MAMBO MANNE MUHIMU KWA WATEULE WA MUNGU.

BWANA YESU atukuzwe ndugu.
Karibu kwenye maarifa ya uzima.
 2 Kor 4:1 ''Mtu na atuhesabu hivi, kuwa tu watumishi wa KRISTO, na mawakili wa siri za MUNGU. ''
Wateule wa BWANA YESU ni mawakili wa siri za MUNGU.
Wateule wa MUNGU ni watumishi wa KRISTO.
Kama mtumishi wa MUNGU na wakili wa siri za MUNGU lazima ujiweke kiutumishi na kuwa na utii mkuu kwa BWANA YESU aliyekuita ili umtumikie.
 2 Kor 4:1 ''Kwa sababu hiyo, kwa kuwa tuna huduma hii, kwa jinsi tulivyopata rehema, hatulegei;''
Mtumishi wa KRISTO lazima uzingatie yafuatayo;

1.  HAKIKISHA UNAKUWA MWOMBAJI.  

''Nanyi mkiomba lo lote kwa jina langu, hilo nitalifanya, ili BABA atukuzwe ndani ya Mwana. Mkiniomba neno lo lote kwa jina langu, nitalifanya.-Yohana 14:13-14.
Waombaji Hubeba Siri Za MUNGU, Waombaji Hupokea Ufunuo Kutoka Kwa MUNGU, Waombaji Hupokea Maono Kutoka Kwa MUNGU, Waombaji hupokea neno la ufunuo kwa ajili ya kanisa au huduma zao, Waombaji lazima wakae na neno na MUNGU. Wakolosai 3:16 -17 '' Neno la KRISTO na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia MUNGU kwa neema mioyoni mwenu. Na kila mfanyalo, kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la BWANA YESU, mkimshukuru MUNGU Baba kwa yeye. ''. 
Ndugu zangu, utumishi ni huduma hivyo 
Lazima Ulinde Huduma Uliyopewa Na MUNGU. 
Linda huduma yako kwa maombi.

2.  USILEGEE.
 
2 Kor 4:1 ''Kwa sababu hiyo, kwa kuwa tuna huduma hii, kwa jinsi tulivyopata rehema, hatulegei;''
 -Usilegee Kwenye Huduma Yako, 
-Usilegee Kuomba, 
-Usilegee Kumtolea MUNGU, 
-Usilegee Kumwabudu MUNGU.

3.   KATAA MAMBO YA AIBU .

  2 Kor 4:2-3 ''lakini tumekataa mambo ya aibu yaliyositirika, wala hatuenendi kwa hila, wala kulichanganya neno la MUNGU na uongo; bali kwa kuidhihirisha iliyo kweli twajionyesha kuwa na haki, dhamiri za watu zikitushuhudia mbele za MUNGU. Lakini ikiwa injili yetu imesitirika, imesitirika kwa hao wanaopotea;'' 
-Mambo Ya Aibu Ni Matendo Yaliyojificha, 
-Ni Matendo Yanayotendeka Gizani, 
-Ni Matendo Ya Mwilini.  
2 Kor 4:6 '' Kwa kuwa MUNGU, aliyesema, Nuru itang'aa toka gizani, ndiye aliyeng'aa mioyoni mwetu, atupe nuru ya elimu ya utukufu wa MUNGU katika uso wa YESU KRISTO''
-Ndugu Yangu Hujaokolewa Kwenda Mbinguni Bali Umeokolewa Kwenda Duniani Kuhakikisha Ndugu Na Marafiki Zako Wote Wanaokoka, Ungeokolewa Kwenda Mbinguni Ungekuwa Umeshaondoka Lakini Umeokoka Uende Duniani, Mbinguni Utaenda Tu Maana Ni Haki Yako.


 -Watu Wengi Wanafanya Mambo Ambayo Yako Kinyume Cha MUNGU Kwa Sababu Ya Upungufu Wa Imani. Ndugu Yangu Palilia Amani Yako, Ng'oa Vichaka Vinavyoizunguka Imani Yako, Ng'oa Mizizi Ya Miti Inayonyonya Imani Yako.

