoza na rafiki alio nao robo tatu ni wavulana,swali langu Je huyu dada ataweza kumwambia kila rafiki yake hapana ili hali hawa ni watu wa karibu yake ana mahusiano nao sana,ni ngumu sana waulize kina dada watakusimulia juu ya hili,mimi nimewahi kuulinzwa na kuobwa ushauri sana na kina dada
Utamkuta dada analalamika yeye anatongonzwa sana kila mtu anamtongoza mimi huwa nawaambia wao ndio wana matatizo haiwezekani tu from no where mtu akaanza kukutongoza wako wadada wazuri wangapi hivi mbona hawatongozwi hovyo,huwa nawaambia wao ndio wamewafungulia mlango na matokeo yake vishawishi vinawashinda na kuangukia pua kwenye uasherati,Ajifanyiaye marafiki wengi ni kwa uangamivu wake mwenyewe,unajiangamiza mwenyewe tu
Sikiliza nikwambie Yesu mwenyewe alikuwa na wanafunzi(marafiki) wengi sana lakini kati ya wale aliwachagua 12 tu wakuwa nao karibu lakini hakuishia hapo kati ya wale 12 alichagua wengine 3 wakuwa nao karibu sana na kuongozana naye kila mahali,sembuse sisi
Unajua unaweza ukawa na marafiki wengi kweli kweli na ni jambo nzuri kabisa lakini shetani akatumia hao marafiki zako mnaishai kusemana na kupigana vijembe ninyi kwa ninyi,huyu akikutana na huyu anampiga vijembe huyu na fulani naye akikutana na fulani wanampiga vijembe fulani shetani akawavuruga kweli kweli,ni heli kuwa na marafiki na mahusiano ya karibu sana na watu wachache wa maana
Ukajitengenezea marafiki lundo siku ya siku mnakuja kufarakana nao wote wanakuja kuwa maadui lundo na kujisababishia matatizo na uangamivu maishani mwako maana bora uwe na adui tu from no where kuliko adui aliyewahi kuwa rafiki yako,ukaanza kusema ooh ili nifakiwe nahitaji marafiki lakini ili nifanikiwe zaidi nahitaji maadui utakuwa unajidanganya rafiki maana hao maadui uliwatengeneza mwenyewe na wala sio shetani maana wewe ndio ulijikusanyia marafiki lundo na si Mungu alikukutanisha na hao marafiki
Unajua mimi nilipojifunza hili jambo nikaenda hata kwenye Phonebook yangu na kuanza kufuatilia jina moja baada jingine fulani je ana manufaa na umuhimu wowote kwangu ananijenga kipi kama hana maana nikawa nadelete,kwa leo niishie hapa
AJIFANYIAYE MARAFIKI WENGI NI KWA UANGAMIVU WAKE MWENYEWE
chinyulimwinjilisti@gmail.com

Comments