Mwimbaji maarufu wa kundi la Joyous Celebrations afariki dunia katika Ajali mpiga Drums alazwa Hospital


Majonzi yameigubika familia ya kundi maarufu la Joyous Celebration la nchini Afrika ya kusini, baada ya mwimbaji wao wa sauti ya kwanza mahiri wa muda mrefu aitwaye Lihle Mbanjwa kufariki dunia katika ajali mbaya ya gari binafsi waliyokuwa wakisafiria huku pia mpiga ngoma (drums) maarufu wa kundi hilo Siyabulela Satsha aliyekuwemo katika gari hilo akijeruhiwa kichwani na kulazwa hospitali.
Marehemu Lihle Mbanjwa akiimba kwa hisia katika tour ya 17 ya kundi hilo, mwaka jana.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na kundi hilo, imesema ajali hiyo imetokea mapema siku ya jana jumapili, ambapo ndani ya gari hilo pia alikuwemo ndugu wa marehemu ambaye pia amelazwa hospitali pamoja na Sabu kwa matibabu zaidi. 
Siyabulela akicharaza ngoma.

Marehemu Lihle ambaye alifunga ndoa mapema mwaka huu na bwana Busie Shozi
  alikuwa mmoja kati ya waimbaji nyota kwa upande wa sauti ya kwanza, hali iliyomfanya kushirikishwa katika kanda za waimbaji mbalimbali akiwemo malkia wa muziki wa injili Rebecca Malope, Ntokozo Mbambo, Nqubeko Mbatha na wengineo.
Marehemu Lhile Mbanjwa wa kwanza kushoto mstari wa pili, akiimba kwa hisia katika onyesho lao la jumamosi iliyopita huko Kimberley Afrika ya kusini.

Mwimbaji huyo pia aliweza kuongoza wimbo katika rewind DVD ya 1 ya nyimbo za zamani za kundi hilo akiwa sambamba na mwanakaka Xolani Mdlalose, huku pia akianzisha wimbo katika DVD ya 15 part 1. 
Lihle akiwa na Ntokozo, Hlengiwe pamoja na Kuki ambao kwa pamoja wanaimba bendi ya Ntokozo na Nqubeko kama waitikiaji.
Lihle alikuwa na urafiki wa karibu sana na waimbaji waliomaliza mkataba na Joyous akiwemo Duduzile, Mahalia, Ntokozo, Hlengiwe, Brenda ilifikia mpaka wakataka kuanzisha mfuko wa pamoja wa kuwasaidia watu wenye shida. Kundi hilo limepatwa na msiba ikiwa jumamosi walifanya onyesho huko Kimberley, wiki hii wakitarajiwa kuelekea nchini Swaziland kabla ya kuelekea nchini Kenya tarehe 14 kwa onyesho lingine.

source:Gospelkitaa



Comments