4. PALILIA IMANI YAKO.

 TUNAPALILIA IMANI KWA 
 -Kusoma Neno La MUNGU, 
-Kwa Maombi, 
-Kwa Kumsifu MUNGU 
-Kumwabudu MUNGU, 
-Kujumuika Na Watakatifu, 
-Kumsikiliza ROHO MTAKATIFU, 
-Kumtii KRISTO 
-Na Kutenda Kazi Ya MUNGU. 

Ndugu Yangu, Ilinde Imani Yako, Ipalilie Imani Yako, Tengeneza Imani, Jenga Imani Yako, Nenda Kwa Imani Mathayo 17:20 '' YESU akawaambia, Kwa sababu ya upungufu wa imani yenu. Kwa maana, amin, nawaambia, Mkiwa na imani kiasi cha punje ya haradali mtauambia mlima huu, Ondoka hapa uende kule; nao utaondoka; wala halitakuwako neno lisilowezekana kwenu. ''

 5. HAKIKISHA UWEPO WA MUNGU UPO PAMOJA NA WEWE.

Musa kama mmoja wa watumishi wa MUNGU aliona haiwezekani kutumikayaani kuwa mchungaji kwa waisraeli  bila uwepo wa MUNGU. Ndugu zangu MUNGU Sio Demokrasia Ya Watu Wote, MUNGU Hushughulika Na Mtu Mmoja Binafsi anayeamua kumtii na kumpokea BWANA YESU na kulitii neno lake.

Ukitaka Kubarikiwa 
-Acha Ya Aibu. 
-Hakikisha Huduma Yako Inafanya Kazi, 
-Hakikisha Unajua Huduma Yako, 
-Lazima Tulinde Huduma Zetu. 
-Jihadhari Kuchangia Utukufu Wa MUNGU. 

KWANINI UNATAKIWA KUACHA MAOVU. 

MUNGU Anajua Moyo Wako Zaburi 44:21 ''Je! MUNGU hatalichunguza neno hilo? Maana ndiye azijuaye siri za moyo. ''. 

ILI UFANIKIWE FANYA YAFUATAYO.

-Omba Maombi Ya Kukataa Kutumiwa Na Shetani, 
-Kataa Kutumikishwa Na Dunia, 
-Omba Kuinuliwa. 
-Ruhusu MUNGU Achunguze Moyo Wako Zaburi 139:1-4 ''Ee BWANA, umenichunguza na kunijua. Wewe wajua kuketi kwangu na kuondoka kwangu; Umelifahamu wazo langu tokea mbali.  Umepepeta kwenda kwangu na kulala kwangu, Umeelewa na njia zangu zote.  Maana hamna neno ulimini mwangu Usilolijua kabisa, BWANA. '', MUNGU anakuwazia mema sana Yeremia 29:11 '' Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema BWANA, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho. ''. 
-Mruhusu MUNGU Aingilie Mambo Yako, 
MUNGU Huingilia Maisha Yako Kwa Wewe Kumpokea YESU KRISTO. 
Kumbuka Baraka Za MUNGU Hazitakuja Maishani Mwako Kama Huna YESU KRISTO Maishani Mwako. 2 Timotheo 2:16-19 '' Jiepushe na maneno yasiyo na maana, ambayo si ya dini; kwa kuwa wataendelea zaidi katika maovu, na neno lao litaenea kama donda-ndugu. Miongoni mwa hao wamo Himenayo na Fileto, walioikosa ile kweli, wakisema ya kwamba kiyama imekwisha kuwapo, hata kuipindua imani ya watu kadha wa kadha. Lakini msingi wa MUNGU ulio imara umesimama, wenye muhuri hii, BWANA awajua walio wake. Na tena, Kila alitajaye jina la BWANA na auache uovu. ''.
 Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani.
ROHO MTAKATIFU aliyenipa ujumbe huu ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA.
MUNGU akubariki sana
Ni mimi ndugu yako katika BWANA YESU.
Peter M Mabula
Maisha ya ushindi Ministry.
0714252292
Bali wote waliompokea(YESU KRISTO) aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa MUNGU, ndio wale waliaminio jina lake; -Yohana 1:12

Comments